Mwana Mapinduzi John Okello

munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
392
703
John Okello ambaye aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa mwaka 1937 huko Uganda katika kabila la Langi ambalo pia ni la Rais wa Zamani wa Uganda Milton Obotte. Alizaliwa akiitwa John Gideon Etuku. Wazazi wake walifariki Akiwa bado mdogo na kulazimika kwenda kulelewa na mjomba wake pamoja na wadogo zake wawili lakini kutokana na utukutu wake hakuweza kuishi kwa mjomba sababu alikuwa akipigwa na akakimbia kwenda kuanza vibarua huko Soroti katika Gineri ya kuchambua pamba. Inasemekana alitaka kwenda kujiunga na jeshi lakini hakufanikiwa kutokana na umri mdogo.

Katika harakati za kutafuta maisha alifika hadi Nairobi nchini Kenya na kuendelea hadi Mombasa ambapo alikuwa ukifanya kazi za vibarua. Alichukia kiuitwa boy , mtumishi, au mtumwa . Mwaka 1955 aliwekwa gerezani huko na akiwa humo alikutana na wapiganaji wa maumau waliokuwa wakipinga Ukoloni nchini Kenya kutoka kwao alipata hamasa ya Kupambana na ukoloni na ukandamizaji.

Mwaka 1959 akiwa na rafiki yake Mluo walienda Pemba katika eneo la Vitongoji na akawa anafanya kazi ya kugonga na kuuza mawe. Huko alipendwa na kuwa na ushawishi na ndipo alipoanza kuonesha nia yake ya kuuondoa utawala wa Sultan. Wakati anaondoka Pemba alipatia chama cha ASP nyumba yake ili waifanye ofisi ya chama.

Mwaka 1963 alihamia Unguja na kuanza kufanya kazi za kupaka rangi nyumba pamoja na kufanya kazi katika kiwanda cha kuoka mikate na akaendelea na vuguvugu la kisiasa.

Kumekuwa na Tetesi kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi na askari polisi na askari wa Mau mau lakini pia kuwa aliwahi kupigana wakati wa vita vya pili vya Dunia, dhana zote hizo si za kweli. Ukweli ni kuwa Okello hakuwahi kuwa mwanajeshi au kupata mafunzo ya kijeshi. Majigambo yake kuwa alikuwa na uzoefu wa kijeshi yalikuwa ni mbinu tu ya kumsaidia kuongoza mapinduzi

Alifanikiwa kuanzisha chama cha Mafundi rangi wa Unguja na Pemba na kupitia chama hicho aliweza kupenyeza ushawishi wake wa kufanya mabadiliko ya kumuondoa Sultan

Baada ya kufanikisha Mapinduzi aalimkaribisha Karume kuongoza serikali. Tatizo la Okello hakuwa na back up ya kisiasa na hakuweza kuaminika. Akatupwa na kufukuzwa bila shukrani. Mwanzoni alipelekwa Kenya lakini akafanya jitihada za kutaka kurudi nchini akakamatwa Mwanza na kufungwa. Lakini baadae akarudi Uganda.

Wakati Idd Amini alipompindua Obotte mwaka 1972 alikwenda kumpongeza. Lakini baadae akawa na Mawasiliano na kundi la Obotte lililokuwa Tanzania, katika harakati za kutaka kujiunga na kundi hilo alikamatwa na kuuwawa na Idd Amin.

Kwa hiyo tunaona kuwa Okello alikuwa Mwanamapinduzi. Kuongoza na kushiriki Mapinduzi ya Zanzibar haikuwa kwa ajili ya Mshahara, bali ilitokana na nia yake ya dhati ya kupinga ukoloni na ukandamizaji.

Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
 
Inasikitisha
Alipoenda kenya kenyatta hakumuamini,alipoenda kongo huko hakuaminiwa,kwenda Uganda idd amin akaona huyu atamtengenezea
MapinduZi ...akammaliza

Na angebaki tanganyika,ameonekana
Huyu atakuja kuwa mwiba

Mission zingine siyo kabisa

Ova
 
Hvyo ndvyo wanamapinduzi huwa

Sikuzote wanamapinduzi hawapendwi na wapenda kitonga

Karume hajaipambania Zanzibar Kama nyerere pia waliopambana kuhusu Uhuru wengi walitupwa nje ya mfumo au walipewa tuvyeo tusitokuwa na impact kwenye siasa za nchi

Waulize wazee wa mzizima wanalijua hilo
 
Laana za Allah ziwe juu yake hadi siku ya hukumu. Hapo walipofika Wazanzibari juu ya kila hali yao basi sababu ni yeye na genge lake lote. Wazanzibari walipata uhuru wao Disemba 10 mwaka 63. Mtu kutoka Uganda yanamhusu nini Mapinduzi na harakati za Zanzibar!! Tafakari
 
Msikilize Field Marshal John Okelo akiongea siku chache baada ya mapinduzi.

Yuko na Karume .

Ukristo ndio ilimgharimu Okelo, hakupendwa na Wazanzibari pamoja na kwamba walishindwa kuondoa utawala wa kisultani kwa miaka yote, yeye akaweza hilo akiwa na miaka 29 tu.

