Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 136
Vitendo vya wasimamizi wa uchaguzi ni vitendo vya Tume kwani wale wanafanya kazi kwa niaba yake na hivyo inawajibika kwa matendo yao maovu.
vitendo vya wasimamizi wa uchaguzi ni vitendo vya Tume kwani wale wanafanya kazi kwa niaba yake na hivyo inawajibika kwa matendo yao maovu.
Ni kweli. hivyo ndivyo commonsense inavyoelekeza. Lakini ikitokea msimamizi aka-misbehave tume itamtetea na huna pa kuishtaki. Ikishindwa kumtetea itasema ni kosa la msimamizi mwenyewe. Na ndivyo CCM inavyofanya, "CCM si chama chha mafisadi japo baadhi ya Wanachama ni mafisadi."
Ndugu yangu tusifanye ubishi katika masuala haya. Ninazungumza kama mwanasheria na ndivyo sheria inavyosema kuwa kitendo cha wakala knahusishwa moja kwa moja na mkuu wake (principal). Ninajitahidi kuelimisha watu hapa ili watu waelewe sizungumzi tu kwa misingi ya mantiki au akili za kawaida ninatumia sheria. ..................................................
Mahakama Kuu ndiyo Mahakama inayosikiliza kesi zote zinazohusiana na mambo ya uchaguzi na hata uamuzi huo hapo unasema hivyo. Lakini naomba nikutajia vilevile ibara za katiba ya nchi yetu:Mkuu Ruge, nikikusudia kufanya ubishi maana yake muda wote nilioutumia hapa umepotea bure na nisingekuwa na haja ya kunukuu katiba. Binafsi nashukuru kwa uelimishaji unaotupatia hapa. Concern yangu ni uwazi na uwezo wa sheria unazozitaja katika kushighulikia haya tunayoyasema. Nikuulize maswali mawili (unijibu kwa mujibu wa sheria zilizopo):
- Kukiwa na ushahidi kuwa mgombea mmoja wa urais kachakachua na tume ikamtangazia ushindi, ni mahakama gani inaweza kusikiliza kesi hii ili maamuzi yawe ni kutengua ushindi wa mchakachuaji? Ukiweza kunipatia na kifungu cha sheria au katiba kinachoidhinisha mahakama hiyo kusikiliza kesi ntashukuru zaidi.
- Ikiwa msimamizi wa uchaguzi akahongwa na mmoja wa mmoja wa wagombea uongozi (urais, ubunge au udiwani) ni akina nani watashtakiwa?
Mahakama Kuu ndiyo Mahakama ......................................................Na baada ya hapo mahakama itatoa amri kuwa yule msimamizi afunguliwe kesi ya kutoa rushwa na TAKUKURU.
Pale mdai atakapofungua kesi atakuwa anatoa hoja kwamba sheria za nchi zilikiukwa na hivyo kujenga mazingira ya kesi kusikilizwa. Ni kweli kabisa kuwa upande wa serikali utatoa pingamizi kuwa mahakama aina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Lakini upande wa mdai utatoa maelezo ya kuonyesha kukiukwa kwa sheria na hivyo kuipa madaraka mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Na kitu kingine ni kuwa kesi hii itakuwa ni ya kikatiba kudai kukiukwa kwa haki ya mtu kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa nchi katika uchaguzi ambao ni huru na wa haki.Mkuu Ruge, nashukuru kwa kutumia muda wako kutoa ufafanuzi wa kina. Nakubaliana nawe juu ya hukumu ya makosa ya Rushwa katika swali langu la pili. Nimeridhishwa na ufafanuzi wako kuwa kosa tajwa ni la jinai hivyo linashugulikiwa kwa utaratibu ulioutaja.
Bado mgogoro wangu (najaribu kujiuliza ikiwa naelewa vizuri maelezo yako, naridhika kuwa naelewa) uko katika uwezo wa mahakama kuu KUSIKILIZA kesi ya maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maana kwamba kama Mahakama hiyo inaweza kusikiliza kesi hiyo je ibara ya 74(12) ya katiba inazuia nini? (Nauliza hivi kwa kuwa Mahakama Kuu kabla ya Kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa katiba, ni lazima ijiulize juu ya uwezo wake wa kusikiliza kesi yenyewe). Sharti la kuamua kuwa ina uwezo wa kuisikiliza kesi ya Tuhuma dhidi ya Matokeo ya tume ya Taifa ya Uchaguzi halithibishwi na "Evidence" za kuchakachua au kutochakachua bali ni kwa "Evidence" ya uwezo wa kikatiba kusikiliza kesi hii.
Mahakama kuu ikiamua kusikiliza kesi dhidi ya Matokeo yaliyotangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa kuwa "kuna ushahidi wa wazi wa uchakachuaji" then itakuwa imekwishaamua kuwa ina mamlaka ya kusikiliza na kwamba zuio la katiba halifanyi kazi kwa mazingira hayo. Isiposikiliza kesi hii basi ni lazima sababu iwe ni kutokuwa na uwezo kwa mujibu wa katiba na si "kutokuwepo na ushahidi wa kuchakachua" kwa kuwa suala la kutokuwepo na ushahidi si suala la kutamka tu bali suala la mjadala wa kisheria (kesi). Sasa katika mazingira haya ibara ya 74(12) ya katiba inaizuia Kushtakiwa tume katika mazingira gani?
Naamini nimeeleweka. Kama sijaelewa au kueleweka naamini wana jamvi watasaidia.
Pale mdai atakapofungua kesi atakuwa anatoa hoja kwamba sheria za nchi zilikiukwa na hivyo kujenga mazingira ya kesi kusikilizwa. Ni kweli kabisa kuwa upande wa serikali utatoa pingamizi kuwa mahakama aina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Lakini upande wa mdai utatoa maelezo ya kuonyesha kukiukwa kwa sheria na hivyo kuipa madaraka mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Na kitu kingine ni kuwa kesi hii itakuwa ni ya kikatiba kudai kukiukwa kwa haki ya mtu kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa nchi katika uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
Je Mkuu Ruge waweza kuniambia sasa ibara ya 74(12) ya katiba:
"Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."
Inakataza nini?
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
Hapo Nyerere alipotoka kutokana na jazba.Kwa Mungu ndiko rufaa na hana sifa ya kutosikia au kutosikiliza.Asante kwa mchango wako Mkuu Pakawa. Naamini 2015 CCM watarudisha sehemu kubwa sana ya majimbo yao yaliyokwenda upinzani, tena hata kwa ghilba. Tutaongea haya haya tena. Tuombeane uzima.
Nimnukuu Nyerere, "Tunataka Wakoloni watupe Uhuru wetu. Wasipotupa tutawashtaki Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa wasipotusikiliza tutawashtaki kwa Mungu. Mungu asipotusikiliza tutawashtaki kwa shetani."
Mbinu ambazo zinatumika hata na wenzetu duniani ni:-3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
Mkuu 3D
umechambua vizuri lakini, Mie naomba niweke mawazo yangu kwa somo nililolipata MUAFAKA WA CCM NA CAF ZANZIBAR,,kuna wanachama waliojitolea maisha yao, waliuwawa, kuna wengine walienda ukimbizini mpaka SOMALIA kwa kusimamia HAKI je sasa hivi CCM na CAF wanakula BATA je HAWA watu waliwakumbuka, kabla ya huo muafaka wao ni kwanini wasingewafikiria waliokimbia nji na walio uwawa
MWANAKIJIJI anachojaribu kutafadhalisha kama nimemuelewa vizuri zitumike njia mbadala; Haihitaji akili ya kushe kuelewa kwamba UCHAGUZI HAUKUWA WA HAKI NA HURU lakini unataka wananchi wahamasishwe waende barabarani??Hilo halitakuwa na tija sio kwa CHADEMA Wala TAnzania kwa ujumla