Kutunza pesa pia ni kipaji

Kutunza pesa pia ni kipaji

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,042
Reaction score
20,045
Wakuu ipo hivi kwa mtazamo wangu nashawishika kusema kwamba utunzaji wa pesa ni kipaji si bure nishawaza kila aina iman juu ya utunzaji pesa hatimaye nimefikia hitimisho hivyo.

Nilishajitahidi sana na kujiapiza sana ila wapi yaani lazima tu itatokea kisanga cha kupelekea kutumia pesa niliyohifadhi au basi tu hizi statements za acha nitoe alafu nitarudishia ndio usiseme zinafilisi balaa.

Hivi wale watu ambao hata wakutwe na balaa gani hawatoi pesa walizohifadhi ni discipline tu au kuna namna wanakuwa hivyo automatic au ni wabinafsi sana au wachoyo au ni wanaroho ngumu tu. mimi mbona siwezi kumuona mtu anakufa njaa afu nina hela mfukoni basi nitatoa tu kiroho safi.

Binafsi naona utunzaji wa pesa ni kipaji kama vipaji vingine kama hujajaaliwa na Mungu huwezi, utaishia kujilaumu tu kulaumiwa.
 
Tatizo kushindwa kudhibiti tamaa na kutokuweza kukubaliana na shida mlizonazo.
Ukidhibiti tamaa basi utafanikiwa vingi. Simamia msimamo malengo yako.

Unataka kuweke weka! Ukiwa na msimamo kwenye mambo yako hakuna kinachoshindikana. Hata kama unaingiza buku unaweza kusave mia mía hadi ukatimiza lengo.

Tamaa inatuponza

Tamaa ya pesa, tamaa ya umaarufu..tamaa ya Uongozi. Very Deadly things
 
we..kidogo unaanza kunifungua macho sasa..kivipi nifafanuli mkuu
Iko hivi mkuu, usianze kutunza pesa nyiiingi wakati bado haijawa tabia yako. Kwanza anza na pesa za sarafu mia, mia mbili, hamsini jero nk. Ukirudi home rushia chenji zote ulizonazo mahali endelea na mambo yako. Kesho tena hivyo hivyo nk.

Utajikuta unaanza kusahau ziko kiasi gani mwisho mahitaji yanaanza kutokuzihitaji zile sarafu mpaka kipindi umesema utahesabu unaenda kufungua laaaah haulaaa million.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we..kidogo unaanza kunifungua macho sasa..kivipi nifafanuli mkuu
Ningeweka picha ya pesa ninavyoweka ila sitokuwa salama coz kuna ndugu zangu kadhaa wanajua wataona. Ila mm kwa sasa naweka hata kwenye kindoo kidogo simple tu mpaka kinajaa hata kama ni miaka 2 ndo nahesabu. Mwaka jana mfano nilikuwa na visado vinne
1. Kimejaa jero jeroo
2. Kimejaa 200 mia 2
3. Mia mia na
4 hamsini hamsini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa na uwezo huo usingeweza kuishia kuandika mistari mitatu iliyojaa majivuno na kusepa. Umemsaidiaje mleta Uzi?
Nonsense!

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko hivi mkuu, usianze kutunza pesa nyiiingi wakati bado haijawa tabia yako. Kwanza anza na pesa za sarafu mia, mia mbili, hamsini jero nk. Ukirudi home rushia chenji zote ulizonazo mahali endelea na mambo yako.

Kesho tena hivyo hivyo nk. Utajikuta unaanza kusahau ziko kiasi gani mwisho mahitaji yanaanza kutokuzihitaji zile sarafu mpaka kipindi umesema utahesabu unaenda kufungua laaaah haulaaa million.
Msaada unaanzia hapo mkuu usipanic.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom