Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Kabla sijaliongelea hili na-declare interest kuwa mimi ni MKE (WIFE).Wives uleta shida katika familia zetu na ukiwasikiliza sana unapotea
P square naona tatizo lao kubwa ni huyo mwenye mke aliye owa juzi juzi
Kuna ambao watadhani kuwa huu ni utetezi kwa sababu (huenda) nami nikakumbwa na hiki kimbunga siku moja.
Kutoka ndani ya moyo wangu nachukia sana sentensi kama hizi. Mara nyingi familia zinapoingia kwenye migogoro basi mtu wa kwanza kutupiwa lawama huwa ni mke wa mmoja au zaidi walioingia katika familia hiyo. Na mbaya zaidi mama katika familia hiyo anaweza kuwa mstari wa mbele kushikilia hilo, anasahau kabisa kuwa naye alikuwa mke kwenye hiyo familia. Huwa inasikitisha sana na sijui kwa nini watu wanawaza hivyo.
Napenda niwaeleze ndugu wa waume zetu kuwa sisi (wake) tunatambua umuhimu wa familia za waume zetu kuwa na umoja. Msifikirie kuwa kila kibaya ambacho mume anachokifanya kwa familia basi shinikizo linatoka kwa mkewe. Kuna wake ambao ni Blessings katika familia za waume zao, tusiendelee kuwakwaza kwa maneno kama haya.
Nawatakia uvumilivu wake wenzangu pindi tunaposikia maneno kama haya. Mungu anaona nia zetu NJEMA.
Mubarikiwe sana