Kutokukujua Kiingereza kumenifelisha kiasi cha kukosa madili kibao

Kutokukujua Kiingereza kumenifelisha kiasi cha kukosa madili kibao

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,042
Reaction score
16,872
Salaam JamiiForums

Natamani kujua vyema lugha ya Kiingereza.

Natamani ningeongea Kiingereza hata Kwa asilimia 50 tu naamini ningetisha sana.

Achana na stori hizi, eti tunakuza na kudumisha lugha yetu,mara tuwe wazalendo.

Acheni hizo kama hujawahi kusafiri kwenda nchi yoyote ya ughaibuni huwezi kulijua hili. Nilikosa zawadi ya laptop 5. Kwa kutojua lugha hii nikashindwa kuitafsiri lugha hii nikijua naagizwa kumbe napewa bure na wajapani, Mimi Kwa kutokujua nikakunja uso na kusema siwezi kuchunga vitu vya watu.

Lakini pia niliwahi kwenda ng'ambo nikatongoza mwanamke, akanikatalia kwakusema ana mume,sasa Mimi sikumwelewa nikajua kanikubalia,kama mjuavyo mzungu anakukatalia lakini anaendeleza urafiki na wewe,na ukimualika sehemu anakuja,sasa Mimi mtoto wa kimasikini na Kiswahili nikajua nimekubaliwa ,nikaanza kutuma tuma vijiemail mpaka aibu iliponipata bahati nzuri sikujaziwa watu.

Nyie wazungu wazuri,naamini wale ndiyo binadamu wanaozungumziwa kwenye vitabu vya dini.

Na nchi hiyo siyo nyingine ni Denmark, ina wanawake warembo hakuna mfano Wana jiji lao Kobinhavin kama watamkavyo warusi,halafu wewe tamka Coppen hagen inatosha.

Nyie yaani ukirudi Tanzania unaanza kumchukia hadi mkeo unamuona kama unaishi na mlugaluga ,siyo huyo tu ukishuka airport unagundua uko na watu toleo fulani lisiloridhisha.
(Wallah acha wazungu watubague tu)

Kuna watu wamekosa michongo na dili za maana Kwa kushindwa kuongea sentensi moja tu ya kiingereza.

Watu wengi ,na watanzania wengi wanajua kusoma na kuandika kiingereza vizuri ila ni vigumu kwao kuongea hii lugha kwa usahihi hata asilimia 30 acha kudumu zaidi ya dakika 10.

Lakini pia tunao watu kadhaa wanaojinasibu kuongea hii lugha tuwapo mtaani lakini hawahawa wakipewa dakika 3 tu mbele ya watu miambili ni mtiti.

Hali hii imefanya watu wengi kuichukia hii lugha na kuanza kuona si chochote,lakini ukweli ni kwamba English language ndiyo lugha ya Dunia hakuna lugha itakaa iishushe hii lugha iliyojichimbia kwenye mlima mreeeeefu wenye kilele kilichochongoka.

Tusiyaige mataifa yenye nguvu kama China, Russia nk.haya ni mataifa yenye nguvu,yaani yanaweza kujiamulia mambo yao kwakuwa wameweza kuwa na teknokojia kubwa na kuwa class .

Kitendo cha Mimi kukosa dili la pesa nyingi mwenye moja ya nchi za Asia Kwa kushindwa ,hii lugha huwa naumia sana,si hapo tu ,hata Waturuki wa Yap Merkez juzi kati hapa kama 3 years iliyopita nilipanga nao ishu lugha zikagongana ,siyo wao wanajua sana ni vile Mimi nilipaswq niwe najua zaidi hii lugha walinidumb kwa kushindwa kuongea kiingereza tu. Nikaamua kwenda ng'ambo lakini nako mara nyingi napigwa za uso kwani dili zangu hazihitaji mkalimani.

Nyingine ni hapa Tz kuna dili la maana zaidi lilishirikisha watu watano white people watatu Sisi black wawili sasa jamaa kuongea kiingereza hawawezi ila mtu ukiongea kiufasaha wanaelewa , kumbuka dili haihitaji mkalimani kwani ilikuwa ya usiri kidogo,basi tuliishia kutumbuliana macho,huku kila mtu akiwa kama kiziwi au bubu.dili likapeperuka.

Hapa naongelea kiingereza really siyo hizo broken zenu mnazorudia rudia maneno.hicho na Mimi naongea.tatizo ni pale unapokutana na mzungu asiyejua kiingereza vizuri, ni wewe unapaswa uwe unajua zaidi hapa ndipo dili linapopeperuka kama kindege kwenye Casino.

Lakini pia kuna mwanangu alikosa tenda ya kusupply bidhaa fulani Kwa kushindwa kuongea hii lugha.yaani zile dili fulani unapachikwa kisha maisha yanaendelea .

Ikabidi tumsake jamaa mmoja muongoza watalii kwenye hifadhi fulani akapata dili kilaini mno ,na kufanikiwa parefu sana, kwasasa ni mmoja wa Watu wenye vipato vizuri. Kuwa na Semi trailer zaidi ya 10 si mchezo.

Lakini kuna hii ,kuna wahuni walipanga kuuza vifaa (equipments) Kwa bei ya chini yaani nusu hasara,yaani Super Generator zaidi ya Mia na hamsini ,madalali tukajaa Kati halafu lugha gongana kwani mmiliki anaongea Portugal tu,halafu mnyamwezi anaonekana kapigika akataka auze atimkie kwao,sasa kwakuwa hii halikuwa dili la Siri likahitaji mkalimani.kulifanikisha

Jamaa mmoja akanisanua kuwa kuna mwana anaongea kireno kama kazaliwa hukohuko ,hivyo tukaona anaweza kusaidia ,so alivyofika Kwanza sikuamini kwani alikuja yard na miguu tulimuuliza akadai kakosa 1000 ya boda boda yaani mchizi alichoka kimaisha.tukampa mchapo kuwa tutamlipa Kwa kazi maalumu,ya lugha Tu mambo mengine tutarekebisha wenyewe.

Tukawapambanisha,Yule mreno alifurahi sana kuona jamaa anatereza na ile lugha,cha ajabu walituzunguka na kumalizana halafu Yule jamaa yetu akatuambia Yule jamaa kasema tusubiri baada ya wiki mbili.tukakubali si hatujui!!

Kumbe jamaa bwana aliingia mtaani akasaka wanunuzi na kwenda kule akapiga bingo ya maana,kiasi cha kubadilisha maisha Kwa siku moja
Just imagine unapiga 70 million kwa mpigo kwanini usifanye yako?

Ya mwisho ni hii ,wakati nipo site fulani kipindi cha mambo ya bwawa la Nyerere yanaanza ,nilikutana na mzungu mmoja ni binti mdogo ambaye alikuwa na haraka ya kufika Dar sasa akaomba lifts nikakubali, nikapanga kumtongoza,ili nifaidi dogodogo la kizingu sasa kila nikiongea akawa hanielewi halafu anaongea kiingereza kile cha kijerumani , mzungu Kwanza alikuwa Hana kitu ,sijui nini kilimpatq nikahisi aidha kuna vitu kapoteza lakini sikuwa na uhakika hadi leo, (kumbe aliwatoroka wenzake)

Tulifika kibiti mzungu akaniashiria ana njaa na hana pesa.nikaweka chuma pembeni ,nikatafuta sehemu ya kawaida ili tupate msosi,Kwanza mzungu hakuchagua chakula akawa anafakamia wali Maharage wa nazi huku kila dakika akionesha kushukuru kutokana na ukarimu wangu.kumbe wenzake wamegundua yupo na Mimi kwani wakati anapanda kuna watu walimuona ,Mimi baada ya kumaliza Kula Kwa kutumia ufundi wa Hali ya juu kikamuomba mzigo Yule mzungu kiishara kwanza alionesha hajapenda ila akawa kama kakubali kishingo upande,angefanyeje sasa na Hana kitu.nikapiga safari zangu nne za baridi nikijua nitaongeza ujasiri tu lazima tupige stori humo njiani siwezi kuwa na pisi halafu tupo kimya muda wote

Moyo ulilipuka Kwa furaha siyo kwamba sijawahi piga mzungu,ila ni Yule alikuwa dogodogo nywele nzuuuuuuri. Sasa wakati narudi kwenye chombo ili niwahi mjini nikasake lodge ya maana nifaidi yule mtoto,nikakuta mbele ya chombo changu kuna Gari ya watalii wazungu watatu pamoja na dereva wa kibongo,aisee Yule mzungu Mzee kuliko wote tall halafu giants likanikwida huku likinisogelea na kuanza kuniuliza maswali nisiyoyaelewa. Wenzake wakawa wanaongea Kwa sauti huku wakiniona kama jambazi Yule dereva akaniambia wanakuuliza binti Yao ulikuwa unampeleka wapi!!

Ndipo nikajitetea kwamba kaniomba msaada na pia alikuwa na njaa tunatoka Kula ,Yule dereva wao akawaelewesha wakaelewa.wakaniachia huku washanipiga mabao ya maana

Sema nini Elimu haina mwisho wakuu tuihifadhi hii lugha kwa wivu mkubwa inasaidia Sana kwenye hustle zetu za kila siku.
 
Watanzania tunajikua sema hatuna komfidensi. Kiingereza cha graduate akikiongea KWA ujasiri ni Bora kuliko hata cha hao wajapani na Wadenmaki.

Ukisikiliza usahili wa wachina, wajapani, wahindi, na watu ambayo kiingereza SIO lugha yao mama, wanaongea Brocken nyingi sana ila hawasiti Wala hawajishtukii Wala hawajali alafu wanaongea KWA kuririka na makosa yakiwemo humohumo. Sisi wengine tukigundua tumekosea tensi tu, tunasita na kuanza kupoteana.
 
Watanzania tunajikua sema hatuna komfidensi. Kiingereza cha graduate akikiongea KWA ujasiri ni Bora kuliko hata cha hao wajapani na Wadenmaki.

Ukisikiliza usahili wa wachina, wajapani, wahindi, na watu ambayo kiingereza SIO lugha yao mama, wanaongea Brocken nyingi sana ila hawasiti Wala hawajishtukii Wala hawajali alafu wanaongea KWA kuririka na makosa yakiwemo humohumo. Sisi wengine tukigundua tumekosea tension tu, tunasita na kuanza kupoteana.
Upo sahihi sema ni kuloose confidence tu
 
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri kuna story yako moja ulishawah ileta humu na ukaji specify wewe kama engineer, sasa kaka miaka mitano (5) ya kukaa chuoni ushindwe kujua kingereza cha mawasiliano tu mkuu?
Au zilikua kamba zile????
 
Back
Top Bottom