Kutumia majina ya waume zetu

Siri Sirini

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
547
198
Samahanini kama si mahala pake, me hki kitu kinanichanganya, husika na kichwa cha habari, mfano me naitwa Mary Andrew Katundu, nimeolewa na Richard Moses Mkumbukwa, je itabidi niitwe Mary Richard Mkumbukwa au Mary Andrew Richard? Mana kwenye kadi zangu za bank na vitambulisho nimetumia ubini wa baba mana nilikuwa bado sijaolewa, je naweza badilisha nitumie ubini wa mume?
 
Ni utashi wa muhusika, hakujatokea act yeyote toka mjengoni iliyosema kubadili/kutobadili jina baada ya ndoa ni sheria.
 
hubadili jina la baba, unabadili jina la ukoo kama unapenda.

Mfano, huyu dada anaweza amua kuitwa Mary Andrew Mkumbukwa.
 
Mfano hai uko kwako Mkuu !
Gender yako MTIHANI !
Hata Mods hawaijui !
Kwani Mungu hakuoni ?
Anakuona ujue...
 
Ubaki na jina lako bhana... utasumbuka hapo baadae kwenye mambo fulani, huwa vinasumbua. wewe mtaani jiite tu mama Mkumbukwa, lakini usibadili kwenye documents zako za kazi, nk.
 
hayo mambo ya kubadili jina yanaishia mtaani,kwenye kamati za harusi na vyama vya kina mama.ukibadili hadi kiofisho inasumbua sana
 
i will never change my name! period! kesho keshokutwa tumedivorce, nafuta tena majina ya mume wa zamani, naweka ya mume mpya YM! GOD FORBID!
 
Hahhaha! Nimeona mdada anaitwa say Mary Lyimo Massawe!
Kazi kweli! Kwani kubadili jina ni muhimu? For what reason? Mi nataka kuandika Mama Nyambilee
 
ubadili jina usibadili wewe ni mkewe tu.....

Wengine hatujabadili huko maofisini, ingawa kote wanajua kuwa ni mrs fulani.....

Ila kujibu swali lako unapaswa kuitwa Mary Katundu Mtambukwa.... Jina la ukoo wako liwe katikati, ukijiita mary richard mtambukwa, richard ni baba yako? Hapana.

Kiusahihi ni mary katundu mtambukwa
 
Hahhaha! Nimeona mdada anaitwa say Mary Lyimo Massawe!
Kazi kweli! Kwani kubadili jina ni muhimu? For what reason? Mi nataka kuandika Mama Nyambilee

hakuna umuhimu, ni kukompliketi maisha tu.....ubadili usibadili haibadilishi kuwa nyie ni mke na mume...
 
Samahanini kama si mahala pake, me hki kitu kinanichanganya, husika na kichwa cha habari, mfano me naitwa Mary Andrew Katundu, nimeolewa na Richard Moses Mkumbukwa, je itabidi niitwe Mary Richard Mkumbukwa au Mary Andrew Richard? Mana kwenye kadi zangu za bank na vitambulisho nimetumia ubini wa baba mana nilikuwa bado sijaolewa, je naweza badilisha nitumie ubini wa mume?

Kubadili jina haijalishi, imagine jina lenyewe kilivyo "mrs. Mkumbukwa"

Baki na jina ulopewa na wazazi wako.

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Naona huko mbeleni tutaulizana mtoto wa kwanza ni mali ya nani

Waswahili husema ukitaka kumla bata usimchunguze sana,na kadri haya mambo ya ndoa yanavyojadiliwa ndivyo pia ugumu wa ndoa unavyoongezeka,hizi ndoa hipo siku hazitamake tena make watu wanaanza kuhoji na kutaka kujua kila kitu

Nakumbuka mke wa Dr.Leakey aliitwa Mary Leakey pia ...kuna tatizo??
 
mi sibadili jina na wala sion umuhim wake, iyo ilikuwa zaman sana, jina la mume wangu nitaitwa kanisan
 
Ubaki na jina lako bhana... utasumbuka hapo baadae kwenye mambo fulani, huwa vinasumbua. wewe mtaani jiite tu mama Mkumbukwa, lakini usibadili kwenye documents zako za kazi, nk.

hakuna usumbufu wowote, sheria za uraia "uhamiaji" zinatambua hili pia. Kitu cha muhimu vyeti vyako ulivyovipata baada ya kuhitimu masomo usivibadili majina, document kama passport inaweza ikawa na surname ya baba yako au mumeo inategemea unapenda kutumia ipi, lakini ukitumia ya mumeo utahitajika kuamnatanisha cheti cha ndoa ambacho ndio pekee kinachoweza kutabanaisha uhalali wa majina yako kubadilika.
 
Sasa yote ya nini? kutembea na cheti cha ndoa.
 
i will never change my name! period! kesho keshokutwa tumedivorce, nafuta tena majina ya mume wa zamani, naweka ya mume mpya YM! GOD FORBID!

Kwa nini unawaza divorce wakati umekubali kuolewa na unayempenda na yeye anakupenda..unless kama umelazimishia kama wadada wengi wanavyofanya siku hizi.. Stop being negative...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom