kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,310
- 12,607
Binadamu wote wake kwa waume wanazaliwa wakiwa uchi kabisa, kuvaa nguo ipi na ivaliwe wapi na nani kwa sababu gani ni utashi tu wa wanajamii wenyewe. Bahati mbaya au nzuri Mwenyezi kuna maeneo na viungo vya mwili ambavyo alishavifunika yeye mwenyewe kwa sababu zake kwa kutumia nywele ndefu na nywele fupi kutokana na umuhimu wake na sababu zake. Mfano, Mungu amekifunika kichwa cha kila mtu kwa nywele ndefu bila kujali jinsia yake, kabila wala dini yake, Mungu akakifunika kinena cha kila mtu aliyebalehe kwa nywele ndefu tunazoziita mav*zi. Hakuishia hapo akakifunika kidevu na kifua cha mwanaume kwa nywele ndefu pia kwa sababu zake mungu mwenyewe. Hakuishia hapo akaifunika ngozi ya mwili ya watu wote kwa nywele fupi tunazoziita malaika kwa sababu zake pia, akatupa pia nyusi, kope na nyweli puani bila ya kumuomba. Hivyo kila nywele ilikuwa na sababu yake na ilitosha kabisa kuifanya kazi iliyokusudiwa kufunikwa na kukingwa. Hii ni kuonyesha kuwa Mungu anayajuwa mahitaji yetu yooote.
Ni nani ambae hataki kumuona mwanamke ambae asiyefunika nywele zake? Je, ni mwanamke mwenyewe kwa sababu zipi? Je, ni mwanaume kwa sababu zipi na je, ni Mungu aliyetufanya tuzaliwa uchi lakini akatufunika kwa nywele kwa sababu zipi?
Utafiti wangu kwenye hili ni kwamba, sio Mungu anaetaka wanawake wavae Hijab bali ni wanaume tu kwa sababu ya wivu na kujifanya kuwa wao ni dhaifu kwa kutazama tu nywele, matiti, mapaja na vitovu vya wanawake wakasahau kuwa Mungu angetaka asingeshindwa kuwafanya wanawake wazaliwe wakiwa na hijab tayari. Tuache ujinga wa kuwadhulumu wanawake kwa kujificha kwenye kichaka cha dini. Nini sio Hijab wala nywele za mtu.
Ona haya mauaji na maandamano ya kijinga kabisa, eti msichana hakuvaa hijab.