Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,884
2,000
Wanabodi,

Kwa wale wenye nafasi, ifika saa 4:15 asubuhi hii, tujiunge na TBC kuangalia matangazo ya moja kwa moja ya live mubashara kutokea ikulu ya Chato.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Tweet ya Gerson Msigwa.

Pia leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa habari, huku Tanzania tukiwa kwenye hii vita ya kimataifa ya kupambana na janga la Corona, serikali ya Tanzania ikishutumiwa kuficha idadi ya kweli ya vifo vya Corona, hivyo tufuatilie kwa makini tukimsikiliza rais Magufuli atazungumza nini.
P

==========

041014FB-364A-4AB1-8471-56A5D4722BC5.jpeg


BAADHI YA NUKUU:

Rais Magufuli: Miaka ya nyuma ulikuwa ukienda kutembela sehemu ukaambiwa kuna Surua unaogopa. Leo ugonjwa huo umeonekana wa kawaida na hofu imeondoka. Ni hivyo kwa magonjwa mengi ambayo tumekuwa tukiyaona kama nchi kama TB na Ukoma. Hofu hiyo imeondoka hata kwa Ebola


Rais Magufuli: Niwaombe watanzania hili tatizo (#COVID19) litaondoka na tuendelee kuchukua tahadhari zinazotakiwa tusihusishe na uchumi wa nchi yetu.

Nchini waajiriwa zaidi ya 49% ni walimu ila tumelipa mishahara shule zikiwa zimefungwa na tutaendelea kulipa.

Rais Magufuli: Waziri Mwigulu nimekuapisha leo, itabidi mkafanye uchunguzi kwenye masuala fulani ktk maabara ya Kitaifa inayohusika kupima #Corona

Nimeona walikuwa wanatoa tu matokeo watu wameathirika tu. Nilitoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakaangalie.

Rais Magufuli: Namshukuru Katibu Mkuu mpya, wameenda na kufanya yafuatayo; Tulichukua sampuli ya Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari na kupeleka maabara bila wao kujua

Sampuli ya oil kwa mfano tuliipa jina la Jabri Hamza mwenye miaka 30, ile ilileta “negative”

Rais Magufuli: Sampuli ya Fenesi iliyopewa jina la Sara Samweli matokeo yake yalikuwa 'inconclusive'

Sampuli ya Papai tukaipa jina ya Elizabeth Anne, majibu yakawa Positive kwamba lina Corona kwamba maji ya ndani ya papai yana #COVID19

Rais Magufuli: Sampuli ya ndege Kware imekuwa ‘positive’, ya Sungura ikawa ‘indeterminate', ya Mbuzi ikawa ‘positive’, ya Kondoo ikawa ‘negative’

Sasa ukiona ya binadamu ikawa positive maana yake na mapapai yote yaweke isolation au mbuzi na fenesi wote wawe isolated.

Rais Magufuli: Ukigundua kitu hiki lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika katika maabara hii na katika nchi hii.

Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, au hawana utaalamu; kitu ambacho si kweli au vifaa maana hadi vipamba vinatoka nje.

Rais Magufuli: Kama hadi mapapai yana #CoronaVirus basi WHO inatakiwa ifanye kazi kubwa ktk haya, na kama hadi Mbuzi wana Corona basi wanasayansi hawajafanya kazi ya kutosha

Kutokana na hizi taarifa lazima kuna watu wameambiwa ‘positive’ wakati si wagonjwa wa #COVID19

Rais Magufuli: Kuna wengine si ajabu wakafa kwa hofu. Papai halijafa lipo tu linaiva, Mbuzi yule yupo tu wala hajafa hata fenesi lipo

Natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu. Wale ambao hawajachoka wala kuumia kwanini uwe na hofu? Mafua yamekuwepo ila haya ni advanced.

Rais Magufuli: Kitendo cha kukuta hata papai lina #COVID19 mule ndani wala sio juu, kwasababu ingekuwa juu wangesema labda aliyegusa ana #CoronaVirus. Wametoa specification vizuri kabisa, walichoma ndani wanachukua sampuli. Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Rais Magufuli: Kuna vitu vingi vya kujiuliza, huenda kuna kitu hakijaeleweka kwa wanasayansi lakini hata dunia hawajakielewa

Natoa wito kwa wanaotumia vifaa hivi hasa Afrika, wachukue sampuli ya kitu chochote hata ukuta, mjusi watakuja kuthibitisha haya.

Rais Magufuli: Tuendelee kuchapa kazi, uzalishaji uendelee maradufu, tusitishane. Wanasiasa waache kuitumia #COVID19 kama agenda, haitasaidia

Mtu anasema funga Dar, funga Tanga, sifungi nilishasema. Ni lazima Watanzania tuchape kazi na kuendelea kuchukua tahadhari.

Magufuli: Inawezekana fenesi, papai lingekuwa linasikia kuwa lina #COVID19 lingekuwa limeshaoza kabisa. Lakini kwa vile halisikii, lina #CoronaVirus na bado lipo

Sasa wewe kama Waziri (Nchemba) mkashirikiane na Wizara ya Afya mkaangalie hiyo Maabara ya Taifa kuna nini?

Rais Magufuli: Mbeleni ninafikiria hata kuruhusu ligi iendelee ili watu wawe wanacheza tukiangalia kwa TV. Tuweke utaratibu mzuri.

Ninaelewa hata walioathirika na #COVID19 sijaona mwanamichezo aliyedhurika sana. Hii ni wazi kuwa wanaofanya michezo #Corona inawakwepa.

Rais Magufuli: Kama tunazuia hata kucheza mpira maana yake tunawaambia wapate #Corona. Najaribu kusubiri wataalamu wanishauri vizuri

Inawezekana tunaishi na huu ugonjwa kama watu wenye UKIMWI, TB, Surua na maisha yakaendelea. Tuache kuogopana na kutishana.

Rais Magufuli: Ninajua wapo wengine wangependa kuzungumza kuhusu #Corona. Naona na vyombo vingine vya habari wao ni corona tu, tena vya nje na huko vinapotangazia ndio imeua watu wengi

Lazima mjiulize kwanini havizungumzii ya kwao wanaongelea ya #Tanzania?

Rais Magufuli: Natoa wito kwa hasa vijana ambao kila siku wakimuona mtu amekufa ni #COVID19

Jaji Mkuu (Augustino Ramadhani) tumehangaika naye hapa kwa mwaka mzima, si vizuri kutaja matatizo yake. Baba yangu kafariki kwa saratani kama Jaji Mkuu ila watu wamebadili maneno ya ajabu.

Rais Magufuli: Si kila anayekufa ni #Corona. Malaria inaua, ajali inaua. Juzi Mkuranga wamekufa watu 21 kwa ajali, roho zao Mungu azipumzishe kwa amani

Siku hizi mtu hata akijifia chumbani kwake wanapoenda kuchukua ile maiti ni Corona. Ninawaomba Watanzania tubadilike.

Rais Magufuli: Nawapongeza madaktari, manesi na watendaji wa Wizara ya Afya kwa kuendelea kuhudumia Watanzania ktk kipindi hiki.

Kuna mengi ya kushangaza nchini. RC wa Mtwara nikamsikia kwenye vyombo vya habari eti "DC huyu hawezi kusafirishwa kwenda kwao", inasikitisha.

Rais Magufuli: Kama madaktari wanaenda kuwaona wagonjwa wakiwa na PPE. Walishindwaje viongozi wa Mkoa wa Mtwara chini ya RC kuifunga maiti PPE na kuipeleka Moshi?

Niwaombe viongozi wenzangu tusichukue hili kwa papara, tuwatumie wataalam kupata ushauri utakaosaidia.

