kenethedmund
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 347
- 89
Kwa siku za hivi karibuni wote tumeshuhudia ccm wanavyohujumu mchakato wa kupata Katiba ya Tanzania kwa Watanzania. Ni jambo la ajabu kwa asieelewa pale wapinzani walivyo anza kulalamika kuanzia mchakato wa awali wa kupata katiba mpya ulivyoonesha ccm watakuwa na wajumbe wengi kuliko taasisi na vyama vingine vya upinzani kwamba kunahatarisha na kunaweza kupatikana katiba ya ccm ni si ya wananchi. Jambo ambalo kwa sasa ndilo linalojidhihirisha na hata pale walivyolalamika kuhusu kanuni kuvunjwa na kuanza kwa Jaji Warioba kuwakilisha rasimu ya pili ya katiba kabla ya rais kufungua bunge la katiba kuna ambao walisema wana wasiwasi tu, lakini ndilo lililotokea matokeo yake rais alienda kupiga kampeni ya serikali mbili na kuligawa bunge na kujibu hotuba ya Jaji Warioba na kwenda mbali zaidi kwa kuwadhalilisha tume ya katiba ingawa maoni hayakuwa ya kwao bali ni ya wananchi. Na sasa kuna la kura ya siri na ya wazi, wote tunajua wajumbe wengi ni wa chama cha ccm ambao wameshaelezwa hawatakubaliana na rasimu ya pili ya katiba, na wanajua kuwa kuna wabunge wengi wa ccm ambao wanaweza kupiga kura kinyume na misimamo ya chama cha ccm ndio maana wanawashinikiza kupiga kura ya wazi ili waiteke demokrasia ya wajumbe. Jambo hili halikubaliki ni bora ccm waachwe watengeneze katiba yao badala ya kutuvurugia mchakato na kuharibu fedha za wananchi kwa kulazimisha wanayotaka wao. Ni bora wajumbe wote wasiokubaliana na hili ikibidi waufahamishe umma wa watanzania ili tutoke kama taifa na kupinga jambo hili ovu. Huu mchakato umetumia fedha nyingi sana za wananchi hatutakubali kuacha itikadi za kichama kuingilia mchakato huu.