Kuweni makini na facebook

wakuu kuna kisa cha ukweli mke wa rafiki yangu kalala na mwanaume amekutana nae facebook tena kwa aibu kubwa mana wameanza kuchat ndani ya mwezi mmoja tayari wakasex na kibaya zaidi huyu demu mke wa rafiki yangu alikua na mimba ya miezi 5!!!...kiukweli huyu dada kafanya tukio la aibu sana mana hata mume wake anashindwa kumwelewa mtu mzima kuwa na tabia chafu kiasi hiki...

Ukiangalia watu walioko facebook hakuna kitu cha maana wanachoweza kujadili kwa maana ya issues!!! Pale watu wanaandika pumba tu mara nimechoka,naumwa,nina hasira na mambo mengine meengi ya kienyeji..

Kama mkeo ama mumeo yuko facebook kuwa makini sana...

mkuu kwanza nawapa pole sijui hongera kwa yaliaomkuta maana jamaa ameamua kuongezea mashikio na pua unajua mwezi wa tano ndio muda wake huo.....sasa labda akaona pua ya jamaa iko kama ya babu yake wacha asitoe kituko cha mwaka ajazie wka mshikaji

pili
nafikiria huyo jamaa yako kaoa mlupo tena wa nguvu na tatizo kubwa vijana wetu wa kileeo mnakimbilia wanawake bomba amjui ametokea wapi ana maisha gani..hayo ndio mapito lakini ukija kuangalia vizuri rusimlalamikie tu huyo dad mwambie afanye marping ya wakwe zake lazima kuna kufumaniana sasa hii ni fundisho kwa mnaoingia kanisan jumamosi na jumapili na wenzangu wa ijumaa ..swala sio tu demu anarembea mnakimbizana nae...mpe pole sana

tatu
facebook aina matatizo mkuu kabisa kabisa kabisa ..yaani hiyo mutu yako iko na problema kuba tuu haata angekuja jf wangemfukunyua tu kwa style yake uliosema la maana baba
chukua chako mapema mwambie aanze amefuga pepo tena makata
 
:nimekataaJamani acheni kuwahusisha watu wote na tukio la mtu mmoja...........huwezi sema kwakuwa fulani yuko hivi kwenye fb, basi kila aliyeko fb yuko vile. Kila mtu ana tabia yake na anatumia kulingana na mahala alipoona ni sahihi kutumia hiyo tabia.
Ila kusema kweli huwezi kulinganisha fb na JF. JF ipo juu. JF wanadiscuss issues za maana sana zinazojenga jamii. lakini fb, mhhhhhhhhhhhhhhhh. Acha tu. Yaani hata ukipost kitu cha maana wengi watakuona mjinga tu na hawatachangia chochote. Kwa hilo nakuunga mkono ila usifikiri ni kila mtu yuko kama mwana dada huyo.
 
Wakuu kuna kisa cha ukweli mke wa rafiki yangu kalala na mwanaume amekutana nae facebook tena kwa aibu kubwa mana wameanza kuchat ndani ya mwezi mmoja tayari wakasex na kibaya zaidi huyu demu mke wa rafiki yangu alikua na mimba ya miezi 5!!!...kiukweli huyu dada kafanya tukio la aibu sana mana hata mume wake anashindwa kumwelewa mtu mzima kuwa na tabia chafu kiasi hiki...

Ukiangalia watu walioko Facebook hakuna kitu cha maana wanachoweza kujadili kwa maana ya Issues!!! pale watu wanaandika pumba tu mara nimechoka,naumwa,nina hasira na mambo mengine meengi ya kienyeji..

kama mkeo ama mumeo yuko facebook kuwa makini sana...
Huyo mwanamke kicheche kwenye mtandao kagawa uroda je kama unakutana naye kwenye safari simnaenda kupanga hotel moja bila hatakutongozana??sema huyo mshikaji wako hakumstukia demu kama Cheche languvu!!
 
Jaribu kufanya hesabu rahisi ili kupata faida na hasara za fb. Kama wewe in mathematician mzuri utabaini kuwa kuna faida nyingi za kijamii zitokanazo na mitandao kama fb kuliko vinginevyo. Mbona mleta thread hajasema kuweni makini na simu nk?
 
