Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

wengine huweka kutangaza kazi zao. Sioni tatizo sana. ila shida ni wale wanajaza status hata mambo yasiyo na msingi.
akienda kunywa chai kaweka, kula kaweka, kunywa kaweka.

ila kuna kauuhusiano ka kuweka weka status na maturity.
kiasilia kuna baadhi ya watu nimeacha tu kuwa naangalia status zao coz najua hakuna la maana.
Pia me huwa mwekaji status kiasi kidogo mara nyingi niwapo free.
 
Mwezi mmoja au miwili iliyopita ndio nimejua status Nini, Nilikua najua ndio profile pic.

Na watsup nimeanza kuitumia tangu enzi hizo za Nokia E72(Symbian).
Mimi hata kuweka hizo status nilikua sijui na mwezi April ndio nilifundishwa kuweka. Hii kitu inataka mazoea nilijitahidi kuweka kwa kipindi kifupi vyenyewe haiko akilini mwangu mbona nlijikuta naacha

Wako watu wanaweka status daily naweza sema hii ni addiction, wengine hadi wakikwaruzana wanaweka status aisee ni hatari
 
mtazamo wangu naona kuna watu wa aina mbili kwenye swala la kuweka na kutoweka status.
kuna wale nadhani wana insecurity issues kwamba hawataki kuonekana kama walivyo na aibu pia.
lakini pia kuna wale pia naona ni watu wa privacy tu hawataki watu wajue wanafanya nini au wapo wapi au wanafikiria nini.
nawasilisha
 
Kuna mtu humu nina namba zake huu mwaka unaenda wa pili, ila hata siku moja sijawahi muona akiweka status ama akiview zangu.

Siku nyingine naweka naset aone yeye mwenyewe lakini zitamaliza masaa 24 sioni akiview

Watu wa hivyo wana shida gani? Ni utu uzima au ndio wako busy hawana muda na status??

Bado nawashangaaa aisee
Usishangae ni mambo ya preference tu! Mama yeyoo wangu ni mtu wa kuangalia status kila muda kuna muda namwambia Oya hivi huchoki? Anasema anataka kusoma mood za watu kupitia status
 
Back
Top Bottom