Elections 2010 Kutumia nguvu (violence) kwenye siasa kunaruhusiwa

Vitendo vya wasimamizi wa uchaguzi ni vitendo vya Tume kwani wale wanafanya kazi kwa niaba yake na hivyo inawajibika kwa matendo yao maovu.
 
vitendo vya wasimamizi wa uchaguzi ni vitendo vya Tume kwani wale wanafanya kazi kwa niaba yake na hivyo inawajibika kwa matendo yao maovu.

Ni kweli. hivyo ndivyo commonsense inavyoelekeza. Lakini ikitokea msimamizi aka-misbehave tume itamtetea na huna pa kuishtaki. Ikishindwa kumtetea itasema ni kosa la msimamizi mwenyewe. Na ndivyo CCM inavyofanya, "CCM si chama chha mafisadi japo baadhi ya Wanachama ni mafisadi."
 
Ndugu yangu tusifanye ubishi katika masuala haya. Ninazungumza kama mwanasheria na ndivyo sheria inavyosema kuwa kitendo cha wakala knahusishwa moja kwa moja na mkuu wake (principal). Ninajitahidi kuelimisha watu hapa ili watu waelewe sizungumzi tu kwa misingi ya mantiki au akili za kawaida ninatumia sheria. Uamuzi huo wa majaji ulitokana na matendo mabovu ya wasimamizi wa uchaguzi, tume na viongozi wa CCM. Yote hayo ndiyo mahakama iliyakemea na kuubatilisha. Kama hufahamu maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ni sheria na yanatakiwa kufuatwa.
 
Ndugu yangu tusifanye ubishi katika masuala haya. Ninazungumza kama mwanasheria na ndivyo sheria inavyosema kuwa kitendo cha wakala knahusishwa moja kwa moja na mkuu wake (principal). Ninajitahidi kuelimisha watu hapa ili watu waelewe sizungumzi tu kwa misingi ya mantiki au akili za kawaida ninatumia sheria. ..................................................

Mkuu Ruge, nikikusudia kufanya ubishi maana yake muda wote nilioutumia hapa umepotea bure na nisingekuwa na haja ya kunukuu katiba. Binafsi nashukuru kwa uelimishaji unaotupatia hapa. Concern yangu ni uwazi na uwezo wa sheria unazozitaja katika kushighulikia haya tunayoyasema. Nikuulize maswali mawili (unijibu kwa mujibu wa sheria zilizopo):

  1. Kukiwa na ushahidi kuwa mgombea mmoja wa urais kachakachua na tume ikamtangazia ushindi, ni mahakama gani inaweza kusikiliza kesi hii ili maamuzi yawe ni kutengua ushindi wa mchakachuaji? Ukiweza kunipatia na kifungu cha sheria au katiba kinachoidhinisha mahakama hiyo kusikiliza kesi ntashukuru zaidi.
  2. Ikiwa msimamizi wa uchaguzi akahongwa na mmoja wa mmoja wa wagombea uongozi (urais, ubunge au udiwani) ni akina nani watashtakiwa?
 
Mahakama Kuu ndiyo Mahakama inayosikiliza kesi zote zinazohusiana na mambo ya uchaguzi na hata uamuzi huo hapo unasema hivyo. Lakini naomba nikutajia vilevile ibara za katiba ya nchi yetu:

Ibara ya 33 (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria kwa ajili ya-
(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;

(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;

(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.

NA
ibara ya 108.-(1) Kutakuwa na Mahakama Kuu ya JamhuriI ya Muungano (itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama Kuu") ambayo mamlaka yake yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.

(2) Iwapo Katiba hii au sheria nyingine yoyote haikutamka wazi kwamba shauri la aina iliyotajwa mahususi litasikilizwa kwanza katika Mahakama ya ngazi iliyotajwa mahsusi kwa ajili hiyo, basi Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la aina hiyo. Hali kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutekeleza shughuli yoyote ambayo kwa mujibu wa mila za kisheria zinazotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu.

Isipokuwa kwamba masharti ya ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri mamlaka ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kama ilivyoelezwa katika Katiba hii au katika sheria nyingine yoyote.

Sasa suala la hongo:

Hilo ni kosa la jinai na vilevile ni kosa dhidi ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985. Wanaoshtakiwa hapo ni mgombea uraisi, Tume, Msimamizi wa Uchaguzi, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwanasheria Mkuu wa serikali anashtakiwa kwani yeye ndiye anakuwa wakili wa Msimamizi wa Uchaguzi na Tume. Msimamizi na tume wanashtakiwa kwani kisheria wanawajibika kwa unafsi na umoja wao. Cha maana hata hivyo ni kuwa kosa la huyo msimamizi ni kosa la tume na hivyo pindi ikibainika kuwa alitenda kosa hilo basi mahakama itatengua uchaguzi huo kama yule aliyehonga ndiye alishinda. Na baada ya hapo mahakama itatoa amri kuwa yule msimamizi afunguliwe kesi ya kutoa rushwa na TAKUKURU.
 
Mahakama Kuu ndiyo Mahakama ......................................................Na baada ya hapo mahakama itatoa amri kuwa yule msimamizi afunguliwe kesi ya kutoa rushwa na TAKUKURU.

Mkuu Ruge, nashukuru kwa kutumia muda wako kutoa ufafanuzi wa kina. Nakubaliana nawe juu ya hukumu ya makosa ya Rushwa katika swali langu la pili. Nimeridhishwa na ufafanuzi wako kuwa kosa tajwa ni la jinai hivyo linashugulikiwa kwa utaratibu ulioutaja.

Bado mgogoro wangu (najaribu kujiuliza ikiwa naelewa vizuri maelezo yako, naridhika kuwa naelewa) uko katika uwezo wa mahakama kuu KUSIKILIZA kesi ya maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maana kwamba kama Mahakama hiyo inaweza kusikiliza kesi hiyo je ibara ya 74(12) ya katiba inazuia nini? (Nauliza hivi kwa kuwa Mahakama Kuu kabla ya Kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa katiba, ni lazima ijiulize juu ya uwezo wake wa kusikiliza kesi yenyewe). Sharti la kuamua kuwa ina uwezo wa kuisikiliza kesi ya Tuhuma dhidi ya Matokeo ya tume ya Taifa ya Uchaguzi halithibishwi na "Evidence" za kuchakachua au kutochakachua bali ni kwa "Evidence" ya uwezo wa kikatiba kusikiliza kesi hii.

Mahakama kuu ikiamua kusikiliza kesi dhidi ya Matokeo yaliyotangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa kuwa "kuna ushahidi wa wazi wa uchakachuaji" then itakuwa imekwishaamua kuwa ina mamlaka ya kusikiliza na kwamba zuio la katiba halifanyi kazi kwa mazingira hayo. Isiposikiliza kesi hii basi ni lazima sababu iwe ni kutokuwa na uwezo kwa mujibu wa katiba na si "kutokuwepo na ushahidi wa kuchakachua" kwa kuwa suala la kutokuwepo na ushahidi si suala la kutamka tu bali suala la mjadala wa kisheria (kesi). Sasa katika mazingira haya ibara ya 74(12) ya katiba inaizuia Kushtakiwa tume katika mazingira gani?

Naamini nimeeleweka. Kama sijaelewa au kueleweka naamini wana jamvi watasaidia.
 
Pale mdai atakapofungua kesi atakuwa anatoa hoja kwamba sheria za nchi zilikiukwa na hivyo kujenga mazingira ya kesi kusikilizwa. Ni kweli kabisa kuwa upande wa serikali utatoa pingamizi kuwa mahakama aina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Lakini upande wa mdai utatoa maelezo ya kuonyesha kukiukwa kwa sheria na hivyo kuipa madaraka mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Na kitu kingine ni kuwa kesi hii itakuwa ni ya kikatiba kudai kukiukwa kwa haki ya mtu kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa nchi katika uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
 
Je Mkuu Ruge waweza kuniambia sasa ibara ya 74(12) ya katiba:

"Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."

Inakataza nini?
 
Lengo lake ilikuwa ni kuzuia mtu yeyote kupinga maamuzi ya Tume. Hiyo ni kawaida ya sheria nyingi duniani lakini mahakama huru huwa hazikubali vifungu hivyo kwani vinaingilia mamlaka ya mahakama. Mahakama inasema tu kuwa uamuzi wa Tume au chombo chochote kile cha kisheria ni lazima ufanywe kwa misingi ya kikatibakisheria. Kama unafanywa hivyo basi hakuna anayeweza kuupinga lakini pindi unapofanywa kinyume cha sheria au katiba basi unapingwa.

Na hiyo ndiyo hoja yangu kwamba maamuzi na vitendo vingi vya tume kuhusiana na uchaguzi wa Rais vilikuwa kinyume cha sheria, katiba na hivyo uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
 
3D nadhani ni kati ya wale waramba viatu wa mafisadi au fisadi mwenyewe. Hata hivyo amepoteza muda mwingi kujibu 'propaganda' mfu kwa propaganda mfu na chafu. Hakuna la maana analotaka kusema. Anasema Slaa asituharibie nchi. Nchi iharibike mara ngapi iwapo inatawaliwa na wezi wa mchana wanaojulikana? Nchi iharibike mara ngapi inapobambikiwa rais atokanaye na ufisadi, uongo, usanii, uchakachuaji, udugu, kujuana, kuhongana na jinai nyingine nyingi?

Bahati mbaya sina muda, ningemjibu huyu gendaeka inavyopaswa. Muhimu ni kumpuuzia kwa vile tunajua ima ni fisadi mwenyewe ua ajenti wao. Hawa ni wachumia matumbo wayatumiayo kufikiri badala ya vichwa. Pole sana 3D.
 
HONGERA WACHANGIAJI WOTE WA MADA HII! Hii ndiyo mijadala inayohitajika hapa jamvini,unasoma na unaelimika.

Nimesoma makala kiasi za mwanakijiji na kwa sasa napitia MEREMETA report, naamini ni mtu aliye na machungu na nchi hii.

SLAA ameshindwa lakini kwangu mimi na nimeandika katika thread nyingine humu ndani ni kuwa kwa ujumla ameshinda kwa kuweza kuongeaza wabunge na madiwani.

Tusitumbukie katika mtego na ikaonekana kuwa yeye ni mtu wa fujo, njia mbadala zipo na watu watafakari kwa umakini.

Maisha ni lazima yaendelee na mapambano yaendelee katika sehemu husika.
 
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
 
- JF bwana kiboko yao, hapa mtumzima ni kusuka au kunyoa!

FMEs!
 
Hata tufanyeje.... Tanzania haitabadilika bila vurugu na damu kumwagika, hayo ndiyo mapinduzi kama ya kina Lenin na wengineo... na chanzo kikubwa cha haya mapinduzi ni mabwaneyenye... of which Kinana, Kikwete, Lowassa, Roastam ndio wenyewe

Ila tu naamini nguvu ya umma si lazima ionekane wakati wa kupiga kura, hililinatakiwa kuwa vuguvugu la kudumu until the old lady sings
 
Hii damu ya kumwagika ya nani hasa? Maana kule Kenya siyo Kibaki wala Raila aliyemwaga damu! Hata Zimbabwe Morgan tunaweza kusema alimwaga damu.. but guess what? Mugabe hakumwaga damu.!
 
Ukimshitaki mtu ambaye anahakika hana kosa,ataicha mahakama itende kazi yake kwa uhuru. Lakini ukimshitaki mtu ambaye anajua anamakosa, hawezi kuruhusu haki itendeke, hasa kama majaji nao anawateua-ni maoni yangu tu wana JF.
 
Asante kwa mchango wako Mkuu Pakawa. Naamini 2015 CCM watarudisha sehemu kubwa sana ya majimbo yao yaliyokwenda upinzani, tena hata kwa ghilba. Tutaongea haya haya tena. Tuombeane uzima.

Nimnukuu Nyerere, "Tunataka Wakoloni watupe Uhuru wetu. Wasipotupa tutawashtaki Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa wasipotusikiliza tutawashtaki kwa Mungu. Mungu asipotusikiliza tutawashtaki kwa shetani."
Hapo Nyerere alipotoka kutokana na jazba.Kwa Mungu ndiko rufaa na hana sifa ya kutosikia au kutosikiliza.
Pamoja na hivyo usikilizaji wake wa mashataka ya waja wake si lazima uwe kwa namna vile mwenye kushtaki anavyotaka.Viumbe tuna upeo finyu sana juu ya mambo yajayo.Twaweza kuchukia jambo ikawa ndio kheri kwetu na kinyume chake.
Mungu katika kuitikia huangalia na hali ya huyo muombaji na hicho kinachoombwa.Kwa ujumla wake anachokupatia ndicho bora kwako.
Iwapo hao waombaji ni watu wenye hadhi ya kuomba na kusikizwa kwa namna kwamba hawana makosa yanayozuia dua kukubaliwa, basi watakachokipata kitakuwa bora na cha kuwapendezesha.Kwa upande mwengine iwapo waombaji ni watu wasiostahiki kusikizwa dua zao,mfano watu wenyewe ni waovu na hata maombi yenyewe yanafanyika maeneo maovu na kwa njia ovu basi watakachopata hakitowapendeza lakini itakuwa ndicho bora kwao,ili wazinduke na kuwa wema.Watapata shida kwa kitu hicho na kuteseka nacho hatimae watajirudi makosa yao.
 
3D - Ni mbinu gani za matumizi ya nguvu (violent methods) ambazo unafikiri zinafaa kutumika sasa hivi Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi? Na kati ya hizo ni zipi wewe uko tayari kuzitumia ili kufikia malengo ya kisiasa.
Mbinu ambazo zinatumika hata na wenzetu duniani ni:-
1.migomo ya wafanyakazi na wanafunzi
2.maandamano ya watu wote
hizi ni njia mbili ambazo zikitumika huwa zinaleta matokeo mazuri daima, mfano hugo chaves alivyopinduliwa wananchi waliandamana bila kikomo wakahama majumbani mwao wakahamia barabarani mwisho chaves akarudi madarakani,pia kumbuka afrika ya kusini namna wanachi walivyopigana kufa kupona kuupinga ubaguzi wa rangi na wakafanikiwa, mimi hiki kijineno cha amani naanza kukichukia kwa sababu ndicho kinachohalalisha zuluma kwa mtanzania.NIONAVYO MIMI WAKATI SASA UMEFIKA WATU TUAMUE KAMA WALIVYOWAHI KUAMUA WATU WA THAILAND HAPO TUTAFANIKIWA.KUMBUKA UPOLE WETU UNALETA DHULUMA KWETU NA SUBIRA YETU YA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI NDO KASI YA KUIBIWA KWA RASILIMALI ZETU.TUUNGANE PAMOJA TUFANYE MAAMUZI YA PAMOJA ILI TUSHINDE KWA PAMOJA.
MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
AMEN!
mimi niko tiyari kwa maandamano
 
Nafikiri kwasasa hakuna tunachoweza kufanya bali kukubaliana na kilichofanywa na kukubali kuendelea na miaka mingine 5 ya usanii na ujanjaujanja.Kwa namna composition ya bunge ilivyo sidhani kama kuna mabadiliko yoyote katika katiba hasa kwenye vipengele vinavyohusu uchaguzi na tume ya uchaguzi vinavyoweza kubadilishwa. wasiwasi wangu ni kwamba tunaweza kuingia kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kama tulivyoingia kwenye uchaguzi huku mazingira yanayoruhusu kuwepo na uchaguzi huru na haki yakiwa hayapo. Swali langu,je kama wananchi tunapaswa tufanye nini ili haya tuliyoyashuhudia katika uchaguzi wa mwaka huu na miaka mingine iliyopita tangu tumeingia kwenye mfumo wa vyama vingi yasijitokeze tena kwa kiwango cha kutisha kama ilivyokuwa mwaka huu?
 
Mkuu 3D

umechambua vizuri lakini, Mie naomba niweke mawazo yangu kwa somo nililolipata MUAFAKA WA CCM NA CAF ZANZIBAR,,kuna wanachama waliojitolea maisha yao, waliuwawa, kuna wengine walienda ukimbizini mpaka SOMALIA kwa kusimamia HAKI je sasa hivi CCM na CAF wanakula BATA je HAWA watu waliwakumbuka, kabla ya huo muafaka wao ni kwanini wasingewafikiria waliokimbia nji na walio uwawa

MWANAKIJIJI anachojaribu kutafadhalisha kama nimemuelewa vizuri zitumike njia mbadala; Haihitaji akili ya kushe kuelewa kwamba UCHAGUZI HAUKUWA WA HAKI NA HURU lakini unataka wananchi wahamasishwe waende barabarani??Hilo halitakuwa na tija sio kwa CHADEMA Wala TAnzania kwa ujumla

Ningependa mwanakijiji angekuja na angalau mfano hai wa nchi gani iliyokuwa ya kidikteta ilitumia njia mbadala zaidi ya nguvu ya uma kuingiza serikali halali ya wanainchi bila mizengwe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom