Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, May 21, 2018.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
  [​IMG]
  LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

  Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
  Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

  Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

  Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
  Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

  Mchanganuo Wa 69500 ni:-
  Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

  Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
  Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
  layer's consetraite

  Kilo 25 kifuko. = 21500.

  Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

  Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

  Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
  Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
  Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

  TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
  Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

  Jogoo 1 = 20000
  Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
  Itakuwa imebaki shs. 60500

  -Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

  Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
  Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

  Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

  Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

  Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
   
 2. mahondaw

  mahondaw JF-Expert Member

  #81
  May 31, 2018
  Joined: Apr 9, 2013
  Messages: 16,258
  Likes Received: 24,519
  Trophy Points: 280
  Sina hamu na magonjwa ya kuku yakianza ni balaa..


  Cc Smart911
   
 3. soine

  soine JF-Expert Member

  #82
  Jun 1, 2018
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 881
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Haya ndio mawazo mema
   
 4. Nas Jr

  Nas Jr JF-Expert Member

  #83
  Jun 1, 2018
  Joined: May 15, 2018
  Messages: 370
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 60
  Utekelezaji sasa ndio mtihani kwa wengi, tunapenda stori tu na kuishia kutamani.
   
 5. bachelor sugu

  bachelor sugu JF-Expert Member

  #84
  Jun 1, 2018
  Joined: Jan 30, 2018
  Messages: 926
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 180
  Yaani huu mchanganuo nauona hapa ni kama mara ya 88 toka nimeanza kuuona sehemu mbalimbali miaka kibao iliyopita but ukweli ni kuwa theoretical expectations km hizi kamwe hazitatuacha salama,just simple like that mtu awe milionea pasipo kwanza kuwafundisha watu changamoto kuu zinazoukabili mfugo huo.Issue sio kwamba watu hawana huo mtaji but changamoto kuu inayokwambisha watu ni hayo magonjwa yasiyoelezeka na bahati mbaya wataalamu wengi hawana uwezo wa kukabiliana nayo na mwishowe wafugaji wengi kuishia kuangukia pua.Leteni kwanza elimu ya kutokomeza magonjwa ya kuku ndio mtuletee mchanganuo wa faida ama sivyo tutakuwa tunapiga story tu za KIBANGA AMPIGA MKOLONI.
   
 6. devor

  devor Senior Member

  #85
  Jun 2, 2018
  Joined: Oct 15, 2017
  Messages: 158
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Majani sio shida kwenye wadudu nikiwapa dagaa"
   
 7. PatriceLumumba

  PatriceLumumba JF-Expert Member

  #86
  Jun 2, 2018
  Joined: Mar 9, 2016
  Messages: 399
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 80
  HABARI,
  "Kibanga Ampiga Mkoloni,
  Hongera kwa habari nzuri ila pale mwanzo uliposema kuku 11 baada ya miezi mitatu utakuwa na kuku 300 au zaidi hiyo inawezekanaje kibanga?

  LUMUMBA
   
 8. Rais Wa Malofa

  Rais Wa Malofa JF-Expert Member

  #87
  Jun 2, 2018
  Joined: Aug 27, 2015
  Messages: 234
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Nimejitahidi saana kufuga lakini nikifanikiwa kupiga hatua kidogo unakuja ugonjwa unaondoka na kuku woote. Na hii ndio changamoto kubwa kwenye huu mradi.
   
 9. Chiwaso

  Chiwaso JF-Expert Member

  #88
  Jun 2, 2018
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 4,738
  Likes Received: 2,555
  Trophy Points: 280
  Ukizingatia chanjo pamoja na kufugia kwenye eneo ambalo liko controlled hiyo ndio itakuwa salama yako.
   
 10. lukesam

  lukesam JF-Expert Member

  #89
  Jun 2, 2018
  Joined: Feb 23, 2015
  Messages: 7,934
  Likes Received: 11,547
  Trophy Points: 280
  Biashara ya ufugaji sio rahisi kama una moyo mdogo wa kukata tamaa.

