Kutokana na ahadi yake: Haji Manara kesho rasmi anahamia Yanga kuitumikia

Mara baada ya Liverpool kupangwa na Barcelona kwenye hatua ya nusu fainali Afisa habari wa Simba Haji Manara akatamka kwa mdomo wake na bila kulazimishwa kuwa endapo Liverpool wataitoa Barcelona kwenye hatua hiyo na kuingia fainali atahamia Yanga pamoja na kuwa mstari wa mbele kuchangisha fedha kwa ajili ya Yanga.
Sasa Barcelona wametolewa rasmi na Liverpool na kuingia fainali,Je Manara atakamilisha ahadi aliyotoa mbele ya hadhara??
Tusubiri...
Manara ni shabiki wa man united kwahyo liverpool alipopangwa na barca alidhan lazma liver atolewe kama man u
 
Kamwene Mtani.

Huyo ndo kashakuwa wenu, mpokeeni.

Kasema anachangia na hela kabisa, nadhani ni zile za faida kwenye perfume.
Akaaaaaa. Abakie tu huko Mtani sababu nyie ndio mmezowea kupewa kauli tamu za uwongo ambazo huwa zinawafariji wenyewe.

Kama ile eti Simba saizi yake ni Barca. 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom