Kutongoza ni sifa ya kiume

Kutongoza ni sifa ya kiume

Katika zama hizi za utandawazi uliotuacha wazi, jinsia ya kiume imekuwa ikikumbana na changamoto nyingi. Katika kuutetea na kulinda uanaume-asilia kuna masuala ambayo hatuna budi kuyajadili kinagaubaga. Mojawapo ni hili la kutongoza.

Teknolojia imerahisisha sana mawasiliano, siku hizi watu hawatongozani tena. Wanaume wamekuwa wazito kutumia stadi na mbinu za asili katika kuwasilisha nia. Na kundi jingine limekuwa viwete kabisa kwenye kutongoza.

Wapo wanaodhani kuwa wanawake wanachukia kutongozwa, lakini kumbe si kweli. Kwa asili wanawake wanapenda kutongozwa. Bila kujali umri wao, wanapenda na wanahitaji kutongozwa. Na kimsingi kutongozwa ni sifa ya mwanamke. Inaonesha ukamilifu wa jinsia yake na kumuongezea hali ya kujiamini. Hata kama asipokukubalia, lakini anafurahia.

Kutongoza ni sifa ya kiume, hasa ikizingatia staha na mazingira ya faragha. Haifai kabisa mwanaume kuogopa kumtongoza mwanamke bila kujali status yake. Kutongoza kunaonesha nia, sababu na uwezo wa kutaka kuwa naye. Na pia kunaonesha hali ya kujiamini, hilo likifanyika katika mazingira tulivu na yenye faragha.

Ni nadra kumtongoza mwanamke anayejielewa hadharani akakubalia. Atakukatalia na mbaya zaidi atakuchukia.

Kutongoza ni jambo adhimu likizingatia muktadha, kwani humpa mwanamke nafasi ya kutathmini upeo wako, ufahamu wako, ustahimilivu na msimamo wako. Kutongoza humuonesha hali ya mamlaka na kujiamini kwako kama mwanaume; jambo ambalo ni turufu muhimu kwa mwanamke katika kujihakikishia usalama wake.

Kutoa zawadi kama vile hela, simu, mavazi nk. ni sehemu tu ya kuonesha hisia zako kwake, lakini bila kumtongoza kwa maneno na ushawishi anaweza kuwa na wewe kimwili huku hisia zake akiziwekeza kwa mwanaume mwingine mwenye mtaji wa maneno.

Kutongoza kunasaidia pia kutambua mwanamke unayetaka kuwa naye ni wa aina gani.

Kumbuka mwanamke unayemtamani leo, ni kama mteja adimu katikati ya lundo la wafanyabiashara wenye bidhaa za aina moja. Kuna wanaume kibao huko barabarani wanamtongoza. Kumshawishi aje kununua kwako, ni lazima uwe na kitu cha ziada. Huu uziada unaanzia kwenye kutongoza.

Moja ya sababu zinazochangia mahusiano ya kisasa kuwa 'delicate' ni pamoja na ombwe lilopo katika tasnia ya utongozaji. Watu wakishapeana namba za simu kazi imekwisha. Kinachofuata ni kupanga muda na venue la mizagamuo.

Baadaye mapenzi yanakolea watu wanatangaza ndoa. Siku chache ndani ya ndoa moto unaanza kuwaka; baada ya kugundua yale ambayo hawakupata muda wa kuyavumbua.

Zamani ilikuwa lazima utongoze ili kummiliki mwanamke wa ndoto yako. Ukikaa kimya na yeye anakuchunia. Huku na kule utasikia kachukuliwa na mwamba wa mtaa wa pili. Na ukijitia kumlaumu anakupa ukweli wako.

"Nilikuwa nasubiri unitongoze nikaona kimya, ndo maana nikamkubalia Joze!"

Na majibu ya tongozo yalikuwa yanachukua miezi kadhaa na wakati mwingine hadi mwaka kabla ya mwanamke kukukubalia. Ina maana mpaka anapokukubalia, anakuwa amejiridhisha na wewe kwa mengi.

Vijana wa siku hizi hawana huo muda wa kusubiri. Na wanawake pia hawataki kabisa kumzungusha mwanaume. Chambo moja ndoana imenasa. Mpaka Fid Q akaamua kumwambia wa kwake, usinikubali haraka!

Ndipo wazungu wakaja na msemo wao; Easy come easy go!

HITIMISHO

Wimbi la vijana wanaohangaika kusaka nguvu za kiume kwa mazoezi makali ya kukomaza na kukuza misuli limekuwa kubwa. Wengine wanameza na kupaka madawa ya kuchochea hisia na kukuza maumbile. Lakini ukweli ni huu, misuli mikubwa si nguvu za kiume bali ni sehemu ya mwonokeno wa kiume. Vinginevyo ndoa/mahusiano ya watu wenye misuli mikubwa na nguvu nyingi zingekuwa hazitetereki.

Uanaume wa mwanaume timamu unaanzia kichwani. Yaani ufahamu wake, uwezo wa kutawala mazingira yake ya ndani na ya nje, uwajibikaji na kudhibiti hisia zake. Mwanaume ni mtawala, na utawala hautegemei misuli ya mwili zaidi ya akili inayojitambua.

Naam; kutongoza ni sehemu ya nguvu za kiume, kwajili ya mahusiano imara. Mdada, ukiona jamaa yuko busy kukupa mijizawadi lakini mdomo wake mzito, mshawishi akutongoze upate kusikia sera zake.

NB; Hii post haihusiani na udangajiView attachment 2763970
Nimeupenda sana huu uzi. Ni uhalisia
 
Kutongoza kuna raha yake ni uwezo wako wa kushawishi, sio kila mwanaume anajua kutongoza,kutongoza ni ujasiri, kutongoza ni kujiamini, naamini hata wanawake wanapenda kutongozwa dunia nzima.
 
Kutongoza kuna raha yake ni uwezo wako wa kushawishi, sio kila mwanaume anajua kutongoza,kutongoza ni ujasiri, kutongoza ni kujiamini, naamini hata wanawake wanapenda kutongozwa dunia nzima.
Wanaume siku hizi watongozi wengi wanatumia nguvu waliyonayo, pesa au urembo yaan mvutoo,
 
Wanaume siku hizi watongozi wengi wanatumia nguvu waliyonayo, pesa au urembo yaan mvutoo,
Mwanaume kutongoza ni sehemu ya maisha yake ni natural, kutongoza ni kushawishi, kushawishi ni kuongoza ikiwa mtongozwa ataelewa somo ni rahisi kuongozwa na kutawaliwa, strong woman huwezi mpata bila kumtongoza, imagine umekutana na mwanamke ametoka familia inayojiweza, kaenda shule, ana exposure, ana pesa, ni independent woman,anajiamini, atababaikia nini?!! utampataje kama kumtongoza huwezi, tuongee ukweli wanaume sisi wa siku hizi kutongoza ni shida uenda sababu ya teknolojia au ujasiri umepungua sana wengi utongozea kwenye simu, wakikutana game over!
Hawa waliotoka familia zenye changamoto au wanaoishi maisha yenye changamoto ni rahisi kubabaikia show-off za wanaume, mwanamke akiona mwanaume ana gari tu anachanganyikiwa.

Siku moja ijumaa natoka kazini nimempitia mshkaji wangu Mwanga Tower tunaenda mlimani Cinemax kucheki movie ile ya Kandahar ilikuwa ndio inaonyeshwa possibly ilikuwa tarehe 26 sijui ilikuwa May kitu kama hiko, binti katoka kazini nae jengo lile alipojirusha yule MC, akaomba lifti tukamwambia tunaishia mlimani akadai atashukia ifungila tulivyofika ifungila wakati anajiandaa kushuka akashukuru na kusema mna mioyo mizuri hata namba ya simu hamjaniomba, tukaishia kuangaliana na jamaa yangu...poor lady!
 
Ulishindwa kutumia u'naturally wa wanaume wa kutongoza tongoza, wanaume wa zamani akimuona demu yoyote mbele yake lazima amtongoze hata kama hamli, sasa ww umewaangusha mabahari hadi demu kajisemea mwenyewe kwa kuwashangaa nyie wanaume wa wapi
 
Back
Top Bottom