jamani jana jioni nilipo rudi kibaruani kwangu na kujipumzisha sebuleni huku nikiangalia kipindi kutoka bungeni tbc1
mara nikamuona mzee mudhihir akichangia bajeti kwa maneno makali sana na akimtuhumu waziri hadharani na kumfananisha na joka la mdimu
anasema waziri huyo anakwamisha ujenzi wa kiwanda cha saruji jimboni kwake kisa ni yeye mudhihir maana akisikia waziri jina la mudhihir huwa kama aliekuwa na mimba anakuwa hajifai huhitaji ndimu na mbirimbi mbichi
kwa kweli vijembe na lugha za kuudhi zilikuwa nyingi hadi nikajiuliza kuna nn nyuma ya pazia tusichokijua
jamani jana jioni nilipo rudi kibaruani kwangu na kujipumzisha sebuleni huku nikiangalia kipindi kutoka bungeni tbc1
mara nikamuona mzee mudhihir akichangia bajeti kwa maneno makali sana na akimtuhumu waziri hadharani na kumfananisha na joka la mdimu
anasema waziri huyo anakwamisha ujenzi wa kiwanda cha saruji jimboni kwake kisa ni yeye mudhihir maana akisikia waziri jina la mudhihir huwa kama aliekuwa na mimba anakuwa hajifai huhitaji ndimu na mbirimbi mbichi
kwa kweli vijembe na lugha za kuudhi zilikuwa nyingi hadi nikajiuliza kuna nn nyuma ya pazia tusichokijua
kwa hiyo anaweza kuwa nani??hata mimi nilisikia, lakini alisema waziri wa mikoa ya kusini, siyo nyanda za juu kusini!
Hebo tueleze, imekuwaje akawa mwandosya?
Tena mwandosya ni prof siyo dr!!! Vipi mkuu, uko sawasawa??!
When you talk of a biased mind,mzigo mzito unambebesha unayemchukia!huyu jamaa jina la mwandosya limemkaa sana kichwani,
Mkuu Mtu wa Pwani, wewe ni mzoefu sana hapa jamvini, watu tunakutegemea sana, tutatarajia kupata full info sasa hii ya Prof. Mwadosya mbona haina mshiko? kwanin i usimtaje Hawa Ghasia (Lindi) au Bernard Membe (Lindi) (hawa ni Mawaziri wanatoka eneo jirani na majirani wa Mdhihir). Au waziri wa viwanda, mazingira nk.?
kwa hiyo anaweza kuwa nani??
Na mimi nilimsikia Mudhihiri na kwa kweli hakutaja jina la waziri yeyote kiasi kwamba Marmo akaomba mwongoza wa Spika akimtaka mbunge huy ataje jina la waziri kuliko kutoa blanket statement inayoonyesha mawaziri wote ni wabaya. lakini spika alikataza kutajana majinaMtu wa Pwani heshima mbele.
Kwanza mimi sikuwa na bahati ya kumsikiliza Mudhihir,pengine ningepata bahati ya kumsikiliza nisingekuwa na maswali.
Mkuu nashindwa kuelewa Dr/Pro Mwandosya anaingiaje katika sakata la ujenzi wa kiwanda cha saruji katika jimbo la mheshimiwa Mudhihir.Pengine ungesema waziri wa viwanda na biashara mama Mary Nagu ningekuelewa kidogo.
Mheshimiwa Mudhirir nadhani tayari kashaingiwa na kale kaugonjwa ka homa ya uchaguzi ndiyo maana anaongea pumba zake hana hoja ya msingi kwanza siku hizi wawekezaji ndiyo wanaamua wapi wanataka kuwekeza baada ya kuangalia sababu mbali mbali hasa za kiuchumi.
Uropokaji wa Mh Mudhihir uliwahi kumpa Unaibu Waziri enzi ya awamu ya tatu baada ya kumchambua vilivyo Mh Mrema. Mara hii nadhani ni masuala ya uchaguzi 2010.
Mradi upi wa Umeme? kwa ninavyo jua Stiggler Gorge kwa wakati ule ulikuwa mradi mkubwa saana kwetu na hizo Megawatts 3,000 tulikuwa hatuna mahali pa kuzitumia, lakini sasa ni wakati muuafaka. Reli iliondolewa au kungolewa kwa sababu ya kuanguka kwa zao la karanga kama sikosei etc, lakini pia ungeonyesha mwenyewe need ya kuwepo Reli huko kwa kuwepo production fulani ambayo wakati ule wa Mwl ulikwazwa kutokana na kutokuwepo kwa Reli infact Reli yenyewe ilikuwa inatoka Nachingwe kwenda bandarini Mtwara/Lindi kama sikosei.Hii ngoma ni nzito kuliko mnavyotaka kuijadili
jiulizeni kwa nini Nyerer alingoa reli ya kwenda kusini?
na kwa nini ule mradi wa hydroelectric ulihamishwa?
Na kwa nini wale wajaani walipokuja waliambiwa wakalime mpunga huko juu
acheni hizo mnajidai waTanzania lakini historia ya nchi yenu hamuijui..mind you humu kuna wanafunz wa UD ambao wana access to all sorts of data kuhusus hili suala
Mudhiri hapa anarudia story tuuu