Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Sawa, sasa hoja yako ni nini?
UKAWA wanakwamisha mchakato wa Katiba Mpya!
Sawa, sasa hoja yako ni nini?
Jenga hoja kwa kuzingatia utaifa, yani uepuke kuwagawa wana jf na pengine wananchi kwa misingi ya kisiasa.
UKAWA wanakwamisha mchakato wa Katiba Mpya!
Sidhani kama nimewagawa wanaJF/Wananchi, labda uniambie nimewagawaje!
CCM wamechoka na amani kutokana na ulevi wa madaraka wanayojihakikishia kwa ubabe utokanao na ujinga wa Watanzania na udhaifu wa katiba.
Inasikitisha sana kuona waziri mkuu naye anaanza kwenda kwenye media ku campaign uuuu mawazo yake. Eti waziri asipokuwa mbunge hatakuwa responsive kwa matatizo ya wananchi. Hivi TTTanznia inaongozwa nna system yaa aina gani ?
UKAWA ni nini? Je, unapowapakazia ukawa kua wanakwamisha mchakato huoni kua wananchi wanagawanyika kwa wengine kuwaamini na wengine kuwachukia?
1. UKAWA ni nini?
2. Lengo lake ni nini?
3. Thibitisha usemacho kua wanakwamisha mchakato.
Sidhani kama hujui UKAWA kiasi kwamba unahitaji maelezo toka kwangu! Nishauri kama kundi fulani likifanya jambo fulani lisilopendeza, kwa ufahamu wangu, liachwe tu kwa kuhofia "kuwagawa" wananchi?
1. Walivyopanga kumzomea Rais?
2. Wanavyokataa vyeo kwenye kamati?
3. Wanapotishia kujitoa kwenye mchakato wa kuandaa Katiba Mpya?
Sasa mkuu, mimi nakuachia jukwaa uendelee na majukumu ya kuitumikia jf lakini fikiria upya kuhusu kauli unazozitoa humu. Alamsiki.
Mkuu, kwa kawaida sina utamaduni wa kubishana kwa kutumia hoja za nguvu. Tuishie hapa kwa leo tena kwa nia njema kabisa ya kutoleta mfarakano miongoni mwetu wana jf.
Jamani tuwe tunajadili kwa uhuru na watu tusioshabihiana mawazo na ndio maana tuko hapa Jukwaani!
Kuna watu ukitoa mawazo yako basi utaitwa majina yote sababu kuu ikiwa ni kwamba umetoa hoja wasiyoikubali!
Tunafanya yale yale ambayo Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanavyofanya, huku tukiwa busy kwenye simu/keyboards kuwalaumu! Tujibu hoja kwa hoja na si kususa kama wengine wafanyavyo!
hakuna matarajio ya kupata katiba mpya tutegemee kupata katiba ya kiccm
Kumradhi kwa kukutoa nje ya mjadala, naomba uniwekee nukuu niliyokutaja majina.
Halafu ningependa ieleweke tu kua sijasusia hizo unazoziita hoja zako hadi ukanilinganisha na hao wabunge, kawaida yangu hua napenda sana kujadili na watu ninaotofautiana nao kimtazamo na fikra ila kwa kutumia nguvu za hoja na ikitokea zikaanza kutumika hoja za nguvu hua naendelea kua msikilizaji/msomaji zaidi.