Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Imeandikwa kwenye Biblia, kitabu cha Mithali 14:34 "Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.
Kwa huu mwendelezo unaoendelea kutolewa mahakamani Katika kesi ya ugaidi ya akina Mbowe, hakika ni aibu kubwa Sana kwa Taifa letu kuwa na Jeshi la Polisi, ambalo halitaki hata kufuata kanuni zao zinazojulikana kwa lugha ya kigeni kama "PGO" na badala yake linajifanyia mambo kivyake, kwa ajili tu ya kuwakomoa wapinzani na kuhakikisha wanaendelea kuwabakisha nyinyi CCM madarakani.
Rais Samia utambue kuwa hii kesi ya akina Mbowe, inafuatiliwa kwa karibu Sana na Jumuiya ya kimataifa na ndiyo sababu mabalozi mbalimbali wa nchi za magharibi wanahudhuria mfululizo kesi hiyo.
Hata hivyo ni majuzi tu umerudi kutoka kwenye mkutano mkubwa wa UN, ambako uliitangazia Dunia kuwa nchi yetu ina "vibrant democracy" na inazingatia kwa hali ya juu haki za binadamu.
Hivi haki gani za kibinadamu zinazofuatwa kwenye nchi yetu kama Polisi wenyewe hawataki hata kuzifuata kanuni zao wenyewe zilizopo kwenye "msahafu" wao wa PGO??
Kama Polisi wetu wanaweza kuthubutu kutaja kwenye ushahidi kuwa watuhumiwa walikutwa na madawa ya kulevya, wakati kwenye "charge sheet" hakuna tuhuma hiyo, hivi unadhani kweli Jeshi letu la Polisi linafanya kazi yake kwa weledi??
Hao Polisi wanaweza kutueleza alipo mtuhumiwa Moses Lijenje kama siyo wamemtanguliza ahera??
Wajibu wa kwanza wa Jeshi la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia na mali zao, sasa inapotokea Jeshi hilo ndilo linaongoza kuwapoteza wananchi wake, maana yake limeshindwa kutekeleza wajibu wao
Kama hutaweza kumstaafisha IGP Sirro kutokana na aibu kubwa aliyoiletea Taifa, Katika kesi hii ya uonevu wa hali ya juu, ya akina Mbowe, basi tutaamini kuwa Jeshi la Polisi, ni "kitengo" ambacho kipo mahsusi na kinalindwa na Dola hii ya CCM kwa lengo la kuendelea kuwabambikizia kesi za uongo wapinzani wa nchi hii, ili CCM iendelee kutawala milele!