Mwaka 2018 ni mchungu kwa vigogo 18 waliotajwa kamati za madini

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mwaka 2018 huenda ukawa mchungu kwa viongozi wa umma 18 ambao Rais John Magufuli aliagiza vyombo vya dola kuwachunguza na kuwachukulia hatua baada ya kutajwa katika ripoti nne za uchunguzi wa biashara ya madini nchini.

Wakati baadhi ya vigogo hao wakisimamishwa kazi kupisha uchunguzi, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola amesema kazi ya kuwachunguza inaendelea na kuwataka wananchi kusubiri siku watakayofikishwa mahakamani.

Miongoni mwa vigogo hao ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara kabla ya kujiondoa kupisha uchunguzi, Eliakim Maswi; waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, William Ngejela, Profesa Sospeter Muhongo, Daniel Yona, Nazir Karamagi na George Simbachawene.

Simbachawene pia aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) katika Serikali ya Awamu ya Tano. Pia wamo waliowahi kuwa wanasheria wakuu wa Serikali, Andrew Chenge na Johnson Mwanyika.

Wengine ni waliowahi kuwa makamishna wa madini Paulo Masanja, Dk Dalaly Kafumu ambaye sasa ni mbunge wa Igunga (CCM) na Kaimu Kamishna, Ally Samaje ambao wote Rais Magufuli aliviagiza vyombo vya dola kuwachunguza na wakibainika hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao.

Vigogo hao na wengine walitajwa katika ripoti mbili za kamati zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga wa madini na masuala ya kiuchumi na kisheria kwenye makinikia ambazo ziliibua kasoro lukuki ikiwamo ya sheria zinazosimamia rasilimali hiyo.

Nyingine ni ripoti mbili za kamati za Bunge zilizoundwa na Spika Job Ndugai kuangalia uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi ambazo nazo zilibaini ukiukwaji wa taratibu zinazolisababishia Taifa hasara.

Baada ya ripoti mbili zilizoundwa na Rais Magufuli kuwekwa hadharani kuchunguza madai ya wizi na ufisadi unaodaiwa kufanywa na wawekezaji kwa zaidi ya miaka 19 iliyopita tangu walipoanza uzalishaji wa dhahabu, mazungumzo kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Corporation yalianza.

Mazungumzo hayo yanalenga kujadili kasoro zilizobainishwa na ripoti hizo na yamekuwa yakielezwa na kiongozi wa timu ya Tanzania na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuwa yanakwenda vyema na nchi itegemee kunufaika.

Akizungumza na gazeti hili jana Kamishna Mlowola alisema, “Utaratibu wetu ni kwamba nikishachunguza napeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.”

“Wananchi mtapata matokeo yatakayojitokeza mahakamani, mtaona watu wanapelekwa mahakamani, kama watapelekwa sambamba na tathmini inayofanywa na mwanasheria wa Serikali.”

Alisema kulingana na kazi zinazofanywa na taasisi hiyo kwa sasa hawezi kuweka wazi walipofikia katika uchunguzi huo.
“Uchunguzi ni mwendelezo na siwezi kukuambia kwa sasa tumefikia wapi,” alisema.

Ripoti ya kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma iliyowasilishwa kwa Rais Mei 24, ilibaini kasoro za usimamizi na kumng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo katika wadhifa huo huku Rais Magufuli akiivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

Pia, Rais Magufuli alimsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wake, Dominick Rwekaza na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi dhidi yao ikiwamo watumishi wote wa TMAA na wakibainika hatua kali zichukuliwe.

Katika ripoti ya pili ya kamati maalumu chini ya Mwenyekiti Profesa Nehemiah Ossoro iliyowasilishwa Juni 12, ilibaini usafirishaji mchanga uliolipotezea Taifa matrilioni ya fedha tangu mwaka 1998 shughuli hizo zilipoanza.

Upotevu huo ulitokana na sababu kadhaa ikiwamo ukwepaji kodi, utoaji taarifa za uongo za usafirishaji makinikia na uwajibikaji usiozingatia masilahi ya Taifa.

Ripoti hiyo ilibaini ubovu wa sheria ya madini na matumizi mabaya ya madarakani yaliyofanywa na mawaziri, makamishna na wanasheria katika kuingia mikataba na kutoa leseni ambazo Rais Magufuli tayari amekwishatoa zuio la utoaji wa leseni mpya.

Kutokana na matatizo hayo, Serikali ilipeleka bungeni miswada mitatu ya mabadiliko ya sheria zinazohusu sekta ya madini na rasilimali inayotoa fursa mbalimbali za Taifa kunufaika.

Mbali na vigogo hao waliotajwa kuhusika na kuisababisha Serikali hasara, naibu wanasheria wakuu Felix Mrema na Sazi Salula na wakuu wa idara, Mikaba Maria, Ndossi Kejo na Julius Malaba pia walitajwa.

Vigogo wengine wanaochunguzwa ni wale waliobainishwa katika kamati mbili za Bunge ambazo awali Spika Ndugai alizikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 6 mjini Dodoma, ambaye naye alizikabidhi kwa Rais Magufuli Septemba 7, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya vigogo waliotajwa na kamati hizo na tayari wamejiuzulu ni Simbachawene, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani na Maswi.

Wakati kamati ya Profesa Mruma ikibaini makontena 277 yaliyozuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam yana tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya kati ya Sh676 bilioni na Sh1.147 trilioni; ya Profesa Osoro ilianika uozo uliopo kwenye mikataba ya madini.

Ripoti hiyo ilifichua kutosajiliwa kwa kampuni ya Acacia Mining inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, North Mara na Pangea.
 
by 2019 Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa 'corruption free country"
 
Kwa nini usiseme kwamba habari hii nikutoka kwa mwananchi news paper ya leo?? 19.12.2017?? Yaani ume copy naku paste umeshindwa hata kutoa credit kwa mwananchi news paper???
 
Wewe bado unaamini hadithi za makinikia? Mpaka sasa imepatikana hela kiasi gani toka kwa waliotajwa kuwa, 'wanatuibia'. Mtu akikufanya mjinga na wewe ukaamini ujinga unaoambiwa huwi mjinga tu bali utakuwa mp.umbavu.
 
Eti Valentino Mlowola ni Mkurugenzi wa PCCB, rudi tena ukajipange na story yako
 
Zile reports zote zilikuwa ni uongo mtupu kwa ajili ya kumfurahisha bwana mkubwa, hivyo kuwachukulia hatua kwa kutumia reports za uongo uongo ni kutowatendea haki
 
Kwa kweli biashara hii inalipa haswa

Huko Sierra Leone pastor aliyeahidiwa kulipwa pesa za almasi alioichimbua amekataliwa tena na serikali yake na kupewa 40% tu ya $6.5m na nyingine inachukua serikali kwa kuwa alikuwa hajapewa bado licence ya uchimbaji.

Hii Almasi iliuzwa mjini New York wiki iliyopita
Kwa kweli tuna utajiri mkubwa sana Africa kama tungeutumia vizuri
 
Pesa ya makinikia vipi? Imeshawasili nchini au ndio ili bilioni moja dola aliyeikamata mwenyewe kule JNIA.

makinikia jamaaaaaani. Tuonyesheni yale Matrilioni yalikokwenda.
 
Tatizo la TAKUKURU sio kuwa hawana utendaji.. No TAKUKURU ni watendaji wazuri ila shida ni kuwa wanapambana na symptoms of a problem rather than a real problem.. Rushwa sio tatizo.. Ila rushwa ni dalili ya tatizo.
Tatizo linalosababisha watu kutoa/kupokea rushwa ni perceived injustice, kipato kidogo kisichokidhi mahitaji na pia kutoa rushwa as an easy way to get out of a bad situation or problem.
 
Back
Top Bottom