Kutongoza ni sifa ya kiume

Hivi kutongoza kukoje maana me kwa wote niliowah kuwa nao sikuwah kuwatongoza fanya vitu vitakavyowavutia mbn watajitongoza wenyewe kutongozana na kukimbizana ni jau muda mwingne 😀
 
Waafrika tunakwama wapiiii? ina mana kufanya mazoezi leo hii kumebeba dhana ya kutafuta nguvu za kiume
 
Fact
 
aje baharia mmoja hapa aweke muongozo kamili wa jinsi ya kutongoza wengine hatujui
Wazee wa zamani walikuwa wasanifu wazuri sana kwenye kutongoza.

Kama wiki mbili zilizopita nimeishuhudia hii pale ferry; vanguard nyeusi ilipoingia kwenye panton askari wa Suma JKT wakamuamuru dereva amshushe abiria kwani sheria ya kivuko hairuhusu abiria kubaki ndani ya gari isipokuwa dereva.
Sasa ukashuka mshangazi mmoja wa kwenda, ambao kwa alama na ishara zote alikuwa mke wa jamaa.

Pembeni yangu alikaa mzee mmoja wa makamo around 60 kwa makadirio. Akapiga 'Mashallah' kwa herufi kubwa!

Kama zali, huyo mwanamke akaja kukaa karibu yetu. Ile harufu ya manukato yake, mavazi yake ya gharama na lile umbo la kibantu vilitosha kutunyamazisha wote na kuishia kumeza mate, lakini haikuwa kwa huyo mzee.

Kwanza, alimpokea na kwa sifa babkubwa na kummwagia maua yake. Kisha nikamsikia akitema cheche....

"Mama, hii nyumba yako mashallah! Laiti nikipata nafasi ya kuishi humu ndani, wallah siwezi kuhama. Naomba unifanyie wepesi niwe mpangaji wako, maana najua siwezi kumiliki nyumba kama hii. Lakini nakuahidi, ntakuwa mpangaji mzuri na ntaihudumia hii nyumba kuliko unavyodhani.... "

Hiyo mistari iliniacha hoi. Na sikushangaa kuona mshangazi ukitoa namba ya simu huku ukichekelea nahau za mzee huyo, ambaye namjua kama muuza samaki tu pale magogoni.
 
utakuwa mtu kutoka pwani, ndio wana tunu hiyo!
 
Mnadanganyana tu hapa. Malaya ua khaba unamtongoza nini?

Mwanamke akishaamuwa kuufanya mwili wake ndiyo kiwanda chake kuna kutongoza hapo? Hapo kuna wateja wangapi tu alionao.

Kwenye biashara, kuna namna nyingi za biashara na unaiendesha vipi. Kuna who;esellers, kuna retailers, kuna major accounts, kuna targeted marketing. Kwa ufupi kuna kila aina na kila namna za kuifanya biashara.

Kuna anaeuza Rolls Royce na kuna anaeuza kibajaji, vyote vyombo vya usafiri lakini vina wayeja wake na namna zke.

Mwenye rolls Royce au Bentley anaweza kupanda kibajaji au bodaboda na akavipenda sana na kuvitumia mara kwa mara kuliko rolls Royce yake.

Mwanamme hata uwe mtongozaji vipi, bila turufu bure tu.

"Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…