Kwa dalili hizi, hakuna Katiba Mpya!

Kwa dalili hizi, hakuna Katiba Mpya!

hatma yetu iko mikononi mwa wazanzibar. unajua huku bara kuna mbumbumbu wengi mno aka bora liende
 
Kabla ya Hotuba ya Rais kikwete Bunge lilionekana kama kuanza kupata suluhu ya kuendesha mambo kwa muafaka zaidi na hali ya utulivu ilianza kujitokeza.

Lakini baada ya Hotuba ya Warioba wanaccm wengi wakaonekana kuhamaki na kumtaka rais badala ya kutoa hotuba ya kufungua Bunge, amjibu Warioba kipengele kwa kipengele. Licha ya wachambuzi wa mambo kumuonya rais kutokufanya hivyo, rais alionekana kukubaliana na maoni ya baadhi wa wanachama wake na kwenda kuijadili hotuba ya warioba na kusisitiza msimamo wa chama chake.

Si hayo tu bali alijaribu kuonesha kuwa CCM wako wengi na wanaweza kuibadilisha rasimu yote na kwamba haiwezekanai watoke wapige kampeni ya nguvu rasimu ishindwe kupita!

Kuanzia hapo wajumbe wa CCM ndani ya Bunge la katiba wakaanza kuvunja ile misingi ya maridhiano kwa kuanza kufanya mambo ya hila na yanayoashiria kutumia uwingi wao kulimiliki Bunge maalumu. Mwenyekiti wa Bunge naye akaonekana kubadili msismamo wake wa kubalance uwakilishi ndani ya kamati mbali mbali za bunge. Yeye mwenyewe alijitapa baada ya rais kuhutubia kwamba atahakikisha anabalance kamati na majadiliano ili makundi mbalimbali yaweze kuwakilishwa.

Gafla amebadilika na kushindwa kutimiza ahadi yake kwa kigezo kwamba CCM ni wengi kwa hiyo lazima wadhibiti maeneo yote kwa sababu ndio hali halisi wanannchi walivyoamua. Kwanza hao CCM waliojazana huko bunge la katiba walichaguliwa na wananchi lini na wapi kwenda kuwawakilisha kwenye bunge la katiba? La pili, mbona tulivyoweka utaratibu wa kubalance gender hatukusema wananchi ndio waliamua kuwachagua wanaume kwa hivyo tuache ilivyo? Je Sitta anamini kabisa bila kubalance kamati zake kuna kitachoendelea? Moja ya hasara za kujaza CCM wengi ni kwamba kila jambo litakoletwa litatiliwa mashaka na upande mwingine.

Cha ajabu basi, ni kwamba badala ya hotuba ya Kikwete kuongeza mshikamano na maridhiano na kutoa dira ya namna ya kuvumiliana imekoleza hisia za uchama na ubabe wa tupo wengi. Na hii ndio maana wengi wakasema Kikwete alikwenda kuvunja bunge maalumu na sio kulizindua. Pinda mwnyewe amedhihirisha hili kwa kuonesha wasiwasi kwamba hakuna uwezekano wa kufikia maridhiano kuendana na hali ilivyo kwa sasa na bunge litaahirishwa!

Lawama zote kwa Kikwete, alionywa hakusikia! Nadhani pia mapigo ya Waznazibar ameanza kuyapata! yangu macho!

All comedians, We the laughing stock!!!
 
Tangu rais ahutubie bunge la katiba wenye akili tulijua ndio kikomo cha bunge.

Kama bunge la katiba likivunjwa ama kuahirishwa kwa namna yeyote ile wa kulaumiwa ni JK.
 
hakuna raisi hovyo kama kikwete aliyewahi tokea tz
 
Yote haya sababu ya UKAWA. Wakati akina Lissu, Jussa na Abubakar walipokuwa kwenye kamati ya Kanuni, mambo yalitulia kwa vile wao walikuwa sehemu ya watendaji wa abunge Maalum. Wamemaliza kutunga kanuni sasa wameanza vurugu. Hakika UKAWA ndo tatizo
 
Mtaelewa tu japo kwa shida na gharama ya wengine ila somo litaeleweka kuwa nchi ni ya Watu na sio ya vyama !!!!!!
M only sad sababu kuna wazee watapoteza heshima zao kwa hili!!!!
 
Wewe siku zote huna hoja. Kazi ya kupiga debe tu mambo ya akina Mbowe
 
Hakika. Serikali tatu ni ushetani kama ulivyotolea mfano huo

Laiti ungeelewa hiyo sentensi yangu usingekurupuka kuichangia..........haya tuambie kati ya HIRIZI, ROZARI na TASBIHI kipi TANGANYIKA, ZANZIBAR na TANZANIA? :eyebrows::eyebrows::eyebrows:
 
Raisi asiyeona mbali. Sasa Wazenji wanataka chama chao cha ASP na Nchi yao. Mtu alipewa nafasi ya kutoa maoni kabla akasema rasimu iko poa. Mwishoni anasema kwa rasimu hii nchi itapinduliwa. Feki kabisa.
 
Back
Top Bottom