Kuzaa baada ya 40's!! Inakuwaje?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
........Hivi mtu unapozaa after 40, tena mtoto wa kwanza unapata kwenye umri huo unafikiri nini?

Siku hizi baadhi ya wanawake kwa wanaume wanapata mtoto kwenye 40 au zaidi ya hapo.......je hawa watu hawafikiri baada ya miaka 15-20 si watakuwa wameezeka? Huyo mtoto si atakuwa kama mjukuu!! Vile vile kwenye umri huo utakuwa umestaafu.......utaleaje huyo mtoto, kama huna hata saving utasomeshaje huyo mtoto ili aje kuwa maisha bora?

Najiuliza tu!!
 
Kila mtoto anakuja na riziki yake dada, wala usiumize kichwa.

Mipango ya Mungu hiyo, umesahau jinsi Yohana Mbatizaji alivyozaliwa ilhali wazazi wake waliishajizeekea na kukata tamaa....Pitia pitia bible dia!
 
Mipango tu na uamuzi wa mtu kuzaa akiwa na miaka hiyo.
 
Hapo umesema kweli kuna haja ya kuangalia,umri ni kitu muhimu na kuangalia maisha ya baadae ya mtoto.
 
Kuwa mzazi haijalishi una umri gani...ni uwezo wako wa kumudu majukumu...suala la wataonekanaje siju kama mjukuu its of less important....uzuri umudu kumtunza mtoto na umlee katika misingi sahihi.
 
Si kwa kipindi hichi,siku hizi watoto nao wana watoto,imagine 25 ana kids watano na ashafunga kizazi,mtoto wake wa kwanza alimpata at the age of 14 njoo kwetu uswazi uone
 
Pretty/Lizzy...kuna ukweli kwenye msemalo..lakini dunia ya sasa si kama ya miaka 20 iliyopita! Zamani wazazi wetu serikalini ilikuwa ni lazima wastaafu wakifika umri flani. Sasa hivi wazazi wengi ni either wafanyabiashara au wafanyakazi wa sekta binafsi. Na ukiwa na proffesion yako ya maana basi unaweza ukawa unafanya kazi on a contract basis mpaka hapoooo...Muhimu ni kumuandalia huyo mtoto maisha bora. Fikiria mtoto anayezaliwa na baba wa miaka 30 na huyo baba kufariki baada ya miaka 2 ili hali alikuwa hajamtayarishia mtoto kitu chochote!! Ni balaa kubwa zaidi ya yule mwenye baba wa miaka 50 lakini kamuandalia maisha bora
 
Kulea/kuza mtoto ni zaidi ya pesa Merciful. .. na akili yote ukiweka kwenye pesa ndio matokeo yake mtoto anakua bila kujifunza chochote kutoka kwa mzazi wake, bila kuwa na kumbukumbu nzuri zaidi ya tulikua tunakula wali nyama daily (kitu ambacho hata akikua atapata) na mengine ya aina hiyo. Age different kati ya mzazi na mtoto nayo inamatter sana. . . inadetermine mahusiano kati yao yatakuwaje.
 
Kuzaa watoto wakati umri umeenda sana c vizuri hata kidogo,watu wengine wanasema hadi mambo yawe fresh ndo wazae wansahau kwamba wanazeeka wanaacha watoto.Mi nadhani kuzaa mtoto wa mwisho ni miaka 40,ina maana akifikisha 20 mzazi wake anafikisha 60.
 
Na ukizaa mapema ukaishia kumgawa mtoto kwa majirani na ndugu jinsi mume anavyotumika nje ipi bora mleu??
 
Kuwa na baba ambae hata hawezi cheza mpira na mtoto wake is soooooo not fun. Binafsi nadhani ni vizuri watu wakajitahidi kupata watoto wakati bado wana nguvu za kutosha, uzee ukija wanapumzika.

........Hichi haswa ndicho ninachokizungumzia mimi, ikiwezekana zaa mapema ili uzee upumzike.......sio kuanza kukimbizana na mtoto umri umeshaenda. Hata kama kuzaa ni kupanga, ni vema kuzaa mapema.
 
Kila mtoto anakuja na riziki yake dada, wala usiumize kichwa.

Mipango ya Mungu hiyo, umesahau jinsi Yohana Mbatizaji alivyozaliwa ilhali wazazi wake waliishajizeekea na kukata tamaa....Pitia pitia bible dia!
Nyie ndo munaharibu future za watoto wenu. Wewe kama Baba au Mama unatakiwa kumtunza mwanao kwa kumpatia uwezo wa kuishi pekee yake bila shida.
 
Na inakuwaje unapopanga kupata mtoto mapema lakini kutokana na mipango ya Mungu/matatizo ya kiafya ukapata mtoto/watoto katika umri huo wa kuanzia 40's?
 
Kila mtoto anakuja na riziki yake dada, wala usiumize kichwa.

Mipango ya Mungu hiyo, umesahau jinsi Yohana Mbatizaji alivyozaliwa ilhali wazazi wake waliishajizeekea na kukata tamaa....Pitia pitia bible dia!
Umri siyo hoja sana, swala kubwa hapa ni future ya mtoto. Unaweza ukamzaa katika umri mkubwa ila ukawa umemwandalia mazigira mazuri ya maisha yake ya baadaye.
Na mwengine anaweza akamzaa ujanani na asimjali kabisa mtoto wake.
Nafikir kabla ya kuzaa mtoto, tuangalie na future zao ili waje wawe wanatuombea kwenye makaburi yetu na wala siyo kuyapiga viboko makaburi yetu
 
Pretty, kuzaa mtoto katika umri huo ni sawa tu kama ulivyosema mtoto wa kwanza.....kuna mengi katika hili. Pengine ilikuwa vigumu kupata mtoto wakati wa usichana wake, hakuweza kubahatika kupata mwenza mapema etc.
 
......Kama una matatizo ya uzazi hiyo inaeleweka, ila kuna wengine wanaamua tu kuchelewa kuzaa, wanasema wanaponda kwanza maisha hii kwa wanawake/wanaume.

ukija upande wa kike hawa ndio wale kutwaaaa kutumia madawa ya kuzuia mimba, au kutoa kabisa hizo mimba. Wanaona kuzaa mapema kama kujizeesha.
Ndio hapo, wanapokuja kukumbuka shuka kumbe kumekucha.
 
Back
Top Bottom