Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago!

Kuzorota uchumi: Stone Block wafungasha virago!

Hii nchi inaenda pabaya. Nyie mnaoshadadia kufa kwa biashara mnasahau kuwa licha ya kodi kuna ajira na trickle-down economics at play ambayo husaidia watu wengi sana kuliko mnavyofikiria. Sasa hivi watu hawajengi kwa kuwa hawana hela. Matokeo cement haiuziki, wafanyakazi wanapunguzwa, kodi hazilipwi, pensions funds hazipati mapato, mikopo benki hailipiki, vibarua hakuna, mama ntilie hawapati wateja, matumizi ya nishati ya umeme, gesi n.k imeshuka, watoto wanaondolewa mashuleni, walimu na staff wa shule wanapunguzwa n.k. Athari hasi ni kubwa kuliko mnavyotaka kujiaminisha. Acheni kutetea upuuzi, this is not how you lead a country and especially not how you govern an economy.
 
Mh raisi anafanya kazi kubwa mno wanyonyaji wameanza kukimbia tumechoka kuibiwa na wageni nchi yetu n tajiri
Ndio yake yale ya machinga wa South Africa kudai madaktari kutoka Zimbabwe wanachukua kazi za wazawa. Akiondoka huyo daktari huyo machinga atatibu? Unanyonywa nini usichonacho? Nafikiri tu nje ya boksi
 
Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.

Sawa fanyeni basi nyie wana chato..mnakosa mpaka hela ya kulipa mshahara wafanyakazi.maninaaaa
 
Ni kweli, hili ndilo lilikuwa the biggest shop la Vifaa vya ujenzi along Old Bagamoyo Rd. Count jobloss, revenues loss, aftersale services loss, tenancy loss, quality products loss, etc, etc, Magufuli anaua!.
P
Do we really need investors on building materials?
It is higt time for Tanzanian's to awake.
This is the time for many of you to learn all this kind of businesses the booming time is closer.
Stop complaining, get ready and prepare your selves by aquiring knowledge.
 
Wajinga ndivyo mnavyo amini. Lakini ukweli ni kwamba Nchi imeangamia tayari. Pamoja na cement kushuka sana kote Nchini, lakini ujenzi umesimama na hakuna dalili za kufufuka hivi karibuni. Wachina mmoja mmoja wanaondoka. Mwisho mtabaki masikini watupu mnatazamana huku mkisifiana ujinga.
Pole sana mwerevu wewe! Wasalimie misukule wenzako. Unga mnaokula ukiisha wekeni tangazo la kuomba michango humu, tutawachangia.
Pathetic Nincompoop!
 
Ruhusu akili yako ifikirie kwa upande wa pili.
Nchi zetu kumbuka kuwa serikali hazina msaada wowote kwa wafanya biashara.
Hasa kwenye suala la mitaj.

Mtu anahangaika anapata kamtaji halafu kabla hata hajafungua bishara tayari ameshaletewa bili ya kodi anazodaiwa.

Ingekua kufanya biashara nu rahisi mashirika ya umma yasingekufa.

Hata watu binafsi wanahujumiwa na kuibiwa na wafanyakazi wao. Na hasara nyingi tu wanazipata kila siku ndio maana serikali makini inawalinda sana wafanyabiashara wake kwa mara nyingine kuwasamehe kodi hizi ndogo ndogo na hata kuwapa mitaji yenye riba nafuu sana.
Kutoa ruzuku kwa wale wafanyabiashara walioajiri zaidi ya watu 50.
Kuwatafutia masoko.

Sio kila siku kupandisha kodi tu na kuzuia mzunguko wa fedha .
LIPA KODI msukule wewe.
Acha kulialia kama binti wa darasa la kwanza aliyepoteza hela ya ashkirimu.
 
Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.
Hoja ya kipuuzi kwelikweli. OK! Kama walikuwa wanafanya kwa ujanjaujanja ni kitu kibaya. Sasa unaambiwa biashara ni mbaya, hakuna wateja. Watu hawana fedha za kununua vitu. Hawana "nguvu za kiume" aka fedha. Sasa kampuni ibaki inalipa kodi bila kufanya biashara? Na bado. Mtajuta kuijaribu sumu kwa kuilamba!
 
Kama walikuwa wanaingiza bidhaa kwa kukwepa kidi imekula kwao. Wafungashe tu. Watanzania hawana pa kwenda wataendelea kubangaiza. Tumeshzoea kupata faida kidogo na maisha yanaendelea.
 
Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.

Pointi ya maana sana hii. Na watu kufunga biashara kwa sababu ya kushindwa kuendesha kwa faida si jambo geni. Ndio msingi hasa wa mfumo wa kibepari. Mwenye nguvu umpishe.
 
Ukweli ni upi mkuu!?
Wewe unafahamu ya kwamba kuna watu walikuwa wanaingiza 20ft container ambayo thamani ya mzigo ulio ndani kiuhalisia Kodi yake kwa mfano ilitakiwe ilipwe Tsh 22,000,000/- ...lakini wajanja hao walifanya manuva na ujanja huo mzigo unatoka kwa ushuru wa Tsh 6,000,000/-. Na bado anauza kwa faida kubwa sana. Au suala kama hili wewe unalizungumziaje?
Kwahiyo dawa ya watu hao ni kuwafungia biashara zao? Ndio kodi italipwa stahiki sivyo???

