Hakuna kitu kibaya kama kuishi zama za ujima kifikra huku kimwili upo 2021.Kenya,South Africa,Macedonia, Spain,Netherlands na France ni mojawapo ya Nchi duniani zenye mawaziri wa ulinzi wanawake.Hao wenye fikira hizo fikiria wamelelewa na mama zao na bado wana mawazo kama wanaishi miaka 100 iliyopita.Kinachoangaliwa ni uwezo wa mtu sio jinsia yake.Kuna wanaume wengi wameaminiwa kwenye nafasi kubwa kubwa na wamekuwa failure kiutendaji na kiuongozi. Karibu wauaji viongozi na madikteta wote ni wanaume lakini hakuna anayenasibisha uwezo wao mdogo na ukatili wao na jinsia yao.