Kutongoza ni sifa ya kiume

foroy

Senior Member
May 2, 2018
186
288
Katika zama hizi za utandawazi uliotuacha wazi, jinsia ya kiume imekuwa ikikumbana na changamoto nyingi. Katika kuutetea na kulinda uanaume-asilia kuna masuala ambayo hatuna budi kuyajadili kinagaubaga. Mojawapo ni hili la kutongoza.

Teknolojia imerahisisha sana mawasiliano, siku hizi watu hawatongozani tena. Wanaume wamekuwa wazito kutumia stadi na mbinu za asili katika kuwasilisha nia. Na kundi jingine limekuwa viwete kabisa kwenye kutongoza.

Wapo wanaodhani kuwa wanawake wanachukia kutongozwa, lakini kumbe si kweli. Kwa asili wanawake wanapenda kutongozwa. Bila kujali umri wao, wanapenda na wanahitaji kutongozwa. Na kimsingi kutongozwa ni sifa ya mwanamke. Inaonesha ukamilifu wa jinsia yake na kumuongezea hali ya kujiamini. Hata kama asipokukubalia, lakini anafurahia.

Kutongoza ni sifa ya kiume, hasa ikizingatia staha na mazingira ya faragha. Haifai kabisa mwanaume kuogopa kumtongoza mwanamke bila kujali status yake. Kutongoza kunaonesha nia, sababu na uwezo wa kutaka kuwa naye. Na pia kunaonesha hali ya kujiamini, hilo likifanyika katika mazingira tulivu na yenye faragha.

Ni nadra kumtongoza mwanamke anayejielewa hadharani akakubalia. Atakukatalia na mbaya zaidi atakuchukia.

Kutongoza ni jambo adhimu likizingatia muktadha, kwani humpa mwanamke nafasi ya kutathmini upeo wako, ufahamu wako, ustahimilivu na msimamo wako. Kutongoza humuonesha hali ya mamlaka na kujiamini kwako kama mwanaume; jambo ambalo ni turufu muhimu kwa mwanamke katika kujihakikishia usalama wake.

Kutoa zawadi kama vile hela, simu, mavazi nk. ni sehemu tu ya kuonesha hisia zako kwake, lakini bila kumtongoza kwa maneno na ushawishi anaweza kuwa na wewe kimwili huku hisia zake akiziwekeza kwa mwanaume mwingine mwenye mtaji wa maneno.

Kutongoza kunasaidia pia kutambua mwanamke unayetaka kuwa naye ni wa aina gani.

Kumbuka mwanamke unayemtamani leo, ni kama mteja adimu katikati ya lundo la wafanyabiashara wenye bidhaa za aina moja. Kuna wanaume kibao huko barabarani wanamtongoza. Kumshawishi aje kununua kwako, ni lazima uwe na kitu cha ziada. Huu uziada unaanzia kwenye kutongoza.

Moja ya sababu zinazochangia mahusiano ya kisasa kuwa 'delicate' ni pamoja na ombwe lilopo katika tasnia ya utongozaji. Watu wakishapeana namba za simu kazi imekwisha. Kinachofuata ni kupanga muda na venue la mizagamuo.

Baadaye mapenzi yanakolea watu wanatangaza ndoa. Siku chache ndani ya ndoa moto unaanza kuwaka; baada ya kugundua yale ambayo hawakupata muda wa kuyavumbua.

Zamani ilikuwa lazima utongoze ili kummiliki mwanamke wa ndoto yako. Ukikaa kimya na yeye anakuchunia. Huku na kule utasikia kachukuliwa na mwamba wa mtaa wa pili. Na ukijitia kumlaumu anakupa ukweli wako.

"Nilikuwa nasubiri unitongoze nikaona kimya, ndo maana nikamkubalia Joze!"

Na majibu ya tongozo yalikuwa yanachukua miezi kadhaa na wakati mwingine hadi mwaka kabla ya mwanamke kukukubalia. Ina maana mpaka anapokukubalia, anakuwa amejiridhisha na wewe kwa mengi.

Vijana wa siku hizi hawana huo muda wa kusubiri. Na wanawake pia hawataki kabisa kumzungusha mwanaume. Chambo moja ndoana imenasa. Mpaka Fid Q akaamua kumwambia wa kwake, usinikubali haraka!

Ndipo wazungu wakaja na msemo wao; Easy come easy go!

HITIMISHO

Wimbi la vijana wanaohangaika kusaka nguvu za kiume kwa mazoezi makali ya kukomaza na kukuza misuli limekuwa kubwa. Wengine wanameza na kupaka madawa ya kuchochea hisia na kukuza maumbile. Lakini ukweli ni huu, misuli mikubwa si nguvu za kiume bali ni sehemu ya mwonokeno wa kiume. Vinginevyo ndoa/mahusiano ya watu wenye misuli mikubwa na nguvu nyingi zingekuwa hazitetereki.

Uanaume wa mwanaume timamu unaanzia kichwani. Yaani ufahamu wake, uwezo wa kutawala mazingira yake ya ndani na ya nje, uwajibikaji na kudhibiti hisia zake. Mwanaume ni mtawala, na utawala hautegemei misuli ya mwili zaidi ya akili inayojitambua.

Naam; kutongoza ni sehemu ya nguvu za kiume, kwajili ya mahusiano imara. Mdada, ukiona jamaa yuko busy kukupa mijizawadi lakini mdomo wake mzito, mshawishi akutongoze upate kusikia sera zake.

NB; Hii post haihusiani na udangaji
Screenshot_20230927-111722.jpg
 
1. Kwani wao wanasemaje kuhusiana na post yako?

2. Sasa mbona hitimisho limekuwa refu?

3. Huyo mwanamke mbona kajikuta anafungua vigungo vya nyonyo? Ina maana swaag alizotupiwa na mdau zimempelekea kuvutiwa kiasi cha kuvuta hisia zake zote za mwili. Asipoangalia watamaliziana hapohapo njiani
 
Mie sitongozi. Kwasababu sipendi COMMITMENTS hapa tuna FLIRT tu.... ukiingia kwenye MFUMO fresh.

Kutongozana/kuviziana/kukimbizana ni kwa wale wageni wa hizi show.

Kwanza sipendi kuongea UONGO. na mtu yeyote Mtongozaji ni MUONGO, Lazima aongee uongo ili ashawishi toto la mtu.
 
1. Kwani wao wanasemaje kuhusiana na post yako?

2. Sasa mbona hitimisho limekuwa refu?

3. Huyo mwanamke mbona kajikuta anafungua vigungo vya nyonyo? Ina maana swaag alizotupiwa na mdau zimempelekea kuvutiwa kiasi cha kuvuta hisia zake zote za mwili. Asipoangalia watamaliziana hapohapo njiani
Hahaaa... Wewe kama story teller hukupaswa kuniuliza swali namba mbili.
 
Mie sitongozi. Kwasababu sipendi COMMITMENTS hapa tuna FLIRT tu.... ukiingia kwenye MFUMO fresh.

Kutongozana/kuviziana/kukimbizana ni kwa wale wageni wa hizi show.

Kwanza sipendi kuongea UONGO. na mtu yeyote Mtongozaji ni MUONGO, Lazima aongee uongo ili ashawishi toto la mtu.
Na wanawake wanapenda uongo mtamu kuliko ukweli mgumu. Utapoteza fursa. Wape nyama ya ulimi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom