Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 6,376
- 6,720
Kazi za bunge lolote duniani ni kuisimamia na kuishauri serikali kwa niaba ya wananchi,
Pili, ni kufanya kazi kwa niaba ya wananchi,
Bunge hutoa amri kwa serikali na siyo serikali kutoa amri kwake,
Tatu, bunge hutunga sheria kwa mujibu wa matakwa ya wananchi ambao ndiyo wenye mamlaka,
Nne, bunge lina madaraka yaliyokasimishwa kwake na wananchi.
Je Bunge linapokosa kufanya hayo juu, bado linakuwa na hadhi na haki ya kuwa bunge hata kuitwa bunge?
Je Bunge la tanzania siyo chombo cha ajabu na hovyo ambacho serikali tena watu wachache wanaweza kutumia kubaariki uchafu wao?
Je kwa uhovyo huu, bado watanzania wana sababu ya kuendelea kuliheshimu na kuliamini hili bunge?
Je bado kodi za wananchi zinahitajika kuendelea kulipwa kwa kodi zao wakati limewekwa nyumba ndogo na watu wachache?
Je unamuonaje spika wa bunge ambaye ameonyesha wazi kuwa kifaa na nyumba ndogo ya serikali?
Je rais na mawaziri wako juu ya bunge?
Ongeza nawe mapendekezo yako.