Heshima kwako mkuu,
Labda sijaeleweka kwako vizuri, au wewe ndio unashindwa kunielewa. Sijapinga alichosema Slaa nakiunga mkono sana, kufichua uovu ni sehemu ndogo sana ya kazi ya wabunge wote wa upinzani na walio chama tawala, lakini sio kazi pekee ya upinzani. Ninachosema ni kuwa upinzani kazi yao sio kulipua MABOMU tu, kama alivyokuwa akifanya Mrema, kuna mengi na makubwa ambayo yanaweza kuwa na manufaa zaidi, ya kutufanya watanzania tuwe na alternative government. Lakini Ni vigumu kuwa na watu ambao kazi yao ni kulipua mambomu tu na sio kutuambia strategies zao na policies zao za kufanya mambo kama hayo yasitokee tena. Kama kutakuwa hakuna mabomu ina maana Slaa atakuwa hana cha kusema, thus kwa maana hiyo finyu ya upinzani unayoifikiria wewe kutakuwa hakuna opposition! Elewa vizuri.
Kwa maana unayofikiria wewe wenye uzalendo wote walioko ndani ya CCM walioshiriki kufichua maovu yaliyoko ndani ya serikali ni wapinzani, au wasio wana CCM na waiso serikali walioshiriki nao ni wapinzania, hii si kweli.