Kuuliza si ujinga: Waliotajwa kwenye Ripoti za profesa Osoro na Mruma (kuhusu madini) wamechukuliwa hatua gani kulingana na mapendekezo ya Kamati?

Ndio uje hata kesi waliotufungulia Acacia hatuwezi kushinda na huu ndio ushahidi kuwa tunaibiwa kupitia mikataba tuliosaini wenyewe tukiwa na akili zetu timamu.

Sisiem ni matapeli.
 
Kina nani walitajwa?

Ni hatua gani za kuwachukulia zilipendekezwa na kamati/repoti?

Tuelimishe pia wengine ambao hatuwajui hao waliotajwa!
Aidha, Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji wa muda wa leseni (renewal) wa maeneo ya uchimbaji madini kinyume cha sheria na bila kuzingatia maslahi ya taifa.Kwa mfano, kuongeza muda wa leseni na maeneo ya uchimbaji uliofanywa na Mheshimiwa William M. Ngeleja na Mheshimiwa Sospeter M. Muhongo, kwa kampuni za North Mara Gold Mines limited na Pangea Minerals Limited.Pia
38

leseni mbali mbali zilizotolewa na; Kamishna Paulo M. Masanja, Kamishna Dalaly P. Kafumu na Kaimu Kamishna Ally B. Samaje. Katika kipindi hicho washauri wakuu wa Serkali kwa masuala ya kisheria ni pamoja na Mheshimiwa Andrew Chenge, Johnson Mwanyika na Manaibu Wanasheria Wakuu ambao ni Felix Mrema na Sazi Salula na Wakuu wa Idara ya Mikaba Maria Ndossi Kejo na Julius Malaba.
 
Makinikia yashaondoka, na wanaume bado wanajichotea dhahabu.
USD Billioni 190 sawa na TZS 425 Trilioni malimbikizo ya kodi na adhabu hawajalipa.
USD Milioni 300 sawa TZS 678 Bilioni "kishika uchumba" hawajalipa
Makinia yameondoka huku wao acacia wakiendelea kuchimba na kufunga baadhi ya migodi.

The report was truly a professorial rubbish!
 
Kwani ile ripoti ilikuwa na dhumuni la kuyafanya yale waliyoyaorodhesha?
Wao walitaka tu kuwakomoa wapinzani waliowapa ushauri mzuri tu jinsi ya kulinda utajiri wetu.
Kwa taarifa yako wote waliotajwa hawataguswa na kiumbe yoyote chini ya utawala huu na siku wakijaribu wajiandae baada ya wao kuondoka kuna kupokea ripoti ya uuzaji wa nyumba za serikali, ununuzi wa vivuko vibovu, ndege kuukuu bila kufata taratibu za manunuzi, uvunjaji wa haki za msingi za binadamu, ukwepaji kodi kwa viongozi wa umma, yaani huyo Prof atakaye soma ripoti atatuambia tumeuziwa mitumba kwa bei ya juu sana, kwenye SGR tumepigwa sana kwa hiyo atashauri adhabu kali sana zichukulie kukomesha hayo na hapo ndio utwaona wale wote waliokuwa wanaimba na Bashite wakimsindikiza kwenda Kisutu na kurudi Segerea.
Sasa yote hayo wakiyawazia wanaona bora kuzima fegi tu.
 
Aidha, Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji wa muda wa leseni (renewal) wa maeneo ya uchimbaji madini kinyume cha sheria na bila kuzingatia maslahi ya taifa.Kwa mfano, kuongeza muda wa leseni na maeneo ya uchimbaji uliofanywa na Mheshimiwa William M. Ngeleja na Mheshimiwa Sospeter M. Muhongo, kwa kampuni za North Mara Gold Mines limited na Pangea Minerals Limited.Pia
38

leseni mbali mbali zilizotolewa na; Kamishna Paulo M. Masanja, Kamishna Dalaly P. Kafumu na Kaimu Kamishna Ally B. Samaje. Katika kipindi hicho washauri wakuu wa Serkali kwa masuala ya kisheria ni pamoja na Mheshimiwa Andrew Chenge, Johnson Mwanyika na Manaibu Wanasheria Wakuu ambao ni Felix Mrema na Sazi Salula na Wakuu wa Idara ya Mikaba Maria Ndossi Kejo na Julius Malaba.
Ngoja nisubiri kuona Goli likihamishwa MTU kama huamini ndio utaona ni kwa namna gani kuna maMTU yanamiliki Vichwa kufugia Nywele tu
 
Hivi ripoti si zina muda wa ku-expire? nadhani zitakua zime expire, subiri nyingine zitatoka soon
 
Back
Top Bottom