Ukizomea utashughulikiwa kama mhaini mkubwa nchiniWanabodi,
Saa hizi natafuta usingizi unagoma, hivyo nimeshuka jf, tutafakari pamoja kuhusu huu utafiti uliowahi kufanywa na kubaini kuwa kwenye kila Watanzania 4, mmoja ni kichaa!. Jee katika hizo sampling, inawezekana pia kukawa na baadhi ya viongozi wetu wa vyama, taasisi, mashirika, na serikali na taasisi zake?. Huu utafiti ulipotoka sikuuamini niliuona kama umekuwa exaggerated, lakini kadri siku zinavyokwenda na mambo yanavyokuwa, mwenzenu nimeanza kuuamini kwa kujifanyia self diognosis na kukuta ni kweli!. Wewe jiulize jee wewe ni mzima?, na kisha jiulize hivi sisi Watanzania tuu wazima kweli? !. Tufanyeje kuondokana na hali hii?.
Huu ni uzi wa swali, kuwa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Mtu Aokote Makopo!. Jee Kuna Uwezekano Tanzania Tunao Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
Kuna msemo usemao kuwa kichaa sio lazima mtu mpaka aokote makopo, ila kwa maneno na matendo ya baadhi ya sisi Watanzania wakiwemo baadhi ya viongozi wetu, nashawishika kabisa kuamini, kuna uwezekano wengine sio wazima kabisa kichwani ila pia sio vichaa kwa sababu hawaokoti makopo! .
Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu accross the section, na baadhi ya matendo yao yakiwemo maamuzi yao ,amri zao na hatua ambazo wanachukua kudeal na situations mbali mbali zinanithibitishia kuwa badhi ya wenzetu sio wazima kabisa kichwani na na mimi nikiwemo, hivyo wanahitaji kusaidiwa kujitafakari badala ya kushangiliwa tuu kwa kila wanachokifanya, hata wakifanya ndivyo sivyo, watashangiliwa tuu na kupongezwa! .
Vichaa Viongozi.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko ya baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, na ukafuatilia matendo yao,amri zao na maamuzi yao, utakubaliana na mimi sisi Watanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyo jidhania.
What to do to help out.
Mtu kichaa hajijui kama kichaa mpaka atakapojulishwa ukichaa wake, na kujitafakari, ndipo atajigundua na kubadilika. Namna ya kuwasaidia viongozi wetu kujitambua, ni pale wanapotamka matamshi ya kiendawazimu, au kutoa maamuzi ya kiendawazimu, badala ya kuwashangilia wazomeeni ili wajitambue.
Kitendo cha viongozi hawa kutoa matamshi ya kiendawazimu na maamuzi ya kiajabu ajabu na sisi tukiwashangilia badala ya kuwakemea au kuwazomea, kunapelekea wote kuonekana ni vichaa!.
Hivi kweli Tanzania tumefika hapa kuwaacha vichaa hawa kufanya ukichaa wao huku sote tukishangilia tuu bila kukemea, jee sote ni vichaa au kuna wenzetu wanaona tofauti na wanaweza kusaidia tubadilike?.
Paskali
jingalao YEHODAYAHapana, ukichaa huongezeka pale unapopewa rutuba na vimelea vifuatavyo; Wakudadavuwa, Lizaboni, Ruttashobolwa, stroke, Adharusi, Amrish Puri, Ng'wanapagi, Pamputi, kampelewele, foxplato, mwengeso na gunia zima kutoka Lumumba.
......You are absolutely right! Mark Twain anakuambia kuwa "We are all stupid,Just on different subject".
Umeandika kama Pascal Mayalla na siyo kama Pasco.Hivi ni kwanini ulibadilishaga jina Mkuu?.
......Huu uzi mgumu sana kuchangia; maana ukichangia hovyo tu na wewe automatically unajumuishwa kwenye kundi la vichaa, khaa!
Paschal kwanini umewaza hivyo?
Sawa kabisa ila jina lako linakutambulisha,Bahati nzuri mimi si kichaa...wala sipo kwenye kundi la viongozi.