Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Saa hizi natafuta usingizi unagoma, hivyo nimeshuka jf, tutafakari pamoja kuhusu huu utafiti uliowahi kufanywa na kubaini kuwa kwenye kila Watanzania 4, mmoja ni kichaa!.

Jee katika hizo sampling, inawezekana pia kukawa na baadhi ya viongozi wetu wa vyama, taasisi, mashirika, na serikali na taasisi zake?. Huu utafiti ulipotoka sikuuamini niliuona kama umekuwa too exaggerated, lakini kadri siku zinavyokwenda na mambo yanavyokuwa, mwenzenu nimeanza kuuamini utafiti huu kwa kujifanyia self diognosis na kukuta ni kweli, maana hata mimi mwenyewe kumbe sio mzima sana kivile!

Kumbe hata kukosa tuu usingizi (insomnia) kwa mawazo ni tatizo la akili!. Hata msongo wa mawazo, (depression) ni tatizo la akili!. Naomba na wewe hebu jifanyike a self diagnosis wewe mwenyewe kwa jiulize jee wewe ni mzima?, na kisha jiulize hivi sisi Watanzania tuu wazima kweli?

Tufanyeje kuondokana na hali hii?

93dabf10a9a1ea1c5395c14deb0a409c.jpg


Huu ni uzi wa swali..
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Mtu Aokote Makopo!. Jee Kuna Uwezekano Tanzania Tunao Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.

Kuna msemo usemao kuwa kichaa sio lazima mtu mpaka aokote makopo, ila kwa maneno na matendo ya baadhi ya sisi Watanzania wakiwemo baadhi ya viongozi wetu, wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa vyama vya kijamii, viongozi wa Bunge letu Tukufu, badhi ya waheshimiwa Wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa, nashawishika kabisa kuamini, kuna uwezekano mkubwa, baadhi yao au wengine wetu sio wazima sana kivile!, na wengine sio wazima hata kidogo!, kichwani hawana kitu kabisa bali ni kama vichaa kabisa, ila kwa vile hawaokoti makopo, then watu hatuwezi kuwajua kuwa ni vichaa!. Kuwa kichaa jameni sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.

Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu across the section, na baadhi kauli na matendo yao yakiwemo maamuzi yao ,amri zao na hatua ambazo wanachukua kudeal na situations mbali mbali zinanithibitishia kuwa badhi ya viongozi wetu sio wazima kabisa upstairs, (kichwani) na mimi mwenyewe mwandishi wa bandiko hili nikiwa not exceptional!, hivyo wanahitaji kusaidiwa kujitafakari badala ya kushangiliwa tuu kwa kila wanachosema na wanachokifanya, hata wakifanya ndivyo sivyo, watashangiliwa tu na kupongezwa! .

Najitolea Mfano Mimi Mwenyewe.
Mimi mwenzenu ni mwandishi wa habari wa kujitegemea. Nimebahatika kuishi na kufanya kazi ya uandishi nchini Uingereza, Marekani, Italia, Sweden, Uswisi, India na Afrika ya Kusini.

Kote huko waandishi wapiga picha hutumia pikipiki ili kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Nikiwa nchini Uingereza nilikuwepo wakati wa kipindi cha kifo cha Lady Diana Princes of Wales na kuona jinsi Paparatsi (Mapaparazi) wanavyotumia pikipiki kupata picha vizuri na kwa haraka.

Nikiwa Italy na baadaye nchini Marekani kote ni hivyo hivyo hata matangazo ya live TV ya mashindano ya riadha, mashindano ya magari na baiskeli, watangazaji wake wanatumia pikipiki.

Hivyo nikiwa nchini Marekani nikashuhudia pikipiki kubwa zenye uwezo kama gari kukatisha jimbo moja hadi jingine na nchi moja hadi nyingine "cross country".

Hivyo nikiwa nchini Marekani, nikakata shauri kuwa na mimi nitatumia pikipiki, hivyo nikanunua Pikipiki kubwa ya familia ya Harley Davidson "Buell" yenye 1,200 cc na speed ya 240 kph, (gari zote za Japan mwisho ni 180 kph), ambayo haitumii mnyororo wala haitumii shafti bali inatatumia belti na kuteremka nayo Bongo. Na mpaka hivi ninavyoandika bado sijafanikiwa kuona Buell nyingine yoyote ndani ya Bongo!.

