Hazchem plate
JF-Expert Member
- Feb 25, 2011
- 11,059
- 15,530
Hauna tofauti na Sharif majini
Asante kutukumbushani maneno ya Mhubiri1:1 Mhubiri: Kiebrania: Kohelethi.mwana wa Daudi, aliyekuwa mfalme huko Yerusalemu.
2Bure kabisa, bure kabisa,
nakuambia mimi Mhubiri!
Kila kitu ni bure kabisa!
3Binadamu hufaidi nini
kwa jasho lake lote hapa duniani?
4Kizazi chapita na kingine chaja,
lakini dunia yadumu daima.
5Jua lachomoza na kutua;
laharakisha kwenda machweoni.
6Upepo wavuma kusini,
wazunguka hadi kaskazini.
Wavuma na kuvuma tena,
warudia mzunguko wake daima.
7Mito yote hutiririkia baharini,
lakini bahari kamwe haijai;
huko ambako mito hutiririkia
ndiko huko inakotoka tena.
8Mambo yote husababisha uchovu,
uchovu mkubwa usioelezeka.
Jicho halichoki kuona,
wala sikio kusikia.
9Yaliyokuwako ndio yatakayokuwako,
yaliyotendeka ndio yatakayotendeka;
duniani hakuna jambo jipya.
10Watu husema, “Tazama jambo jipya,”
kumbe lilikwisha kuwako zama za kale.
11Hakuna mtu anayekumbuka ya zamani
wala atakayekumbuka yatakayotukia baadaye.
Aliyoyaona Mhubiri
12Mimi Mhubiri, nilikuwa mfalme wa Israeli, huko Yerusalemu. 13Nilipania kuchunguza na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachotukia duniani. Hiyo ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu.
14Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: Ni sawa na kufukuza upepo!
15Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa,
kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa.
16Basi, nikatafakari nikisema, “Nimejipatia hekima nyingi zaidi kupita wote waliopata kutawala Yerusalemu kabla yangu. Naam, nina uzoefu wa hekima na maarifa.”
17Nilipania kubainisha kati ya hekima, wazimu na upumbavu. Lakini niligundua kwamba kufanya hivyo ni sawa na kufukuza upepo.
18Maana katika kuwa na hekima nyingi mna wasiwasi;
na aongezaye maarifa zaidi huongeza huzuni zaidi
Utamkimbiza[emoji4] [emoji4]100% abdnormal man,hakuna ujiniasi apo.but we are about to find out
An intrepid Eskimo leaves his igloo and travels 12 kilometers north, 12 kilometers east and 12 kilometers north again to reach the North Pole. How many kilometers does he have to travel to return to his igloo in a straight line?
answer please
Celta vgo ameshashinda 2. Genius naomba utoke ulipo jfcha popote ulpo[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]hahaha bado matokeo ya atalanta na certa vigo...atupendi ujinga asee
Kama alichoelezea si chai, basi angalau maelezo yako haya mkuu yana msingi flani wa hali ya huyo mdau.Ni maajabu ulipozaliwa ulicheka badala ya kulia, uliza watu nani alicheka alipozaliwa. Sishangai Atheists wote wana vituko na wengi wao ni genius. Formula zote za kisayansi ni watu kama wewe. Huenda una nguvu ya pekee usiyoijua lakini una jicho la tatu linalofanya kazi kwa ufasaha. Au unaishi katika ulimwengu wa roho
Umenifanya nicheke. Kweli watu mnajua kutumia fursaFanya hvyo ndg yangu
Briton v new castle
Getafe v Villarreal
Eibar v Celta Vigo
Fiorentina v Atalanta
Strasbourg v Nantes Yani hao tu sio lazima uweke MATOKEO yote kama sijui 1-0au 3-0 we weka tu Brighton v Newcastle (kama away win ) inatosha then tukianzia HAPO tutakuelewa vzr
Kama alichoelezea si chai, basi maelezo yako haya mkuu angalau yanafafanua vizuri hali ya Hugo mdauNi maajabu ulipozaliwa ulicheka badala ya kulia, uliza watu nani alicheka alipozaliwa. Sishangai Atheists wote wana vituko na wengi wao ni genius. Formula zote za kisayansi ni watu kama wewe. Huenda una nguvu ya pekee usiyoijua lakini una jicho la tatu linalofanya kazi kwa ufasaha. Au unaishi katika ulimwengu wa roho
Tumetumia fulsa lakn uo utabir unatutokea puani aiseeeKama alichoelezea si chai, basi maelezo yako haya mkuu angalau yanafafanua vizuri hali ya Hugo mdau
Hiyo ni katika kurahisisha tu uandishi..guys be great thinkers!Mbona sasa umekosea kuandika bachelor kama hukoseagi?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23], mawazo yako ni hatari sana, ,,.Unamaana Unajua ni nani alimshambilia Tundu Lissu.??
Maana yake ukimuona mtu unajua anawaza nini.?
Tusaidie mkuu
Itakuwa..!!!!Kirikuu nn?
Kirukuu Mkuu..!!!kama unajua kusoma mawazo ya mtu..niambie nilikuwa nataka nisemaje kabla sijatype hapa
Mkuu, usisahau kutupatia mrejeshoNimelipa 10,000/nangoja return
Kitendo cha kuwa na bachala tuuu badala ya bachelor au bachela inaonyesha kuwa wewe ni Juma ki...la...zaHi members, nitaanza kwa kujitambulisha hapa chini kabla ya kwenda kwenye mada kamili.
Jina: Free ideas(Not official)
Umri:29yrs
Elimu:Shahada
Kabila:Kanda ya ziwa
Familia: Married with 2 kids
Kiufupi nimesoma 0-A level hapa Tanzania kisha nikaenda nje ya nchi(Europe) kuchukua Bachala.
Binafsi kuna hali inanitokea hua mpaka mwenyewe nashindwa kujielewa kama ni kwangu tu ama hata kwa watu wengine, lakini kila nikijaribu kumsimulia mtu kuhusu yanayonitokea hua ananishangaa na kuona kwamba mimi sio mtu wa kawaida.
Nitaeleza japo kwa ufupi hapa chini kuhusu hali hiyo.
1. Nikiwa bado nasoma(primary), sikuwahi kakaa n kujisomea iwe wakati wa mitihani ala la!, kuna wamwaka niliugua mapunye(mashilingi)kichwani nikakaa nyumbani miez 10 nikaenda shule baada ya kupona mwezi wa 11.Week iliyofuata kukawa na mitihani ya kufunga shule kuingia darasa la sita.
Nilifanya mtihani ule bila maadalizi yoyote na kuna walimu walitaka nisiwanye mtihani kwa sababu sikuwepo almost mwaka mzima.Nikalia sana wakaniacha nikafanya.Matokea yalipotoka nikawa mtu wa pili (2) kati ya watu mia moja thelethini na nane( 138.) Mwalimu mkuu aliniita akitak nimwambie kama nilipewa mtihani na mwalimu yeyote , lakini aligundua kwamba sikupewa mtihani.
.
.
2. Napenda sana kukaa mwenyewe na hua nikiwa mwenyewe najikuta naongeaongea na wakati mwingine kucheka mwenyewe.Pia mama yangu aliponizaa anasema kwanza hakusikia uchungu wa uzazi kabisa.Pia nilipozaliwa tu nilicheka badala ya kulia kama watoto wengine.Nikiwa na miaka 3 nikikua na uwezo wa kusoma bila kukosea.
.
.
3. Nikiota kitu ndotoni hua haipiti siku tatu kinatokea kweli.Mwezi ulopita niliota nimepata ajali ya kugongana na bajaji kisha nikaumia kichwani.Baada ya siku mbili nilipata ajali kweli na nikaumia kwenye paji la uso.Hata rangi ya bajaji niliyoota ilikua nyekundu na kweli bajaji ilikua nyekundu.
.
.
4. Nina uwezo wa kujua mgeni gani atanitembelea nyumbani kwangu na kweli mgeni huyo atakuja.Wakati mwingine mke wangu hua anaogopa ninapomwambia leo atakuja mgeni kavaa nguo flani na atakuja kwa shida flani.Nilitabili mama yake mzazi atakuja mwezi flani na akakuja na mtoto mdogo na watakua wamevaa hibi na kweli ikawa hivyo.
.
.
5. Kuna siku nilikua mahala nimekaa vichakani kama kawaida yangu kukaa mwenyewe, nikahisi kuna nyuka mweusi nyuma yangu katokea shimoni.Nilichofanya ni kuinuka taratibu kusonga mbele na kweli ile nageuka nakuta nyoka mweusi.
.
.
6. Mwaka mmoja kabla ya babu wa Loliondo nikiwa nje ya nchi nilimwambia jamaa yangu kwamba mwakani kuna mtu ataibuka maarufu kwa kusema anatibu ukimwi tanzania na atapata watu wengi.Kweli ikawa jamaa yangu mpaka leo anaamini mimi ni ndugu yake huyo babu na kwamba nilijua paln zake.
.
.
7. Nikiwa masomoni nje ya nchi sijawahi kukaa na kujisomea zaidi ya kuangalia movie za ki-Intelejensia na documentary za sayansi lakini hakuna mzungu hata mmoja amewahi kunipita darasani ama kwenye presentation, nimekua nikifanya vizur sana.Baadhi ya presentation zangu na machapisho yangu naskia zinatumiwa chuoni hapo na walimu.(lecturers)
.
.
8. Ninaweza kujua kwamba week ijayo nitaumwa na kulazwa kwa siku kadhaa.Pia naweza kujua nitaumwa ugonjwa gani ama malaria ngapi na hata nikipimwa hua ni kweli idadi ile ile.Mwezi ulipita nilimwambia wife nimewaza kua nitaumia mguu mlangoni, nakweli nikaumia mguu na mpaka sasa sijapona vizuri.
.
.
9. Ninauwezo mkubwa sana wa kutumia computer kufanya kazi.
Naweza kuchapa kwa kasi sana bila kukosea hata herufi moja.Naweza kutatua tatizo la computer lililowashinda mafundi japo sijasoma kabisa maswala ya computer.
.
.
11. Naweza kujua mawazo ya mtu hasa kabla hajaongea hata kama ni mara ha kwanza kuonana nae.Lakini pia naweza kujua kama mtu anasema uongo ama ukweli.Mke wangu akiniaga anakwenda sehemu hua najua anakwenda wapi na muda atakaorudi najua au kama kuna dharura atapata hua najua.
.
.
12. Ninaweza kuongea lugha tano za kimataifa(tofauti na kiswahili na kiingereza) kwa ufasaha lakini sijafanya kozi ya lugha hata moja kati ya hizo.Lugha hizo ni pamoja na kifaransa, kijerumani, kichina, kihispania, kihindi na kiarabu.Nimejifunza kupitia simu ya mkononi.
.
.
13. Sipendi kabisa habari za Dini na maswala yamuhusuyo mungu(mimi ni Atheist) na hua najickia vibaya sana kujadili maswala hayo.Ninaamini hakuna mungu.Pia sina ushabiki wa vitu vinavyopendwa na watu wengi mfano mpira ama siasa.
.
.
14. Napenda kukaa sana vijijini (japo kwa sasa niko mjini sababu ya kazi)na kufanya kazi huko, sipendi kuajiliwa na wala sifurahii kabisa kulipwa mshahara na mtu mwingine.Napenda pia kuzunguka zunguka sehemu zenye mito ama maji yanayotiririka na kuyaangalia huku nikijiongelea mwenyewe.
.
.
15. Kuna mwaka flani nilikua kijijini eneo la mto akili ikanituma niangalie juu ghafla kikashuka kitu kizito sana kutoka angani kama jiwe kubwa, baada ya kutua chini ghafla kitu kile kikageuka ndege mzuri na sijawahi kuona ndege wa aina kama ile tena mpaka leo.Ndege yule aliruka ruka kunizunguka kisha akapaa kurrudi angani vertically. Cha ajabu sikuogopa kabisa hali ile.
.
.
16. Tangu nizaliwe nimefanya mapenzi kwa mara ya kwanza nikiwa na mke wangu.I mean sikuwahi kufanya mapenzi hapo kabla sijaoa.Katika kipindi hicho chote sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke yaani kutamani kufanya sex.
.
.
17. Tangu niwe na akili timamu sijawahi kutoa chozi kwa maana ya kulia.Hata misibani nikienda hua naona ni hali ya kawaida na napenda sana kuishika maiti hasa kichwani.Wakati mwingine hua naomba nioshe maiti iliradi niishike kichwa tu kisha nami najishika kichwa halafu naondoka msibani.
.
.
18. Napenda harufu mbaya sana.Nikipita mahali kuna mzoga naweza kumaliza nusu saa hapo navuta harufu mpaka tumbo hua linajaa.Nikimuona mtu analia ama yuko kwenye huzuni mimi hua nafsi inafarijika na napenda kumwangalia huku natabasamu.
.
.
19. Sina hasira hata mtu akiniudhi namna gani.Hua nacheka na kutabasamu muda wote.Kuna baadhi ya ndugu wanadhani mimi ninamatatizo ya kiakili.
.
.
20. Nikiwa kazini hua ninatumia muda mwingi kufanya kazi za wafanyakazi wenzangu maana zangu hua namaliza kabla ya saa 3 asubuhi.Ofisini tunapangiwa kazi za siku husika hivyo mimi namaliza mapema hata kama kazi ngumu na kisha huwasaidia wengine karibu wote.Kufika sa sita kazi zote zimekwisha.Boss wangu hua ananipa majukumu hata yasiyo yangu (ya kwake)lakini nayafanya kwa haraka na kwa usahihi kabisa.
.
.
21. Sikuwahi kujifunza koz yoyote ya udereva lakini ninaendesha gari aina zote kwa ufasaha.Ninaweza kutumia mitambo mbali mbali hata kama ni mara ya kwanza kuuona.
Mwisho:
Hali hii inaniletea usumbufu sana kwa kua wengine wananitafrisi vibaya kutokana na tabia zangu.
Nimeleta hapa nipate ushauri wenu na kama kuna yeyote ambaye hali kama hii inamtokea nipate kujua kama ni tatizo ama ni kawaida.
.....Free ideas.......