Kuwa first born sometimes ni shida

Kuwa first born sometimes ni shida

Kumbuka pia kuna baraka na neema kuwa mtoto wa kwanza kwenye familia

Nje ya mamlaka ya kiroho, kuwa firstborn sometimes unajitambua mapema kutokana na macho ya wazazi wako wote kukuelekea muda wote
 
Tatizo lenu nyie akina dada, hata ukiwa first-born unajifanya kuwa siyo first-born. Unapitisha majukumu kwa wadogo zako wa kiume.
Mimi ni last born..
1st born wetu alifanya kazi kubwa sana kwa sisi wadogo zake.. kwa kiasi kikubwa amenilea.

Watoto wa kiume labda wanaojitambua,wengine hawajitambui mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Last born kama nakuona!!
Kabisa mkuu.

Mimi nimesoma na mafirst born..yaani akikohoa tu kidogo hela zinatumwa yaani macho yote yapo pale,,sometimes wanawapiga wazazi vizinga vya uongo.

Sisi malast born tunawahurumia wazazi kwa sababu wana watoto wengi wanawahudumia.
Sasa wao wamesoma wamemaliza,
Umefika muda wa malast born kutanua..1st born watuvumilie tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa takwimu zinavyoonesha familia nyingi Watoto wa kike ndo wanasaidia familia. Wakiume Wengi hawanaga habari
Hiyo n kweli, lkn kumbuka mwanaume ni tegemeo kwa familia yake na majukumu yote yanamwangalia.
Lakin mtoto wa kike hata kama anapata meshahara hiyo n hela yake mwenyewe coz matumizi mume atatoa.
 
Familia zijisaidie zenyewe. Familia za watoto wa kiume (mke na watoto wao) zinajisaidia zenyewe. Kwa nini familia zisaidiwe na watu wengine?
Kwa takwimu zinavyoonesha familia nyingi Watoto wa kike ndo wanasaidia familia. Wakiume Wengi hawanaga habari
 
Habari zenu wakuu,

Jamani maFirst born hasa tuliozaliwa kwenye hizi familia zetu za kipato Cha kawaida nadhani msoto wa kukabiziwa majukumu kabla ya wakati mnaujua.

Yani umepata kibarua Chako hata we mwenyewe hujimudu vizuri, unakabidhiwa mdogo wako umsomeshe na majukumu mengine ya nyumbani usaidie. Yani wadogo zako wao slope tu, kitu kidogo mtafuteni kaka/dada Yani ushatwikwa majukumu Kama yote.

maFirst born mliobeba majukumu ya mzazi popote mlipo hongera zenu.
Zamani first born inherit everything wengine mnakaa kimya
 
Kuwa mzaliwa wa kwanza ni changamoto kiroho na kimwili
Ukiwa mzaliwa wa kwanza kwenye familia zetu hizi za kimaskini unabidi uwajibike kama mtoto wa kwanza na wakati mwingine unabeba majukumu ya mzazi ili mambo ya kifamilia yaende sawa
Kwa walio wengi japo siyo wote mzaliwa wa kwanza akifel kwenye maisha na mambo mengine kama elimu hadi wanaomfuata huwa hawafanyi vema
Mzaliwa wa kwanza anapo wajibika kwenye familia wakati mwingine anachelewa kuoa au kuolewa kwa sababu huwa ana majuku ya kwake na ndugu , jamaa na marafiki
MZALIWA WA KWANZA NI LANGO INABIDI KUWAOMBEA SANA HAWA WATU MUNGU AWE PAMOJA NAO.
 
Mi first born ila kuna huyu dogo ni mtukutu nimempa kipondo mpaka hataki kuniona madogo wakizingua lawama zinakuja kwetu zote sasa ilo sipo tayari nitamyoosha sawia tens barabara, niligoroga sabuni ya unga nikatia pilipil kwa mbaalii nikamloesha nikamlamba waya mpaka nikamuonea huruma
 
Huu uzi umenikumbusha mbali sana,that time niko na miaka 19 tu ndo kwanza naanza chuo

Nilikuwa nshajua kuwa nategemewa, so bum likitoka tu kama kuna ada nalipa pango nalipa nabakiwa na kihela cha kula na stationery tu,kilichobaki natuma home dogo asome,sikuwahi pendeza wala kula bata na ile hela,nguo zenyewe nkua najiendea karume na nunua matishet ya bukubuku.

lakini ikafika kipindi akawa hataki shule,mara achague shule hiii ile siitaki,sijawahi kata tamaa,siku moja nilituma hela ya ada,maza aliongea kauli ambayo hadi leo haijawahi nitoka

Alisema "pole mwanangu umekua baba katika umri mdogo" i felt that to my bones

Mshua alifariki nikiwa na 5 years,so all our life na mdogoangu maza amepambana sana,so nlijiwekea ahadi kua,nitapambana mpaka tone la mwisho,ili maza na dogo waishi vizuri,thank God amekua akinifungulia milango, hawawezi kosa mkate wala mahitaji muhimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom