Kuumwa tumbo mtoto mchanga

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
1,044
1,996
Habari wana JF ,Mwanangu ana umri wa mwezi mmoja na siku tatu.Anasumbuliwa sana na tumbo ,huwa anajisokota na kulia muda mwingi na anataka muda wote apakatwe au bebwe.

Lkani pia leo ni kama siku ya 8 au 9 hapati choo kikubwa.Ananyonya vzri,anacheua vzri lakini shida ndoo hilo tumbo kuuuma na kuttopata choo.

Naomba anaejua dawa ya kutumia au ushauri wa kitabibu.Nitashukuru ndugu zangu.
 
Mara nyingi huwa inategema na utamaduni wa sehemu yenu ungewauliza kwanza wazazi wako au wa mkeo kama wapo au mkubwa yeyote,wa kwangu pindi alipokutana na changamoto hiyo bibi alisema kikatwe kipande kidogo cha sabuni kiloweshwe kisha anawekwa kwa kupakaa kidogo sehemu ya ndani ya haja na hakutumia muda alipata choo
 
Hujasema ana umri gani ila tatizo la kutopata choo niliuliza humu mzizimkavu akasema ni kawaida sana kwa watoto hiyo ishu kwakuwa mifumo yake ya mwili haijakaa kiutu uzima bado (namaanisha kwamba hakuna chakula cha maana anachokula cha kumfanya akate gogo za maana)
 
Kuhusu tumbo hiyo mimi nilipewa cotrimoxazole ya maji zahanati, nikaja kupewa dawa fulani ya kulamba (ipo kama mkaa uliosagwa)

Sasahivi yuko fresh sana
 
Kutopata choo kwa umri huo ni kawaida ila awe anajamba,hakikisha anapomaliza kunyonya mama anamlaza kwenye bega huku akimsugua mgongoni au amlaze kwa tumbo kama ameshakatika kitovu,pia paka mafuta ya nazi mikono yako ipashe kwa kuisogeza karibu na jiko kisha mkande tumbo lake baada ya kuoga kuanzia juu kushuka chini baada ya hapo mfanyie mazoezi ya kibaiskeli itamsaidia kurelax na kutoa gas inayomnyima raha.....hongereni kwa kuwa wazazi
 
Habari wana JF ,Mwanangu ana umri wa mwezi mmoja na siku tatu.Anasumbuliwa sana na tumbo ,huwa anajisokota na kulia muda mwingi na anataka muda wote apakatwe au bebwe.Lkani pia leo ni kama siku ya 8 au 9 hapati choo kikubwa.Ananyonya vzri,anacheua vzri lakini shida ndoo hilo tumbo kuuuma na kuttopata choo.Naomba anaejua dawa ya kutumia au ushauri wa kitabibu.Nitashukuru ndugu zangu.
Mkuu nenda pharmacy nunua Gripe Water. Ukimpa hiyo sekunde sio nyingi anaachia gesi na kucheua, anatulia. Kuna brand nyingi, nimesahau ipi ni Bora.
 
Pole sana mkuu
SGN_11_26_2021_1637934876563.jpg

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Digestive system ndiyo inajiimarisha. Akishanyonya akae begani mpaka acheuwe kupunguza gas. Mfanyie massage wakati akiwa begani.
 
Kutopata choo kwa umri huo ni kawaida ila awe anajamba,hakikisha anapomaliza kunyonya mama anamlaza kwenye bega huku akimsugua mgongoni au amlaze kwa tumbo kama ameshakatika kitovu,pia paka mafuta ya nazi mikono yako ipashe kwa kuisogeza karibu na jiko kisha mkande tumbo lake baada ya kuoga kuanzia juu kushuka chini baada ya hapo mfanyie mazoezi ya kibaiskeli itamsaidia kurelax na kutoa gas inayomnyima raha.....hongereni kwa kuwa wazazi
Upo sahihi kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom