Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,161
- 1,493
Ili kuweza kufikia kupanda na kukuza miti angalau bilioni 50 baada ya miaka kumi kutoka sasa, ambapo hali ya ukame inaweza kuwa ni mbaya zaidi kuwahi kutokea ni muda sahihi Serikali ikaazisha Wizara Maalum itakayoshughulikia Upandaji na ukuzaji Miti kufikia miti mipya bilioni 50, Wizara hii iwe chini ya Ofisi ya Rais.
Natambua kuna Wizara ya Muungano na Mazingira, ambapo Mh. Jafo anfanya vizuri, yawezekana kwa muundo ulivyo kea sasa si rahisi Wizara hii kupitia Taasisi zilizo chini yake kupanda na kukuza miti bilioni 50 baada ya miaka kumi ijayo.
Natambua kuna Wizara na ya Mali Asili, ambapo pia Mh. Pindi anafanya vizuri, lakini kupitia Taasisi zake kama TFS na majukumu mengine waliyonayo na wanatakiwa kukusanya maduhuli haiwezekani kusimamia kupanda na kukuza miti bilioni 50 bila kukata.
Pia Kuna Wizara ya OR-TAMISEMI, Kupitia Halmashauri wamekuwa na kampeni ya kupanda miti, sina hakika kati ya miti inayopandwa ni mingapi inasimamiwa katika namna ya kuhakikisha kuwa miti yote iliyopandwa haifi ukizingatia Halmashauri bado ina vipaumbele vingine kama kusimamia miradi ya Maendeleo na kukusanya mapato kwa ajili ya kuhudumia Wananchi.
Janga la ukame ni bomu linalokuja kulipuka, madiliko ya hali ya hewa na athari zake ni tatizo la Dunia, lakini kama nchi tunapaswa kuchukua hatua za makusudi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunapanda miti ya kutosha, turudishe misitu minene kila sehemu.
Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, umekuwa unasisitiza kupambana na ukame, Mh. Rais kwa unyenyekevu na ikikupendeza kama ujumbe huu utakufikia naomba tuwe na Wizara Maalum ya kushugulikia Upandaji na ukuzaji miti tu, Wizara ambayo itategemea Ruzuku ya Serikali ili isijihusishe na ukusanyaji wa mapato katika miti hiyo itakayoipanda, Wizara amabayo Waziri na Wataalam wake watakuwa site kupanda miti ili tuwe na misitu mikubwa tena iliyokuwepo huko nyuma.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan