Kuuliza si ujinga: Waliotajwa kwenye Ripoti za profesa Osoro na Mruma (kuhusu madini) wamechukuliwa hatua gani kulingana na mapendekezo ya Kamati?

Wakuu waungwana wa JF,

Kama kuna yeyote anayejua anisaidie na wengine wanaotaka kujua kama mimi.

Karibuni wajuzi wa mambo

Muktasari wa Ripoti ya Kamati ya Prof. Osoro unapatikana hapa:

https://www.ikulu.go.tz/files/publications/attachments/2_sw.pdf

Waione: JokaKuu, Mag3 Pascal Mayalla na wengineo

Hawajachukuliwa hatua yoyote na hawatokaa wachukuliwe hatua yoyote maana awamu hii hawapambani na ufisadi, bali wanakomesha matumizi ya neni fisadi. Hujawahi kusikia wanaccm kila wakichangia majukwaani na huku social media wakisema wapinzani wanaendesha siasa za kutukana. Kutukana wanayoiongelea ni hiyo watu kuwaita mafisadi. Kichekesho nilikiona wiki ile ya rais akiwa huko Mara eti alituhumiwa mtendaji wa kata kwamba katumia pesa za kijiji, basi rais na waziri Kange wakaagiza akamatwe eti ndio hayo mafisadi rais anayatafuta!! Halafu wananchi (wanaccm) waliokuwepo wakashangilia kwa nguvu kwamba mafisadi yanashugulikiwa. Ukiona mtu kakamatwa kwa kisingizo cha ufisadi kama sio mpinzani basi jua huko nyuma alikosana na jiwe hivyo anakomolewa.
 
Kina nani walitajwa?

Ni hatua gani za kuwachukulia zilipendekezwa na kamati/repoti?

Tuelimishe pia wengine ambao hatuwajui hao waliotajwa!

Usitake kujifanya hukufuatilia, Chenge, Yona, Karamagi nk walitajwa kwa majina, rais akaagiza wakamatwe siku ile ile na uchunguzi dhidi yao uanze mara moja. Hilo halijafanyika na halitokaa lifanyike kwani anayeendesha vita hiyo ni kambale aliyetoka kwenye bwawa chafu na bwawa chafu halitoi kambale msafi. Hitimisho letu likawa hakuna kupambana na ufisadi bali kupambana na matumizi ya neno fisadi kwa kile wanaaccm wanachoamini ni kutukanwa kwani hakuna msafi kati yao.
 
report ya mruma ilikuwa ni ya uongo likiwa na data za 'kupika' mahususi kwa ajili ya kufurahisha jiwe na wendawazimu wezake!
 
Kina nani walitajwa?

Ni hatua gani za kuwachukulia zilipendekezwa na kamati/repoti?

Tuelimishe pia wengine ambao hatuwajui hao waliotajwa!
Wewe unajua udaku na kushabikia yale yanayokutekenya na kukufurahisha

Huwezi jua dunia inavyokwenda kama kazi yako ni kufungua thread za uccm au uchadema huwezi kuwa updated hata siku moja na mapinduzi ya Taarifa na Data

Utaendelea kuwa mtazamji wa watu wanavyoendelea wewe ukibaki kushabikia uccm na uchadema

You are a CERTIFIED Zéro Brain in Tanzania
 
..nimesikia Acaccia wametushitaki.

..mimi nashauri na sisi tuwafungulie mashtaka [ counter sue] ktk mahakama ya usuluhishi ya kimataifa, na tuwatume Prof.Mruma na Prof.Osorro, pamoja na timu zao za wataalamu kuwa mashahidi wetu.

Cc Daimler, Pascal Mayalla, Nguruvi3
Kuna vitu watu tukisema humu, tunaonekana kuwa tunamchukia Magufuli kwa sababu ni watu wa EL!.

Baada ya kutoka ripoti ya pili, nilipandisha bandiko hili, Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Hapa nilisema rais amedanganywa, na kwa vile mpaka hapa ninapoandika, sijasikia juhudi zozote za kuutafuta ukweli wa makinikia, kwa maoni yangu, Tanzania hatuna locusts stand to counter their arguments, mkataba upo, sheria imelalia kwao, tutashindwa miserably!, kitakachofuata, ni tutawapa mchanga wao, kama bado hatujawapa, then watafuta kesi, tutamalizana nje ya mahakama!.

P
 
Back
Top Bottom