Rais Magufuli: Ninaamini #CoronaVirus ipo ila si kwa 'extent' hiyo. Katika siku 2-3 zilizopita tulikuwa na watu 16 waliofariki kwa #COVID19

Sasa tafuta uwiano wa watu 16 na idadi ya watu karibu mil. 60 na uwiano wa nchi nyingine na idadi yao ya waliokufa halafu utaona.

Rais Magufuli: Tunawatisha Watanzania wanaogopa hata kwenda kufanya kazi au sokoni

Nilisoma kwenye WhatsApp mtu anasema “funga masoko”. Nikajiuliza huyu ana akili za kawaida? Hapo alipo hana shamba wakifunga masoko atapata wapi chakula? Tena yupo Dar, ni “shortsighted”

Rais Magufuli: Ukizuia soko la Kariakoo, watu milioni 6 wa Dar watakula wapi? Wabaya wetu wanataka tuingie kwenye ujinga huo.

Nchi zilizofunga mnaona matokeo yake. Sitaki kuzitaja ila kuna nchi watu wamekufa zaidi ya elfu 50 na zina uwezo wa kila kitu.

Rais Magufuli: Tuchukue tahadhari na kuwapuuza wanaojaribu kututisha, hawana maana. Tuendelee kumuomba Mungu.

Kuna Viongozi wengine wa dini wamemsahau Mungu, wameanza kuyumba na wameanza kuweka ubinadamu mbele. Wanasema tuache kuomba ili tujiokoe. Ni mambo ya ajabu!

Rais Magufuli: Hali si mbaya kama tunavyotishwa, sisi tupo vizuri na biashara zinaendelea ndio maana hata tunaweza kulipa mishahara.

Hata hao wanaosema tufunge huku anaendeshwa na gari limeandikwa STK, mafuta anawekewa na Serikali, amesahau alichokalia ndicho kinamlisha.

Rais Magufuli: Ninawasiliana na Madagascar na wameandika barua wanasema kuna dawa imepatikana. Tutatuma ndege ili ziweze kuletwa nchini.

Serikali tunafanya kazi usiku na mchana. Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa sitakiwi kuwa huku? Huku si ndiko nitazikwa?

Rais Magufuli: Tunatakiwa kusimama pamoja. Nampongeza Mbatia (James) ni mwanasiasa mzuri. Wakati wa vita ni vita wote tushikamane twende mbele

Mpaka ananiandika SMS " Uwe na moyo mkuu, tuendelee kuchapa kazi". Ni wa Upinzani ila ni muelewa unajua yupo kwa ajili ya nchi.

Rais Magufuli: Kuna mwingine anazungumzia Dar wala hayupo Bungeni "Leo tumeahirisha kwenda Bungeni". ACHA!

Nimetoa maelekezo hakuna kuwalipa posho. Utalipwaje wakati huifanyii kazi? Usipoenda watakulipa hao mababeru wanaokutumia kuzungumza hayo unayotaka kuzungumza.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,180
2,000
M1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

M2.jpg

Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

m3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo ya Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

m4.jpg
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akizunguma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapishwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

m5.jpg

Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

m7.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

m6.jpg

Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,919
2,000
Of what benefit? Is this news worth paying attention to? What is strange with kuapisha? Of what exceptional leadership value Mwigulu is to arouse people's attention?

Ndio maana tunasema hakuna mwandishi wa habari and I do not have a good term to describe you so-called waandishi wa habari.

Mwandishi wa habari unasema Ikulu ya Chato? Does Ikulu ya Chato exist? This is a clear indication we run short of waandishi wa habari! Nisamehe Pascal kama hutapenda..
 

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Sep 5, 2019
508
1,000
Sasa kuapishana sasa hivi si ni hatari ? Huyu mbunge ametembea sehemu ngapi na amekutana na wangapi na tunajuaje kama jana tu au sekunde nne kutokea sasa hajakutana na mwenye huu ugonjwa ?

Nadhani hatuchukulii hili janga userious unaotakiwa...
Nimewaza hili jambo pia. Sijui wametumia njia ipi kukagua nyendo za MN maana juzi alikuwa bungeni hatujui kakutana na nani huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom