Kutoka Kibanda Maiti - Zanzibar

Kutoka Kibanda Maiti - Zanzibar

Uzanzibari kwanza, Utanzania baadae.

Let Tanganyika come to free Znz
.
 
Wapewe uhuru wao bwana, kwani tatizo nini
Sina uhakika kama neno uhuru hapa linatumika sawasawa. Zanzibar haikuwahi kutawaliwa na nchi nyingine yoyote, zaidi sana imekuwa ikineemeka na resources za bara kuliko ambavyo bara imefaidika na resources za Zanzibar.
 
Mm sioni sababu ya kuwanyima uhuru wao coz muungano ni makubaliano ya nchi mbili kama upande mmoja hawataki, basi uvunjwe kama kutakuwa na umuhimu watauungana tena kipindi kingine kwa misingi ambayo kila upande utarithia.

hapo umeongea mkuu.mfano nzur refer to old east africa community and the newly one
 
Well said Edson, yaani kuna mambo mengi sana yanayonifanya always niuchukie huu muungano. Na ninashangaa sana pale ninapoona eti Wazanzibar wanasimama na kutaka eti wapewe uhuru, halafu sisi ndiyo tunajifanya tunasita kuwaachia waende, na huku sisi daima tunaumizwa na huo muungano. Sioni logic na sitakaa nione hiyo logic ya wabara kuendelea kuung'ang'ania muungano kwa namna yoyote ile.
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii ingekua na uongozi thabiti wote waliokua hapo kibanda-maiti muda huu wangekua lockup akiwepo maalim seif sharif hamad aka mliberal.
 
Hiyo nchi wanayoitaka ni ipi? Nadhani huyu raisi wetu ni mkimya sana.. Au ni dhaifu...
Ebu chukueni hatua za kutosha
 
Si mpaka aliyetuambia tuungane arhusu tuwaachie?
Ninyi mnadhani tuliungana hivi hivi tu?
Kuna mkono wa mtu mkubwa hapo.
Yakheeee umesha wahi mla kifurukombe weye??? Ooh mtamu huyo!!!!
 
Mkutano mkubwa uliovuta hisia za wananchi wengi wa Visiwa vya Unguja na Pemba umefanyika leo hapa Unguja eneo la Kibanda Maiti. Mkutano huo uliokuwa ukitangazwa na vituo kadhaa vya radio hapa Visiwani imehudhuriwa na viongozi na watu maarufu hapa Zanzibar, huku Maalim Seif akiwa mzungumzaji mkubwa katika mkutano huo. Agenda ikiwa ni Muungano na Mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar.
Miongoni mwa mambo yalizungumzwa ni
1. Zanzibar kuwa na Serikali huru na yenye mamlaka kamili
2. Kuwa na Baraza lake la Mitihani - kwa madai kuwa NECTA inawafelisha Wazanzibar
3. Mamlaka ya huru ya Mapato na TRA kutokuwa na mamlaka ndani ya Zanzibar
4.Zanzibar kuwa na fedha yake - na sio kutumia shilingi ya Tanzania
5.Tume ya Uchaguzi yaani NEC na msajili wa Vyama kwa Zanzibar pekee
6. Zanzibar kuachiwa rasilimali zake
7. Wizara ya Mambo ya Ndani yake na wala sio ya MUungano
6.Wizara ya Fedha
7. Kushughulikia mambo yake ya kimataifa yenyewe
8. Kuwa na sera ya dini kwa sababu Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
9.Kuwa na Bunge lake lenye mamlaka kamili
10. Kuwa na katiba yake ambayo haingiliani na katiba ya JMT

Madai mengi yametoa mwanga kwamba Wazanzibari wanaonewa na kunyanyaswa kwa sababu ya ujanja wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Kwa hapa Zanzibar, mazungumzo katika vijiwe vyote maarufu kama Jaws Corner, Malindi na Mkunazini ni habari ya Zanzibar Huru.............

nawasapoti wazenji! Kazi imeanza. Uzuri Rama Ighondu hayuko huko mngeng'olewa kucha na meno bila ganzi
 
Na wasisahau tu kuwa tutawakatia Umeme wetu within 24 Hours
 
huyu maalimu seif si yuko serikalini tena mtu wa pili KUTOKA raisi Kwa nini asilipeleke hili kwenye baraza la mawaziri wakalijadiri?
 
Moja: Mimi Mtanganyika, siruhusiwi kisheria kumiliki ardhi ndani ya Zanzibar! Wao wanaruhusiwa kuja huku kwetu kumiliki ardhi, Muungano kwa hilo haunisaidii, unanidhulumu.

................. Situtaki Muungano. kama wanalilia Zanzibar huru wapewe lakini wajue tunawabeba sana....

Mkuu Edson kama Watanganyika (sijui Wabara) wengi wangeweza kuangalia huu muungano kwa jicho lako nafikiri kusingekuwa na Muungano sasa hivi as ungekuwa umeshavunjwa!

Watu wengi wa huku Tanganyika ukiwauliza Muungano unawasaidia nini wala hawawezi kukujibu - maana faida zake hawazioni. Lakini siku za Muungano zinakaribia mwishoni. Utavunjika tu wala siku si nyingi! watu wengi wanatamani uvunjike hata leo.

Hakuna kitu kinachowakera na kuwaudhi Watanganyika kama kusikia eti Muungano wa Mkataba!.

Hao wazanzibari wanaotaka muungano wa mkataba wajue kabisa kuwa hautakuwepo! - (Hatuhuitaji na wala hatuna shida nao) - HATUUTAKI huo muungano wa Mkataba, nyie vunjeni huu na ndio mwisho wa habari.

Na hao wanaoshangilia sijui mkataba sijui nini wajue kuwa once huu muungano wa kuzushi tuliokuwa nao ukivunjika tu basi mambo yanabadilika, hali haitakuwa sawa kama zamani as kwenye movement za watu na ufanyaji wa biashara.

Kama Mke hataki ndoa anataka Talaka, baada ya kupeana Talaka anataka (MKATABA) tusaini makubaliano ya mimi kuendelea kukaa, kuwalisha, kuwasomesha ndugu & wadogo zake?! - Haiwezekani.

Vunjeni huu Muungano -
Tutakutana Jumuiya ya East Africa kama Burundi & Rwanda tunavyokutana nao.
.
 
huyu maalimu seif si yuko serikalini tena mtu wa pili KUTOKA raisi Kwa nini asilipeleke hili kwenye baraza la mawaziri wakalijadiri?
ceremonial leader hana maamuz hayo labda ingekuwa kuzindua kisima
 
Back
Top Bottom