PostGE2025 Kuzimwa kwa Intaneti wakati wa uchaguzi wa 2025, kuliumiza wengi, haki ya kupata taarifa iliminywa

PostGE2025 Kuzimwa kwa Intaneti wakati wa uchaguzi wa 2025, kuliumiza wengi, haki ya kupata taarifa iliminywa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Joined
Apr 1, 2017
Posts
16
Reaction score
25
Tarehe 29 Oktoba 2025, Tanzania iliingia kizani kimawasiliano baada ya Mamlaka kuzima Mtandao wa intaneti (internet), upande wa pili Serikali ikidai kufanya hivyo kumeweza kuwadhibiti waandamanaji kuhamasishana kuandamana.

Kuzimwa kwa Mtandao kulisababisha madhara mengi kwa Wananchi ikiwa pamoja na kukosa taarifa za kinachoendelea kuhusu uchaguzi na kipekee maandamano. Katiba ya Tanzania inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kupata taarifa, hilo lipo Kisheria na linatakiwa kutimizwa na Mamlaka zote zinazoongoza Wananchi.
Screenshot 2025-12-19 005954.jpg
Tarehe 29 majira ya Saa Tano baada ya video ya maandamano katika eneo la Kimara muda huohuo mtandao ulizimwa.

Wachambuzi wa siasa nchini wamesema Mtandao ungeruhusiwa hamasa ingekuwa kubwa na maandamano ya Gen Z yangepamba moto nchi mzima.

Dickson Kabigumila, kupitia ukurusa wake wa Facebook, amesema kuwa kizimwa kwa mtandao ni kwenda kinyume na katiba ibara ya 18 na 20.


Naye Mohammed Kilobo amesema kuwa kuzimwa kwa mtandao kumerejesha nyuma hamasa ya waandamanaji "Waandamanaji walikuwa wakiona wenzao wa Kimara washakinukisha basi nao wanahamisika lakini baadaye mtandao ulivyozimwa hamasa ilikatika"
Tanzania-Communications-Regulatory-Authority-TCRA.jpg

Uchunguzi wa Mwandishi wa Habari hizi umebaini kuwa maandamano yalipata nguvu baada ya video kadhaa kusambaa Mtandaoni na baada ya mtandao kuzimwa hamasa ya maandamano yalififia kwa kiasi fulani kwa kuwa hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu kinachoendelea.

Vijana (Gen Z) wa Dar es Salaam, Mbeya, Arusha wangeweza kuhamasisha wengine wa mikoa mingine na kungepelekea maandamano hayo kuenea nchini kote.

Hoja ya kwamba kuzimwa kwa mtandao kumewarejesha nyuma waandamanaji iliungwa mkono na Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya ndani na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kombo alipohojiwa na Vyombo vya Habari vya Kimataifa ikiwemo BBC na CNN alisema Mamlaka nchini Tanzania zimezima Mtandao ili kudhibiti maandamano ya Gen Z.
Screenshot 2025-12-19 005728.jpg
Kuzimwa kwa mtandao huku hakujakwamisha maandamano pekee yake, Vyombo vya Habari vilishindwa kufanya kazi kwa siku tano, magazeti hayakuchapichwa kwa muda wote huo.

Runinga na radio nyingi za nchini kasoro zile zilizo chini ya TBC hazikuwa na taarifa ya habari au ripoti yoyote mpya kutokana na kukosekana kwa Internet.

Televisheni kama vile ITV, U TV ya Azam TV hazikuonyesha kabisa taarifa ya habari.
Screenshot 2025-12-19 005855.jpg
Hata TBC hakukuwa na taarifa kutoka kwenye vyanzo vya taarifa kwa kucheza sauti za moja kwa moja (insert) badala yake walikuwa wanapiga simu kutoka kwenye kwa ripota aliyekuwa kwenye tukio hali hiyo iliwagusa pia Shirika la Utangazaji la Zanzibar.

Hata hivyo, taarifa ilikuwa ni matokeo ya uchaguzi ikiwa kulikuwa na matukio ya maandamano siku nzima na siku zilizofuata.

Tarehe 4 Novemba 2025, Gazeti la Mwananchi liliuleza umma kuwa kuzimwa kwa Internet kumesababisha shughuli za chombo hicho za kuhabarisha umma kutofanyika.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo imesema kuwa Oktoba 29, 2025 na siku chache zilizofuata Taifa lilikabiliwa na uzimwaji wa Mtandao wa Internet hatua iliyofanya vyombo vya habari vya ndani kutoweka kwenye mtandao wa kidigitali.

"Mfumo muhimu wa mawasiliano ulidorora upatikanaji wa taarifa ukavurugika na kama ilivyokuwa kwa mamilioni ya Watanzania na taasisi mbalimbali nchini, nasi tulijikuta tukiwa tumeondolewa kutoka kwenye zana muhimu za utendaji wetu wa kila siku.

"Hatukugeuka nyuma. Hatukuiacha nchi yetu. Tulikosa tu njia ya kuwafikia kama ilivyo kwa Watanzania wengine. Hali waliyopitia Wananchi nasi na Waandishi wetu tumeipitia vivyohivyo," ilisema taarifa ya Mwananchi.

Taarifa hiyo ya Mwananchi ilisema kuwa dhamira ya chombo hicho ya kuhudumia umma haijayumba "Tutaendelea kushikilia misingi ya juu ya uandishi wa habari, tukiwatumikia Watanzania kwa uadilifu, ujasiri na kwa heshima kubwa kwa misingi ya kisheria inayotuongoza."

Waandishi wa habari wazungumza
Fedrick Gama amesema kuwa yeye ameshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuuhabarisha umma kwa kuwa alishindwa kupata Internet.

"Kusema kweli kuzimwa kwa mtandao kumenifanya nishindwe kufanya kazi ya habari umma ulituhitaji kuliko wakati wowote lakini unaweza kusema kuwa tumeshindwa kazi yetu," alisema Gama.

Mmoja wa Waandishi wakongwe nchini aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotajwa jina amesema kuwa Serikali ya Tanzania imefika kilele cha ukandamazaji wa uhuru wa habari.

"Afrika inaaminika kuwa ina viongozi wasiopendezwa na ukosoaji na sisi Tanzania ni miongoni mwao lakini kitendo cha kuzima mtandao ni kuhitimisha ukandamizaji wa uhuru wa Habari.

Wakosoaji wanasema serikali imefanya hivyo ili kuficha kinachoendelea nchini Tanzania.

Pamoja na mtandao kuzimwa wananchi wanajihamasisha wenyewe wakidai haki zao na mifumo huru ya uchaguzi - Tito Magoti Mwanasheria wa LHRC.

Shughuli za bandarini zimesimama mipakani shughuli kuendelea.

Matukio yaliyoshindwa kuripotiwa na mitandao mbalimbali, ni pamoja na vituo vya mafuta, polisi na ofisi za serikali kuchomwa moto.

Wakili Jebra Kambole anasema kuwa kuzimwa kwa mtandao ni dhuruma kwa Wananchi na kwamba kitendo hicho hakitakawi kuwa kimya, watakichukulia hatua.

"Uzimwaji wa mtandao, Ukamataji na aina yoyote ya dhuruma dhidi ya Watanzania, amri batili za IGP na ujinga mwingine hatutaukalia kimya tutachukua hatua za Kisheria ndani na nje ya nchi."

Kada maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Martin Masese amesema kuwa kitendo cha kuzimwa kwa mtandao kichukuliwe kuwa ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwengine.

"Kitendo cha kuzima mtandao kinapaswa kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu. Huduma ya intaneti ni hitaji muhimu la kibinadamu ambalo halipaswi kuchezewa kamwe. Kuzima mtandao siyo njia ya kuwanyamazisha watu, bali ni kuwazidishia hasira zaidi. Ni enzi ya giza kwa uhuru wa kujieleza.

Wafanyabiashara wakwama
Wafanyabiashara wanaotumia mitandao kunadi shughuli zao asilimia kubwa zilikwama.

- John Pasia, Dereva wa Taksi Mtandao anasema kuwa siku tano ameshindwa kufanyabiashara zake kutokana na kukosekana kwa mtandao.

"Mimi ili nifanye biashara watu wanatakiwa wawe na mtandao na mimi mwenyewe niwe na mtandao lakini kwa siku tano tangu kumalizika kwa uchaguzi hakuna mtandao," alisema Pasia.

- Sultan Kashona ni Mfanyabiashara katika Soko la Kariakoo amesema kuwa kuzimwa kwa Mtandao kumekwamisha biashara zake.
 
Kuzimwa kwa internet hakujapoka haki za Wananchi pekee yake bali ilikwamisha mambo mengi katika maisha hapa nchini
 
Back
Top Bottom