Kuuliza Bei Kabla ya Kula uwapo Outing ni Akili na kujiamini lakini Malofa huona aibu

Nikiwa form 3 nimetoka mchikichini tuition kwenye pindi huyoo mpaka pande za posta naenda kula upepo wa bahari si nikakutana na kimgahawa mshenzi nikaagiza wali nyama mixer njegele nikijua ni bei zetu za buku jero. Kupiga bill imekuja 4000, balance inasoma 2000 ambayo ni pamoja na nauli, ashukuriwe bro wangu alienifanyia muamala chap ila yasikukute

Wabongo wanatabia ya kukariri na kukadiria Huduma za Watu. Sasa Dawa Yao ni hiyo
 
KUULIZA BEI KABLA YA KULA UWAPO OUTING NI AKILI NA KUJIAMINI LAKINI MALOFA HUONA AIBU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mmetoka out, mmefika kwenye mgahawa, mnaagiza chakula. Huoni aibu kuagiza chakula lakini unaona aibu kuulizia bei
Asee umetema madini kama kawaida yako taikon hii inatukuta sana vijana tukiwa nahivi videmu unaagiza tu naunalipa huku moyon unaumia iliwakunitokea mliman city ice cream moja elf 12 dadek
 
Umeongea point tupu mkuu kwanza mi nimuhanga waiyo kukurupikia sehem za hotel bila kuzijua kwanza.

Kuna siku niko na mama watoto nikasema tupitie sehemu kupata lunch, sehem nzuri, mpya, ila sikuwahi kufika kabla, nilikua naona tu mtandaoni. Tumekaa tumeagiza sina hili wala lile wife akanambia tuhame meza au tuondoke nikamuuliza why!!! Ndo akanambia nyuma yangu kuna mtu ana kumwanglia muda wote af anamuwekea gestures ila hamuelewi nayeye wife anakosa comfort maana angle alipo nilazima amwangalie kos mi nilikua sijamface wife so hapo ndo alarm ikapiga kichwani nikaona kweli mi ni mpuuzi kwanza nimengia sehem bila kujua vzuri kitu ambacho sio utaratibu wangu.

Ipo ivi (TIPS)
Kama unataka kutoka na wife ama familia hakikisha kwanza unafanya visiting kwenye iyo sehem hunapafaham kwa kias, kagua kuanzia bei, mazingira, choo ziko wapi na usalama, wahudumu na huduma zipo kiwango gani, angalia angle zitazokua safe ukuwa na mtu wako

Note. Ukienda sehemu ukakuta watu washakaa af kuna seat ziko wazi mainly izo seat sio nzuri kukaa inabid hue smart kwajicho la haraka chek angle sehem safe mwambie muhudum awawekee seat au kama kuna sehem nyingine mwambie awapeleke.

Binafsi hua nikienda sehemu siulizi bei kwanza naaziga dry drinks then zikifika ndo namwambia alete menu kama hana nilazima niulize bei kwenye kila nachohitaji maana ni uzembe wao kutoandaa menu.
 
Ukiongea mighahawa ya ukweli
Lazima upewe menu..upitie

Ova
20230820_095847.jpg
 
Ukienda Mlimani city una idea ya bei ya soda, at least kadiria 3000, mimi huwa sina haja ya kuuliza maana naenda mahali ninapo class napo. HUWA nimekuwa makini wakati nipo USA na Poland, ila Tanzania? Sina sababu ya kuuliza bei.
Kuna wahudumu wahuni watakuuzia bei tofauti kulingana na ulivyozumbukuku, kutapeliwa ni kubaya hata kama ni hela kidogo tu
 
Niliwahi kwenda Mwanza kwenye shughuli fulani,pembezoni ya hotel tuliyokuwapo palikuwa na mgahawa mzuri tu. Nikaulizia mchemsho samaki unagharimu kiasi gani? Nikaambiwa Tsh.11000.00 nikambiwa hiyo ni samaki kichwa,yaan nusu,nikaona kama ni bei sana. Basi nkamwambia naomba chai ya maziwa na chapati mbili,hapo sikuuliza bei nkijua itakuwa ni kama bei zetu zile😂😂😂,bill imekuja ni Tsh. 8000.00,nilitukana matusi yote kimoyomoyo ila nikalipa. Kama ningeuliza bei ya chai na chapati basi bila shaka ningechagua mchemsho wa samaki.
Kuuliza bei kabla ya kuagiza ni jambo sahihi kabisa.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Siyo malofa mkuu,pesa,pesa.... wenye pesa.ukiwa na pesa huteseki
Hii sawa na mkataba wa bandari, unatia saini tu hujui huko mbele kuna manufaa au hasara. WaTz tubadilike!
Biashara ya mgahawa pia ni mkataba/ makubaliano ya muuzaji na mnunuzi. Unapewa menu, si tu itakuwa na aina ya vyakula, bali na bei yake pia. Mnunuzi unamudu bei ya chakula ukipendacho, unakiagiza na muuzaji atawajibika kukuletea chakula na utawajibika kukilipia, la sivyo unaachana nacho.
 
Popote ninapoingia lazima niwe na ATM card,simbanking na ninajua nikiagiza kitu fulani hakiwezi vuka bei fulani hata waongeze bei vp na experience ya kuingia sehemu zenye class unasaidia(exposure pia)

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Yeah. Ndio maana wameweka bei
Bro Big up sana Mkuu ! Maandiko yako yamekuwa Bible ndogo kwangu kila siku nasoma walau thread moja - nakuchukua madini ya ukweli , ahahaha nakaribia ku - graduate na kuwa Mtibeli kamili - na nitakutafuta unisimike rasmi . Kiukweli Bro unafundisha watu kuwa Solid na kurudisha jamii ile ya zamani yenye watu wa kujielewa ,misimamo na kujuamini - kitu ambacho Dunia ya leo na mambo yake inatoa product ya binadamu soft sana mpaka huruma.Mkuu tupe vitu vigumu tuwe wagumu , nawasilisha !
 
Niliwahi kwenda Mwanza kwenye shughuli fulani,pembezoni ya hotel tuliyokuwapo palikuwa na mgahawa mzuri tu. Nikaulizia mchemsho samaki unagharimu kiasi gani? Nikaambiwa Tsh.11000.00 nikambiwa hiyo ni samaki kichwa,yaan nusu,nikaona kama ni bei sana. Basi nkamwambia naomba chai ya maziwa na chapati mbili,hapo sikuuliza bei nkijua itakuwa ni kama bei zetu zile😂😂😂,bill imekuja ni Tsh. 8000.00,nilitukana matusi yote kimoyomoyo ila nikalipa. Kama ningeuliza bei ya chai na chapati basi bila shaka ningechagua mchemsho wa samaki.
Kuuliza bei kabla ya kuagiza ni jambo sahihi kabisa.
😂😂😂
 
Back
Top Bottom