Awamu hii inayajua matatizo yanaoikabili nchi lakini haijui dawa yake wala namna (approach) ya kuyaondosha hayo matatizo. Tuli- exaggerate mno udhaifu wa awamu zilizopita which is very wrong kwenye administration yoyote.
 
Hii nchi inaenda pabaya. Nyie mnaoshadadia kufa kwa biashara mnasahau kuwa licha ya kodi kuna ajira na trickle-down economics at play ambayo husaidia watu wengi sana kuliko mnavyofikiria. Sasa hivi watu hawajengi kwa kuwa hawana hela. Matokeo cement haiuziki, wafanyakazi wanapunguzwa, kodi hazilipwi, pensions funds hazipati mapato, mikopo benki hailipiki, vibarua hakuna, mama ntilie hawapati wateja, matumizi ya nishati ya umeme, gesi n.k imeshuka, watoto wanaondolewa mashuleni, walimu na staff wa shule wanapunguzwa n.k. Athari hasi ni kubwa kuliko mnavyotaka kujiaminisha. Acheni kutetea upuuzi, this is not how you lead a country and especially not how you govern an economy.

Asante.

Bahati mbaya watz wamekaririshwa kuwa cha muhimu ni serikali kupata kodi. Tumedanganyika kuwa serikali ikipata hela kibao, basi hizo hela zitamnufaisha mwananchi mmoja mmoja directly. Ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho mahali popote duniani. Hata nchi zinazojitahidi sana katika hili (social welfare), kama zile za scandinavia na uarabuni, bado kipato halisi cha mwananchi kinatokana na huyo mwananchi kuwa na ajira yake au kabiashara kanakompatia faida. Unapouwa ajira na biashara kwa kuweka mkakati wa kukusanya kodi kupitiliza, vipato vinapungua, biashara zinakufa, ajira zinatoweka na hata hiyo kodi unayotafuta inapungua. Ni sawa na yule mtu anayekata tawi alilokalia.
 
Kama walikuwa wamezoea kufanya biashara kiujanja ujanja na kukwepa Kodi hayo ndio matokeo na madhara yake mkuu. Suala la msingi pia inabidi uelewe ya kwamba sekta ya ujenzi haiko vizuri kwa sasa. Sababu mafisadi yamesimamisha ujenzi na majizi yako chini ya ulinzi.
Sawa haya ni mawazo yako yanaweza kuwa kweli au yakawa ya kudhania tu
 
Namna muhimu ya serikali kuongeza mapato yake bila kuathiri uchumi, ni kuanza kwa kuongeza ufanisi wa TRA. TRA, inakusanya 11% ya GDP kama mapato ya serikali. Nchi zikizoendelea sana, hiki kiwango kinafika mpaka 30%. Wakenya nadhani wanafika 18%. Ufanisi wa TRA ni mdogo sana na hata huo ufanisi unatokana na kukata kodi za customs, kodi ambayo ni rahisi mno kuadminister. Ukienda kwenye kodi za mapato ya ndani (income tax, vat, etc) utakuta wanacheza. Nilishangaa sana pale niliposikia halmashauri zimenyanganywa kazi ya ukusanyaji kodi ya majengo na kazi hiyo kupewa TRA. Haki nakuambia, kuna siku itakuja kugunduliwa kuwa halmashauri zilikuwa na ufanisi mkubwa zaidi kuliko TRA.
 
Ukweli ni upi mkuu!?
Wewe unafahamu ya kwamba kuna watu walikuwa wanaingiza 20ft container ambayo thamani ya mzigo ulio ndani kiuhalisia Kodi yake kwa mfano ilitakiwe ilipwe Tsh 22,000,000/- ...lakini wajanja hao walifanya manuva na ujanja huo mzigo unatoka kwa ushuru wa Tsh 6,000,000/-. Na bado anauza kwa faida kubwa sana. Au suala kama hili wewe unalizungumziaje?
Kwa hiyo wakilipa kodi stahiki hawapati faida!nadhani bado kuna mahala pana shida tu
 
Nimepata habari "wamepigwa" vibaya tokea NEMC hadi kodi za ajabu ajabu.
Nyie endeleeni na nyimbo zisizo na mashiko, wenye kwao wanasepa!
Wewe pia unalalamikia serikali ya CCM?

Hiyo ndio kunyoosha nchi Jidu.
Rais wa wanyonge anawanyonga wanyonge wake.
 
Do we really need investors on building materials?
It is higt time for Tanzanian's to awake.
This is the time for many of you to learn all this kind of businesses the booming time is closer.
Stop complaining, get ready and prepare your selves by aquiring knowledge.

Do you belive that nationals wont be subject to the same vagaries that face these foreigners? Havent you seen businesses belonging to nationals also folding under the misguided pressure fromTRA, NEMC, TFDA, and the plethora of other government agencies. Did you hear the one about the businessman who commited suicide because of the sudden ban imposed on his stock of legally acquired inventory of alcoholic sachettes?

Do you think that all those businesses that are defaulting on bank repayments (to the extent of endangering the banking sector) are foreigners?
 
Back
Top Bottom