Karume alikua Tanganyika aliporudi Okelo akampatia nchi baadae Karume akampeuka na kumfukuza Zanzibari.
 
munkango
Mwandishi mmoja mzungu alisema kwamba Okello lazima atakuwa alipitia mafunzo ya uaskari kutokana na vile alivyovaa uniform sawasawa (hasa kofia na soksi). Isingewezekana kwa mlalahoi kuweza kuvaa kwa discipline bila ya kupitia mafunzo. Pia jinsi alivyokamata bunduki alikuwa na uelewa nayo na yeye ndiye aliyekuwa akifundisha wengine jinsi ya kuitumia mpaka ikafikia wengine kujipiga risasi wenyewe.

La pili wewe unaamini zile stori za Okello kuwa alikuwa ameoteshwa kuja kuikomboa Zanzibar na zile namba zake za ushetani at 99999...? Uongo mtupu.
 
Msikilize Field Marshal John Okelo akiongea siku chache baada ya mapinduz...

Hakuna cha ukristo wala nini, shughuli za kugombea uhuru wa Zanzibar zilikuwa tayari zimepamba moto na tayari kulikuwa na vyama vya siasa kama ilivyokuwa Tanganyika na nchi nyingine katika kipindi kile.

Uhuru ungepatikana tu bila Okello na pengine bila hata ya kumwaga damu ambayo imeleta uhasama mkubwa katika jamii. Mbona nchi kama Tanganyika, Nigeria, Ghana (aliyekuwa anaongoza shughuli za kugombea uhuru), Uganda na Kenya zimepata uhuru ingekuwaje ibaki Zanzibar tu?

NB: Ugomvi wa Kenya (Mau Mau) ulikuwa wa kugombea ardhi hapo mwanzo lakini baadae ndiyo ukafikia mpaka uhuru.
 
Hvyo ndvyo wanamapinduzi huwa

Sikuzote wanamapinduzi hawapendwi na wapenda kitonga

Karume hajaipambania Zanzibar Kama nyerere pia waliopambana kuhusu Uhuru wengi walitupwa nje ya mfumo au walipewa tuvyeo tusitokuwa na impact kwenye siasa za nchi

Waulize wazee wa mzizima wanalijua hilo

Ndio mana yule mzee side boy kila siku kulia lia,baada ya kuona wazee wake walikosa kukaa pale jumba jeupe.
 
Laana za Allah ziwe juu yake hadi siku ya hukumu. Hapo walipofika Wazanzibari juu ya kila hali yao basi sababu ni yeye na genge lake lote. Wazanzibari walipata uhuru wao Disemba 10 mwaka 63. Mtu kutoka Uganda yanamhusu nini Mapinduzi na harakati za Zanzibar!! Tafakari

Bila yeye vibaraka wa waarabu wangeendelea kuwaminya kende.
 
IMG_0148.jpg
 
Msikilize Field Marshal John Okelo akiongea siku chache baada ya mapinduzi.

Yuko na Karume .

Ukristo ndio ilimgharimu Okelo, hakupendwa na Wazanzibari pamoja na kwamba walishindwa kuondoa utawala wa kisultani kwa miaka yote, yeye akaweza hilo akiwa na miaka 29 tu.

Karume alikua Tanganyika aliporudi Okelo akampatia nchi baadae Karume akampeuka na kumfukuza Zanzibari.

kwenye video iyo Okelo anaonekana kabisa ni askari mpambanaji yupo active.uyo kapitia mafunzo ya uaskari sio bure.
 
Hakuna cha ukristo wala nini, shughuli za kugombea uhuru wa Zanzibar zilikuwa tayari zimepamba moto na tayari kulikuwa na vyama vya siasa kama ilivyokuwa Tanganyika na nchi nyingine katika kipindi kile.

Uhuru ungepatikana tu bila Okello na pengine bila hata ya kumwaga damu ambayo imeleta uhasama mkubwa katika jamii. Mbona nchi kama Tanganyika, Nigeria, Ghana (aliyekuwa anaongoza shughuli za kugombea uhuru), Uganda na Kenya zimepata uhuru ingekuwaje ibaki Zanzibar tu?

NB: Ugomvi wa Kenya (Mau Mau) ulikuwa wa kugombea ardhi hapo mwanzo lakini baadae ndiyo ukafikia mpaka uhuru.
Unaposema hivyo inamaana mapinduzi Zanzibar yalifanyika wakati wa mkoloni ambaye ni Mwingereza?

Ninavyojua mimi ni kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yamefanywa wakati Zanzibar ikiwa huru.
 
Unaposema hivyo inamaana mapinduzi Zanzibar yalifanyika wakati wa mkoloni ambaye ni Mwingereza?

Ninavyojua mimi ni kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yamefanywa wakati Zanzibar ikiwa huru.
uhuru umepatikana december 10, 1963 na mapinduzi ndiyo january 11 usiku. Muingereza alijidai ametoa uhuru kutoka kwake kwenda kwa Sultani wakati yeye ndiye aliyemuweka Sultani madarakani kwa hivyo jamii haikuweza kuona tafauti kabla na baada ya uhuru (hata hivyo ilikuwa ni kwa muda mfupi sana)

Shughuli au mchakato wa kugombea uhuru ndiyo ulianza miaka kadhaa kabla. Baada ya kutoridhika kwa uhuru uliopatikana ndiyo yakafanyika mapinduzi.

Kwa mujibu wa maandishi tafauti hata hiyo mipango ya mapinduzi ilikuweko chini chini, kuna team mpaka ilikwenda Cuba kusomea guerilla warfare (akina Amour Dugheshi, Ali Mahfoudh, Hashil....), pia team iliyotoka bara (soma kitabu cha Ghassany).
 
Back
Top Bottom