Kuzaa baada ya 40's!! Inakuwaje?

........Hivi mtu unapozaa after 40, tena mtoto wa kwanza unapata kwenye umri huo unafikiri nini?

Siku hizi baadhi ya wanawake kwa wanaume wanapata mtoto kwenye 40 au zaidi ya hapo.......je hawa watu hawafikiri baada ya miaka 15-20 si watakuwa wameezeka? Huyo mtoto si atakuwa kama mjukuu!! Vile vile kwenye umri huo utakuwa umestaafu.......utaleaje huyo mtoto, kama huna hata saving utasomeshaje huyo mtoto ili aje kuwa maisha bora?

Najiuliza tu!!

Jiulize pia wanaozaa wakiwa na miaka 15 ama chini ya hapo wanaleaje hao watoto wenzao!!!!!
 
Kusema kweli Pretty wengi ambao nimebahatika kuwaona wakizaa kwenye 40's huwa wanasema imetokea bahati mbaya na mmoja wapo akiwa wifi yangu ambae alishajiandaa kwenda menopouse lakini akajikuta ana mimba tulishangaa sana. Pia kingine wamama/wadada ambao hawajafunga kizazi lakini wanatumia njia za uzazi wa mpango nao wanapojisahau mambo huwa hivo.
 
mamangu alinizaa akiwa over 45...sasa sijui tatizo lake ni nini sasaivi....na bado anafurahia wajukuuu toka kwangu...kitu kingine..labda kama hajawahi kuzaa kabisandio nafikiri ni tatizo..kwasababu mara nyingi unaweza kufanyiwa operation/c-section kama unazaa kuanzia miaka 35....pamoja na kwamba si always....however, ushauri ni kwamba, ni bora mwanamke kuanza kuzaa akiwa chini ya 30...over 30 anakuja kuendeleza tu....ukizidi 35 ni tatizo....pili...wakati mwingine, wanawake wengine wanakosa mabwana..hivyo anajikuta hapati mchumba weee hadi inazidi 35 anaanza kukunjamana bado haolewi tu....katika hali kama hiyo unatakiwa kukubaliana nalolote utakalokutana nalo wakati wa kuzaa...na inatakiwa uzae (kama huna tatizo) au uolewe (kama huna tatizo) ili ujulikane wewe ni mwanaume...wakati mwingine ukiwa huolewi...wenzio wanaweza kukufikiria labda wewe ni bwabwa wa kike...au hata wanaume kama haoi wakati mwingine wengine wanaweza kukufikiria ni punga...hahaha....kuchagua chagua ndiko kunakowafanya wanawake wasiolewe mapema...ukishafika umri kama 35 we hata house boy olewa naye tu alimradi anajiweza kitandani.....kuzunguka wee kama wale wenzangu wa kabila langu kule kilimanjaro wakimendea aje mwanamme wenye mipesa mingi...utajikuta unafika 40 wadogo zako wana watoto wanasoma shule ya msingi...
 
........Hivi mtu unapozaa after 40, tena mtoto wa kwanza unapata kwenye umri huo unafikiri nini?

Siku hizi baadhi ya wanawake kwa wanaume wanapata mtoto kwenye 40 au zaidi ya hapo.......je hawa watu hawafikiri baada ya miaka 15-20 si watakuwa wameezeka? Huyo mtoto si atakuwa kama mjukuu!! Vile vile kwenye umri huo utakuwa umestaafu.......utaleaje huyo mtoto, kama huna hata saving utasomeshaje huyo mtoto ili aje kuwa maisha bora?

Najiuliza tu!!

Ibrahim alimpata Isaac akiwa mzee
 
Mada nzuri hii, tuliochelewa kupata watoto kweli ni mtihani. Japo at 40 pia sitaki kabisa kufikiria uzazi. Kwa mwanaume ukianza kuwatafuta at 25 hadi 39 ni safi kabisa, kwa mwanamke asizidi 35.
 
Mada nzuri hii, tuliochelewa kupata watoto kweli ni mtihani. Japo at 40 pia sitaki kabisa kufikiria uzazi. Kwa mwanaume ukianza kuwatafuta at 25 hadi 39 ni safi kabisa, kwa mwanamke asizidi 35.

Hongera sana
 
Wengine uzazi mgumu unakuta mpk miaka 40 hajashika ujauzito! Kwahyo anaposhika mimba inabidi azae tu hakuna namna
 
“Kila mtoto anakuja na riziki yake”
Siipendi hii kauli kwa nini huku Africa tu ndo tuna mambo na vikauli vya kufuga ujinga mbona wenzetu wana mipango mizuri before hawajapanga kuzaa.(out of thread)
Me binafsi sioni sababu ya kuwai kuzaa kama huwezi kuweka mipango madhubuti ya maisha ya kiumbe unayetarajia kumleta ni bora ukachelewa au usizae kabisa kuliko kuleta mtoto akaja kupata tabu duniani,weka mipango mizuri kwa mtoto ili ata kama utafariki aweze kuish vizur na kupata basic needs.
 
Back
Top Bottom