Huu uzi umenikumbusha mbali sana,that time niko na miaka 19 tu ndo kwanza naanza chuo
Nilikuwa nshajua kuwa nategemewa, so bum likitoka tu kama kuna ada nalipa pango nalipa nabakiwa na kihela cha kula na stationery tu,kilichobaki natuma home dogo asome,sikuwahi pendeza wala kula bata na ile hela,nguo zenyewe nkua najiendea karume na nunua matishet ya bukubuku.
lakini ikafika kipindi akawa hataki shule,mara achague shule hiii ile siitaki,sijawahi kata tamaa,siku moja nilituma hela ya ada,maza aliongea kauli ambayo hadi leo haijawahi nitoka
Alisema "pole mwanangu umekua baba katika umri mdogo" i felt that to my bones
Mshua alifariki nikiwa na 5 years,so all our life na mdogoangu maza amepambana sana,so nlijiwekea ahadi kua,nitapambana mpaka tone la mwisho,ili maza na dogo waishi vizuri,thank God amekua akinifungulia milango, hawawezi kosa mkate wala mahitaji muhimu.