Kutoka Kibanda Maiti - Zanzibar

Kutoka Kibanda Maiti - Zanzibar

Hatutaki unyonyaji wa wazanzibar kuendelea wapate uhuru wao huu ukoloni wa kutawalana weusi kwa weusi baada ya ule wazungu haukubaliki.
 
Mkutano mkubwa uliovuta hisia za wananchi wengi wa Visiwa vya Unguja na Pemba umefanyika leo hapa Unguja eneo la Kibanda Maiti. Mkutano huo uliokuwa ukitangazwa na vituo kadhaa vya radio hapa Visiwani imehudhuriwa na viongozi na watu maarufu hapa Zanzibar, huku Maalim Seif akiwa mzungumzaji mkubwa katika mkutano huo. Agenda ikiwa ni Muungano na Mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar.
Miongoni mwa mambo yalizungumzwa ni
1. Zanzibar kuwa na Serikali huru na yenye mamlaka kamili
2. Kuwa na Baraza lake la Mitihani - kwa madai kuwa NECTA inawafelisha Wazanzibar
3. Mamlaka ya huru ya Mapato na TRA kutokuwa na mamlaka ndani ya Zanzibar
4.Zanzibar kuwa na fedha yake - na sio kutumia shilingi ya Tanzania
5.Tume ya Uchaguzi yaani NEC na msajili wa Vyama kwa Zanzibar pekee
6. Zanzibar kuachiwa rasilimali zake
7. Wizara ya Mambo ya Ndani yake na wala sio ya MUungano
6.Wizara ya Fedha
7. Kushughulikia mambo yake ya kimataifa yenyewe
8. Kuwa na sera ya dini kwa sababu Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
9.Kuwa na Bunge lake lenye mamlaka kamili
10. Kuwa na katiba yake ambayo haingiliani na katiba ya JMT

Madai mengi yametoa mwanga kwamba Wazanzibari wanaonewa na kunyanyaswa kwa sababu ya ujanja wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Kwa hapa Zanzibar, mazungumzo katika vijiwe vyote maarufu kama Jaws Corner, Malindi na Mkunazini ni habari ya Zanzibar Huru.............
 
Wewe ata huhesabiwi huna mbele wala nyuma, Uzalendo wako wote umekushinda kudai mamlaka ya nchi yako ya Tanganyika, Wewe ni kama MTUMWA wa Enzi hizo za Kima na Nyani huna tofauti yeyote., umesaliti nchi yako Tanganyika kuidaia uhuru wake kama wanavyodai wazanzibar.,,
 
Na kwa kumalizia Maalim Seif amewaambia Wazanzibar kutokubali katiba mpya kama haya mambo hayataainishwa kwenye katiba hiyo!
 
Si aseme tu hataki muungano. Sasa huu siiyo uchochezi? Kutangaza Zanzibar ni nchi huru siyo uhaini? Jk Vipi?
 
Kila heri wazanzibar. Lakini muitishe hiyo referendum kama mwanakijiji alivyoshauri badala kuongea majukwaani bila vitendo.
Sidhani kama hii ndoa ilikuwa mpaka kifo kitutenganishe.
 
Seif ni mhaini na amevunja katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea. Anapaswa kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakani bila kusita. Wachochezi hawa ndio wanaoleta shida na matatizo nchini mwetu. Huu ni ukabila ni udini na ni kutugawa watz.
 
Nahisi Maalimu bado anandoto za kuirejesha zanzibar huko Omani tusubili tuone hatma yake.

-Ni dhahili wala hakuna mashaka mara baada ya zanzibar kupata mamlaka kamili,

1. Pemba itahitaji mamlaka kamili

2. Unguja itahitaji mamlaka kamili

Kisiwa nduwi, chakechake nk navyo vitahitaji mamlaka kamili, Hatima ya haya yote Tanganyika itaibuka shujaa siku

moja hapo baadaye na wataikumba lakini kama ilivyo kawaida ya historia majuto atakuwa mjukuu.
 
Na kwa kumalizia Maalim Seif amewaambia Wazanzibar kutokubali katiba mpya kama haya mambo hayataainishwa kwenye katiba hiyo!

Mmemuuliza kuwa yeye mbona juzi juzi kakabidhiwa kitambulisho cha Utanzania?
Je, amewambia ni raslimali zipi ambazo anataka zanzibar iachiwe?
 
Mmemuuliza kuwa yeye mbona juzi juzi kakabidhiwa kitambulisho cha Utanzania?
Je, amewambia ni raslimali zipi ambazo anataka zanzibar iachiwe?

kwani watanganyika wanafaidika na nini kwenye huu Muungano, inaonekana kama hawataki kuiachia zanzibar, kunanai!
 
Seif ni mhaini na amevunja katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea. Anapaswa kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakani bila kusita. Wachochezi hawa ndio wanaoleta shida na matatizo nchini mwetu. Huu ni ukabila ni udini na ni kutugawa watz.

nani wa kulifanya hilo, sio kila dai ni uchochez jipange tena
 
kwani watanganyika wanafaidika na nini kwenye huu Muungano, inaonekana kama hawataki kuiachia zanzibar, kunanai!

Hakuna faida zaidi ya hasara..ila seif akishageuza kuwa hospital y awazi ya vichaa tutapata hasara zaidi ya hii ya kuwalisha bure.
 
me nawashauri wazanzibar waende kwenye tv au radio watangaze kuwa kuanzia leo zanzibar si sehemu ya tanzania, kwisha kazi alafu tuone serikali ya bara itafanya nini.
 
Back
Top Bottom