  Kuku anaweza kutotoa vifaranga woote wakafa
   
 11. l

  lordchimkwese Senior Member

  #90
  Jun 5, 2018
  Joined: Nov 16, 2015
  Messages: 157
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 60
  Acheni kudanganyana wazee
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #91
  Jun 8, 2018
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 9,321
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Kwanza ngoja nihangaike kujenga banda
  Nalog off
   
 13. P

  Peter Agostino Member

  #92
  Jun 8, 2018
  Joined: Sep 23, 2016
  Messages: 51
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 25
  Ufugaji wa namna hii unawezekana kabisa lakini itategemea upo eneo gani, mjini au kijijini na kama ni mjini basi iwe angalao ni maeneo ya nje ya mji kidogo ambapo kuna nafasi ya kutosha kwani kuku zaidi ya 300 kuwafungulia eneo dogo utagombana na majirani kila upande. Kwa kijijini inawezekana na hii ndiyo husaidia ufugaji wa kuku wa kienyeji kuwa na faida huko ijapokuwa kinachowaangusha watu sana ni magonjwa. Ikiwa utafanya hivyo na kuongeza mbinu nyingine mbalimbali unaweza ukafikia lengo hilo japo uchambuzi wa gharama mleta uzi hajafafanua kwa kina sana. Kuku wa kienyeji wana faida kubwa sana ukiweza kuthibiti suala la magojwa na kutumia vyema sayansi ya kutengenez vyakula kwa gharama ya chini.
   
 14. soine

  soine JF-Expert Member

  #93
  Jun 8, 2018
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 881
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Wazo zuri na mada kama ni muhimu kwa afya ya wanajukwaa na taifa kwa ujumla wake.

  ANGALIZO: Tufanye tathimini kwa kungalia soko kwanza isije tukazalisha kwa wingi "kama nyanya" kipindi kile. chunguza ktk eneo lako ka kuna wafugaji wengi na soko pia
   
 15. msafwa93

  msafwa93 JF-Expert Member

  #94
  Jun 8, 2018
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,763
  Likes Received: 2,566
  Trophy Points: 280
  Nzuri sana
   
 16. tpaul

  tpaul JF-Expert Member

  #95
  Jun 9, 2018
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 14,020
  Likes Received: 4,352
  Trophy Points: 280
  ni wazo zuri la kibiashara ila tatizo letu tulio wengi ni ule uthubutu wa kuanzisha huo mradi kwa kuwa watu ni waoga wa ku-take risk.
   
 17. F

  Free Thinker JF-Expert Member

  #96
  Jun 9, 2018
  Joined: Feb 15, 2013
  Messages: 568
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Ha ha ha...
  Hivi nani alitunga hii hadithi aiseeh?
  Kwanza, Kuku wa kienyeji huwa hawatagi kwa pamoja, na hawatagi mfululizo... Ukianza na Kuku 11 na ukienda vizuri inaweza fikisha Kuku 100 ndani ya mwaka mmoja ukijitahidi na uwe na Bahati kweli kweli...
  Utajiri sio kama kucheza draft kwamba unaweka hapa na kupata pale...
  Naongea kama mfugaji mzoefu na mbobevu, hii hesabu ya mada hii field HAIWEZEKANI
   
 18. IROKOS

  IROKOS JF-Expert Member

  #97
  Jun 9, 2018
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,992
  Likes Received: 3,159
  Trophy Points: 280
  Mimi nafuga kuku wa kienyeji kwa matumizi yangu na familia (nyama na Mayai) na kuuza pale wanapokuwa wengi na pia kununulia chakula na dawa. Anachosema mleta mada si sahihi kwa kipindi kifupi hivyo.
   
 19. Tiger SR

  Tiger SR New Member

  #98
  Jun 10, 2018
  Joined: Mar 23, 2018
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Idea nzuri mfano dar es salaam hapa ukiwaacha waende nje c utakua ushawapa waungwana vitoweo
   
 20. rubaman

  rubaman JF-Expert Member

  #99
  Jun 10, 2018
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 4,657
  Likes Received: 949
  Trophy Points: 280
  Kuku 11 (wa kienyeji)wazalishe kuku 300 in 3 months ni impossible labda uwe unafuga panya. Kifaranga kinachukuwa miezi 3 hadi miezi 6 kukuwa na kuanza kutaga mayai. Tuwe tunaandika vitu vya ukweli sio kudanganyana kama wanasiasa wa hiki chama wanavyofanya
   
 21. evocom

  evocom Senior Member

  #100
  Jun 10, 2018
  Joined: Jan 14, 2017
  Messages: 182
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  Good idea, ni kuifanyia kazi tu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...