SoC03 Vyuo vya ufundi na VETA ndio mkombozi wa vijana Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

busy boy des

New Member
Nov 6, 2014
1
2
UTANGUZILI.
Tanzania tumekuwa na mabadiliko mengi sana katika mfumo wetu wa elimu rasmi toka tumepata uhuru mpaka sasa. Tumekuwa katika kipindi ambacho vyuo vya ufundi vilipewa kipaumbele na kuonekana na thamani sana kwa vijana na sasa tuko katika kipindi ambacho vyuo vikuu vimekuwa bora na kukimbiliwa sana na vijana. Je, ni bora upate elimu ya nadharia bila ujuzi au uwe na ujuzi na nadharia ?

MFUMO WA ELIMU YA ZAMANI.
Mfumo wa zamani wa elimu uliwawezesha vijana kuweza kujitegemea na kuweza kufanya mambo yao au shughuli zao bila kutegemea ajira. Wahitimu waliweza kujishughulisha na shughuli za kilimo, ufugaji, ujenzi, uhunzi na shughuli nyingine mbalimbali. Hii ilitokana na kuwa na vyuo vingi vya ufundi kama vile vyuo vya ufundi kushona, useremali, vyuo vya maendeleo ya jamii na vyuo vya ufundi stadi yaani VETA. Elimu hii ilimfunza mwanafunzi kujitegemea na kuweza kufanya mambo kwa vitendo.

MFUMO WA ELIMU YA SASA.
Baada ya maendeleo ya sayansi na tekinolojia pamoja na utandawazi kumekuwa na msisitizo mkubwa wa elimu ya nadharia kuliko elimu ya vitendo. Vyuo vikuu vimeongezeka ambapo sehemu kubwa ya elimu ya vyuo vikuu ni nadharia kitu ambacho hupelekea mwanafunzi kushindwa Kwenda kujitegemea huko mbeleni na kubaki kutegemea ajiriwa.
Kumekuwa na kasumba moja kwamba degree ni bora zaidi kuliko elimu ya ufundi. Hiki kitu sio kweli kabisa. Wanaomaliza vyuo degree huwa na wakati mgumu sana wa kuhimili maisha mtaani kuliko wale waliosoma vyuo vya ufundi. Mfano mdogo, kijana aliyesoma uinjinia wa umeme chou kikuu cha Dar es Salaam na yule aliyesoma VETA hawa wawili wakichukuliwa waingie katika kutafuta maisha kwa kujiajiri, huyu wa VETA atafanya vizuri zaidi kuliko huyu wa degree.

USHAURI WANGU KWA WIZARA YA ELIMU NA SEKTA BINAFSI ZA ELIMU.

Wizara ya elimu ikishirikiana na sekta binafsi ijikite katika kuendeleza na kuviboresha vyuo vya ufundi, vyuo vya maendeleo ya jamii na Vyuo vya ufundi stadi ili kuondoa ombwe la ujuzi kwa vijana. Hii ni kwa sababu Elimu kwenye vyuo hivi ina mambo haya yafuatayo;
  • Hufundisha vijana kupata ujuzi wa kazi na sio nadharia. Vyuo vya ufundi vinafundisha ujuzi wa kazi ambao ni muhimu sana katika soko la ajira. Vijana wanaohitimu kutoka vyuo vya ufundi na VETA wanakuwa na ujuzi wa kazi ambao ni muhimu sana kwa waajiri, na hivyo wana nafasi kubwa ya kupata ajira na kujiajiri kuliko wale ambao hawana ujuzi wa kazi.
  • Gharama zake ni nafuu sana ukilinganisha na vyuo vikuu. Hii itapelekea vijana wengi wasio na Uwezo wa kumudu gharama za vyuo vikuu kujiunga na vyuo hivi vya ufundi.
  • Vyuo vya ufundi humpa Uwezo mkubwa wa kijana kujiajiri na kuwa na shughuli zake ambazo baadae ataweza kuwaajiri vijana wenzake katika shughuli hizo.
 
Back
Top Bottom