Tatizo sio fb, tatizo ni huyo mwanamke na mwanaume aliyemmega na wengine wenye tabia kama zao waliopo kwenye hiyo mitandao
 
Duh!!muoneeni huruma kidogo mwenzenu.....ila naye alitakiwa awe anafikiri zaidi ya anavyofikiri sasa, kwaiyo watu wakikutana makanisani/misikitini na kuamua kufanya uzinzi wao na sisi tuache kwenda kanisani/msikitini?????Huyo mwanamke mzinzi tu!!!!
 
Kwa ujumla mambo ya mahusiano, uzinzi, na uzinifu hayajasalimika na mapinduzi yaliyoletwa na maendeleo ya dotcom. Siku hizi ni rahisi sana kuchiti na unaweza kuchiti bila mwenzio kujua au kuhisi kuwa unachiti.

Unaweza uka hook up na mtu aliye mbali na wewe. Mkapanga mambo mengi sana. Mkapanga mkutane wapi na lini. Mnaweza mkanunua tiketi zenu za ndege kupitia mtandaoni. Mkabook na hata chumba cha hoteli kupitia mtandao. Mtu unaweza ukawa na email accounts kibao kila moja ikiwa na dhumuni lake. Na hata kama umeoa au kuolewa bado unaweza kufanya haya yote bila mwenzio kujua na huyo mwenzio akabaki kujua wewe u mwaminifu kwake kumbe wapi.

Siku hizi kuna hadi tovuti za kutafutia infidelity. Yaani wote mnaokuwa wanachama wa hiyo tovuti na kwa ujumla hali zenu na malengo yenu yanakuwa yamefanana. Wote mnakuwa mko kwenye ndoa na wote mnakuwa mnatafuta infidelity kwa siri. Mkikutana huko na kuongea na kukubaliana yanayofuata ni kitu na boksi.

Kwa hiyo kwa ujumla mtandao (iwe facebook, twitter, gmail, yahoo, JF, n.k.) umekuwa kiungo muhimu sana katika kurahisisha uzinzi wa watu. Inasikitisha lakini ndo ukweli wenyewe huo.

Nimejaribu kuangalia wanaounga mkono hoja na wale ambao wanakuwa wakali kwa watu wanaoisema vibaya fb nikagundua ke wanaipenda zaidi.
 
Huku ni wana JF ss FB inatafuta nn katupe au post huko kwenye FB yenu huku tunajadili mambo ya maana jamani hebu Model tafadhali ondoa hii tuna mambo mengi ya kujadili huku plzzzzzzz!

unaweza ukasema Moderator au Mod kwa kifupi.
 
ana pepo huyo!!!

wala si maswala ya facebook naomba Mungu asiifahamu JF.
 
Hatuwezi kuilaumu facebook na kusema kuwa eti facebook hakuna la maana wanalojadili nadhani hii ni subjective zaidi ya mtandao wenyewe. Nadhani tuwalaumu hao jamaa wazinzi kwa kushindwa kuitunza miili yao na kuitumia kihisia zaidi ya kiakili na busara! Hasa huyo mke wa mtu kwani alijua tayari amekwishafungamana na mwenzie wa ndoa lakini akautoa mwili wake utawaliwe na tamaa zake za mwili!
 
Suala hapa sio huyu shemeji yangu kumegwa...amemegwa akiwa na mimba ya miezi 5!!! na kwa jinsi alivomuambia mume wake alikutana na huyu jamaa FB na akalala nae the whole nite akiwa ameaga anaenda kwao Tanga!!! jamaa yuko njiapanda amuache ama avumilie huu ufuska?!!

Hivi ingekuwa huyo jamaa yako ndo kato€¥£
nje ungeongea maneno haya. Ungeanzisha Uzi huu?
 
mkuu unacholalamikia kamegwa akiwa na mimba ama amemhujumu mumewe@@@@
 
huyo rafiki yako mwambie amtimizie mahitaji yote mkewe inavyoonekana huyo mke wa rafiki yako ana matatizo katika ndoa thats y kafanya anafanya mambo ya ajabu
 
Duuu hiyo ni hatar sasa jamani,sa' best 'ako amelichukuliaje hili?mpe pole na amkabidhi Muumba!!!kweli ni lazima tuwe makini na utandawazi
 
Sure haijalishi, ni wapi watu wanakutana, ukiwa na tabia ya inzi utatua popote penye uvundo, huenda huyo mwanamke alifanya kukomoa. Sio hivi hivi.
 
Back
Top Bottom