Mimi ndio nilikuwa Mtangazaji wa kwanza wa TV Tanzania kufanya kazi kwa kutumia Big Bike na kwa foleni za Dar, kiukweli I was the fastest journalist kufika kwenye tukio. Dar-Chalinze 45 min. Dar Moro 90 min. Dar-Dodoma 4hrs. Dar-Moshi 4 Hrs.

Wakati nikitumia bike, wife alikuwa ni muoga sana wa kupanda pikipiki na kutokana na ukubwa wa pikipiki yangu na mwendo ninaokwenda nao, nikaamua sipakizi mtu kabisa na sehemu ya kiti cha abiria nikafunga sanduku la Kamera. Wife anatumia gari.

Kuna wakati nilikuwa nafanya Maonyesho ya 88 Morogoro huko nikilala Dar, asubuhi ni moto na moto wake kuelekea Moro, na jioni narudi kulala Dar. Kuna siku tuliondoka at the same time na wife mimi nikienda Moro yeye akienda town, huwezi amini, mimi nilitangulia kufika Moro kabla yeye hajaingia town.

Mimi bila kujua kadri unavyokwenda mbio ndivyo akili zinavyozidi kukuruka na kuzidi kuongeza mwendo kwa kupandwa na ukichaa wa mwendo kasi kutaka kupaa!.

Siku ya siku ikafika nawahi Dodoma, nimezilalia hivyo nikachelewa kuamka. Kushtuka ni saa 2:00 asubuhi na nina kipindi saa 6:00 mchana Dodoma, Dar-Dodoma kwa mnyama wangu ni masaa 4 tuu!. Nikawasha moto na moto wake, mimi huyo Dodoma!.

Kumbe siku hiyo ndio ilikuwa siku yangu, naomba nisihadithie kilichotokea, ila mwisho wa siku nilipiga chini mzinga wa haja at 160 kph!. Wala huo mwendo sikuujua, bali kuna gari ya mheshimiwa mmoja ilikuwa at 140, niliipita kama imesimama!, nilipokula mzinga, derava huyo ndio alikuwa wa kwanza kufika, sio kuniokoa, bali kushangalia speed ya bike, baada ya kuelezwa, the man is dead!.

Justification.
Kuhalalisha matumizi ya pikipiki kwa mwendo kasi ni kama ulaya na Amerika wanatumia, why not Tanzania? . Hivyo mimi nimeona wazungu wanazunguka dunia na pikipiki itakuwa kuzunguka Tanzania?. Hivyo kila mahali nilikwenda na bike ila familia gari. Na kwenye events za kuulambia suti na kwenda na wife nilitumia gari, hivyo kule kusimama tuu kwenye foleni kwangu ilikuwa ni kero ya ajabu!.

Kosa.
Kosa kubwa ni kuona Ulaya watu waride big bikes cross country na kuiga kuja kuendesha big bike Bongo. Madereva wa wenzetu wana discipline ya hali ya juu kuheshimu sheria za barabarani, huku kwetu ni Mungu anajua. Wenzetu wana mabarabara mazuri na mengine yana bike lanes kuruhusu high speed bikes, huku kwetu barabara ndio hizo hizo gari, pikipiki, baiskeli na waenda kwa miguu, huku zimepinda pinda mashimo kila mahali, wapi pa kutumia 240 kph? .

Self Realization.
Baada ya kunikuta ya kunikuta na kupata ya kunipata ndipo unapokuja kuzinduka kwenye self realization na kujiuliza, hivi "was I thinking right?!", kutumia usafiri wa pikipiki kwa long safari barabara zetu ndio hizi na madereva wetu ndio hawa! . Unagundua it was a mistake, ni kosa kubwa kuifananisha Bongo na mamtoni!, kumbe huu ulikuwa ni ukichaa!.

Sio Mzima, Sio Kichaa.
Baada ya kuumia huwezi tena kuendesha pikipiki, sasa unatumia gari, japo unakereka na foleni na kuimisi sana bike jinsi ulivyokuwa unapaa, lakini unapopishana na madereva wa boda boda kila uchao, unaangalia mwendo wao, anaangalia fujo zao barabarani, jinsi walivyo rough riders, unajilinganisha na enzi zako ulipokuwa rider ulikuwa very rough kuliko hawa!, then unajiridhisha kuwa kiukweli japo huokoti makopo lakini alikuwa kichaa!.

