Kutoka bungeni: Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki

Kama spika karidhia ushauri wa chadema basi wale waliokuwa wanahonga kupata hizo nafasi wameumia. CCM nafasi kupungua hadi 7 kwa makundi yale imekula kwao..
 
Mwongozo wa Mnyika kuhusu suala la uwiano limewamaliza. Uchaguzi huu unapaswa kuzingati Gender,uwakilishi wa vyama .... n.k. Sasa, upinzani wanachukua viti viwili kwani hakuna kanuni inayosema wabunge nane watoke CCM kwenda kutuwakilisha huko EALA. Na kwa mujibu wa uwiano huo, Zanzibar nao kupewa nafasi yao, na wanawake nao kupewa nafasi yao.

Viva CDM kwa kuonyesha njia kwani haya ndiyo mliyokuwa mnayasimamia, mlipotoa kusudio la kwenda mahakamani kama Bunge letu lingeendeleza huu ukiukwaji na ubakaji wa demokrasia kwa kuipendelea CCM na kuipa nafasi nane. Na hapa ninaomba nimnukuu Mh. Mbowe alivyosema awali "….kule kuna vyama kama hapa Tanzania, walipunjwa viti kama tunavyofanyiwa, ninapenda ieleweke lengo si kwenda mahakamani, Spika pamoja na katibu wake, watatumia busara ili kulimaliza jambo hili bila kuadhirisha uchaguzi baada ya kuonekana una doa. Ni vema walau kati ya viti tisa, tungepewa viwili kutokana na uwiano wa vyama vyenye wabunge ili kuleta usawa na taswira sahihi,".
 
Spika anasema wapinzani wana nafasi zaidi ya mbili, haya ni maajabu yanayopatikana Tanzania tu, mbona hawakulisema hili tangu Mnyika alipowaandikia barua?
Kusikia kwa kenge huja baada ya kupigwa hadi kutokwa na damu maskioni. Magamba ni sawa na kenge.
 
nasikia komu anaendelea kugombea.
sijui atweza kujieleza jamani.
dah tumuombee jamani ajieleze vema.
 
nafasi zilizopo ni tisa kila chama kilitakiwa kufikisha majina ya wagombea wake, kwa mchanganuo wa jinsia,makundi maalum na lazima watoke kwenye vyama vya siasa.
 
nasikia komu anaendelea kugombea.
sijui atweza kujieleza jamani.
dah tumuombee jamani ajieleze vema.
Ni nani aliyekudanganya CCM huwa wanamsikiliza mtu anapojieleza, pesa zilishaongea usiku wa kuamkia leo, na nafasi kwa wapinzani waamuzi ni CCM ndio wao wameshaamuwa wampe nani, wanachosubili ni kui endorse tu.
 
Wagombea wa upinzani ni hawa ;

1. Antony Komu -CHADEMA
2.Twaha Tasilima - CUF
3. Danda Juju - NCCR -MAGEUZI
4.Nderakindo Kessy -NCCR -MAGEUZI
5.Apolisya Mwaiseje -NCCR-MAGEUZI
6.Fortunatus Masha - UDP
7.Mrindoko ...... - TLP
 
Ni matunda gani yatakayopatikana wakati Chadema hawakujiandaa na uchaguzi huu wa leo? hii ni mbinu mbaya sana aliyokuja nayo Makinda ila Balozi wa Uingereza yupo anawasanifu tu wanavyochemka!!

Source post yangu ya awali....imehaririwa!

Hili suala kama nilivyosema tangu awali tulihitaji kuchukua msimamo mkali juu ya hili.Tulitaka hata member states wa jumuiya ya EAC wajue kwamba Tanzania inayoongozwa na CCM haijawa fully commited katika jumuiya ambayo pre-conditions ni democracy,freedom.liberty and equity.Tulitaka jumuiya ya Afrika mashariki itambue kuna watu wanabaka demokrasia kwa maslahi yao.Tulitaka wajue kwamba muda wote Tanzania imekuwa ikipeleka wawakilishi bila kuzingatia matakwa ya kisheria,mahitaji ya jumuiya,watu wasioitakia mema Tanzania na jumuiya.Ni zao la uhuni na ghiliba.Kinachatikiwa ni decency na maslahi ya Taifa Mbele na maslahi ya jumuiya kwa mapana.

It is not just about winning an election: it is about restoring a sense of decency to our society and Region at large. It is about taking pride in, and respecting,ourselves as human beings and consciously internationalizing democratic values. Unless we do this, development and true freedom will forever elude us and talents will never flower in the land.

But if the answer is democracy, what exactly is the question? The question is: Why are we still not properly practicing it? And that is where CHADEMA comes in-to provide the missing link

kama ingeshindikana basi ingekuwa necessary kujitoa katika mchakato huu halafu tufungue kesi mahakamani.Kufungua kesi mahakamani ni kuwatendea haki watanzania kwani imani itakuwa imebaki katika taasisi za kidemokrasia ambayo Mahakama ni mojawapo
 
Back
Top Bottom