Wengi ni Vichaa na Kufanya Ukichaa, Japo Hawaokoti Makopo!.
Kiukweli wengi wa madereva wa boda boda ni vichaa, madereva wa dala dala ni vichaa, wadada na wamama wanavaa nguo za ajabu ajabu ni vichaa, wadada wenye rangi zao za asili za kupendeza lakini wanajichubua kuwa kama wazungu ni vichaa! . Madada na wamama wenye nguvu zao lakini wanafanya ile biashara kichaa ya kuuza miili yao, ili kuendesha maisha yao, (kudanga) ni vichaa, kinababa wanashinda baa kula bia, kuku, bata, nyama choma na kumalizia na ma barmaids huku nyumbani ni ugali maharage, familia zinateseka ni vichaa.

Vichaa Viongozi.
Kwa muktadha huo wa ukichaa, ukiwasikiliza matamko wanayotoa baadhi ya wanasiasa wetu, viongozi wetu wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa taasisi mbalimbali wakiwemo baadhi ya wakuu wa mihimili, na hadi baadhi ya viongozi wetu wa dini, ukifuatilia kauli zao, amri zao, matendo yao na baadhi ya maamuzi yao, utakubaliana na mimi kuwa, japo ukiwaangalia kwa juu juu utawaona ni wazima kabisa, lakini uki wa scrutinize closely, utakubaliana na mimi kiukweli kabisa, wengine sii wazima sana upstairs, na hili litatathibitishwa na muda, hivyo kunauwezekano sisi Watanzania tuna vichaa wengi zaidi kuliko tunavyo jidhania!.

Jee Vichaa Hawa, Wako Katika Makundi Mangapi?.
Vichaa hawa wako katika makundi 5.
Kundi la Kwanza- Hawa ni vichaa wenye temporary insanity, au pseudo insanity, ambacho ni kile kichaa watu wengi wanacho hii huletwa na stress na hasira, au kuchanganyikiwa tuu kwa muda mfupi, ukitulia kinakwisha.

Kundi la Pili- ni la lunatics ambao hawa wanaenda na mwezi, au unaitwa wazimu, mwezi ukiwa mchanga, kinapanda, mwezi mpevu kinatulia, kama maji kujaa na kupwaa, au good moods na bad mood, akiwa kwenye bad mood ni kichaa ni kama kichaa lakini kikawaida yuko completely sane.

Kundi la Tatu -ni la wale wanaojitoa ufahamu, hili lina wanaume wachache sana, majority ni wanawake waliokwisha pita menopause. Hawa huwa wanajisemea chochote kile bila aibu. Kundi hili pia linawahusisha watu wote wenye msongo wa mawazo, depression, na wote wanaoamua kujiua.

Kundi la Nne -ni la wasema hovyo, wapayukaji, watenda vitendo vya kiajabu ajabu na wale wasiofunzwa na wazazi wao, hili ndilo kundi kubwa kabisa, hadi humu jukwaa, wako wengi kibao, wao ni matusi tu, hata ukiuliza kitu simple kwa nidhamu ya hali ya juu, subiria matusi yatakayoporomoshwa, walio bungeni wanaropoka, walio serikalini wanafanya maamuzi ya ajabu ajabu, etc.

Kundi la Tano- ni la wale ambao ni certified mental case, hawa ni wagonjwa kabisa na ukichaa wao ni ugonjwa kabisa, hawa sio kosa lao, ugonjwa wa kichaa ni kama ugonjwa mwingine wowote, tusicheke ugonjwa.

What to do to help out.
Mtu kichaa kwa kawaida huwa hajitambui, wala hajijui kuwa yeye ni kichaa mpaka atakapojulishwa ukichaa wake, na kujitafakari, ndipo atajigundua na kubadilika. Namna ya kuwasaidia viongozi wetu hawa vichaa kujitambua, ni pale wanapotamka matamshi ya kiendawazimu, au kutoa maamuzi ya kiendawazimu, badala ya kuwashangilia wazomeeni ili wazinduke na wajitambue.

Kitendo cha viongozi hawa kutoa matamshi ya kiendawazimu na maamuzi ya kiajabu ajabu na sisi tukiwashangilia badala ya kuwakemea au kuwazomea, hakuwasaidii, na hakutusaidii, na badala yake, kunapelekea wote kuonekana ni vichaa!.

Hivi kweli Tanzania tumefika hapa kuwaacha vichaa hawa kufanya ukichaa wao huku sote tukishangilia tuu bila kukemea, jee sote ni vichaa au kuna wenzetu wameisha jitambua, na wanaona tofauti na wanaweza kusaidia ili tubadilike?. Kama moja ya sifa za kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, ni pamoja na kuwa na akili timamu, hivi huu utimamu unapimwajwe wakati tukiwashuhudia na maneno na matendo ya kiendawazimu, au ili kuwapima, au iwekwe kabisa kwenye sheria, taratibu na kanuni, moja ya vigezo wa kuwa kiongozi wa ofisi za umma ni pamoja na kupimwa afya ya akili, ili kuepuka kuwa na viongozi vichaa?.

Paskali
Rejea
Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu?

Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timamu, Anaweza Kuichagua Tena CCM?!. Kwa Lipi?!.

Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.Tuache Cherry Picking Kutafuta Mbuzi Wa Kafara!.

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?
 
Hata mimi naona nishaambukizwa hiki kichaa..
Afya ya akili inazidi kuporomoka sijui 2020 ntakua na hali ganii..!!
 
NIMEKUELEWA PASKALI nami nitoe oni langu.... kichaa anapochekewa bila kukemewa ukichaa hukua na hiongezeka maradufu.. hivyo shime uonapo/usikiapo tendo lolote la ukichaa tulilaani na kulikemea papo kwa hapo ; kwa njia hiyo tunaweza kumpunguzia hali yake ya ukichaa au matendo ya ukichaa ya muhusika.
 
Viongozi wetu wengi ninahisi niwanafiki na waoga. Wanafikiria nikiachishwa kazi nitaenda wapi. Wanapenda kupamba ili kuridhisha tu mradi wapate mkate wao wa siku. Na ndio maana wakitoka,kwenye uongozi wanakuwa km wameondolewa pazia au wameosha macho na hivyo kutambua kuwa walifanya makosa. Dhamira inawasuta.
 
You are absolutely right! Mark Twain anakuambia kuwa "We are all stupid,Just on different subject".

Umeandika kama Pascal Mayalla na siyo kama Pasco.Hivi ni kwanini ulibadilishaga jina Mkuu?.
 
Hapa wakusudiwa viongozi wawili tu, lakini hawajatajwa majina yao. Magufuli na Makonda
tozi25, acha uchokozi...alichosema mtoa mada ni hii, nanukuu;

"Hoja hii imetokana na kutafakari kwa makini baadhi ya kauli, maagizo, na maamuzi yetu sisi kama Watanzania na viongozi wetu across the section..."

Sasa hebu elezea kwa nini unadhani hao wawili ndio waliokusudiwa, je kwako hawa ndio unawaona ni vichaa?
 
Kujulikana mpaka uwe na National Platform hapo ndio Watu watajua kuwa wewe ni Kichaa au, ni Fit! Kwa wenye Outlook ya Kitaifa Mimi Nadhani Kichaa Kuliko wote ni Mmoja, Kule kwa Wazee wangu Wanasema na nitafasiri Punde! " Mmeku so le, Neeteta sha mndu alesora mmanga we ringa umbe" Huyo Mzee Anaropoka mithili ya mtu aliyemeza Kengele ya Kuchunga ng,ombe! Ukimjua huyo ni nani basi Utajua Mkichaa ni nani.
 
Hata kichaa hudhani watu wenye akili timamu ni vichaa huku yeye akidhani ana akili timamu.

Mtu unatafuta usingizi unagoma halafu unaanza kuwaza matamko ya wanasiasa badala ya kuwaza afya yako. Mbaya zaidi hao unaowaza matamko yao wamelala na wake/waume zao wakifurahia maisha.

First priority ni afya yako.
Second priority ni familia yako.
Third priority ni ndugu zako.
Fourth Priority ni taifa lako.
Fifth priority ni dunia yako.
 
Back
Top Bottom