Kuteswa kwa Kibanda: Kubenea aliumbua Jukwaa la Wahariri (TEF)

Status
Not open for further replies.
Emmanuel god be with us;if god be with us who will be against us?
 
mnaishia kumfariji kubenea jukwaani, mpelekeeni hela ya kula. tef ndo walishamtema hivyoo!. Sa si bora hata awe anahudhuria vikao vya tef apate bahasha, anajifanya ana misimamo!
 
Kubenea ni mwandishi asiyeyumba, anaandika anachokiamini kwa sababu anafanya uchunguzi na kupata uhakika wa habari anyoiandika. Mwanahalisi ni gezeti pekee ambalo liliandika hahari kuhusu 11 shame names na kuwataja kwa majina baada ya mkutano ule wa mwembe yanga. kwakweli nalikosa sana Mwanahalisi. Ila DR. kikwete asidhani kuwa ccm itatawala milele na hivyo kitakuwa kichaka chake milele!!!!1
 
Naomba mtu anihabarishe...hivi kiujumla waandishi wa habari wanaopitia humu JF wana mawazo gani? Umoja wa waandishi wa habari upo kweli? Ndugu zangu mkiwaacha hawa manyang'au yatambe tu iko siku yatawapata na nyie. Kalamu mnazo na kalamu ndizo silaha zenu...kazi kwenu.
 
yap!apo umenena coz ili suala linaonekana ni la kisiasa zaidi....ni lazima hatua ichukuliwe!!
 
kubenea mwenyewe ni mzigo kwa taifa, ina maana hapo anashangilia na kufurahia kibanda kuumizwa.........shame on him

Yaani wewe kwa uandishi huu lazima una zero...... Wewe ndie mzigo kwa taifa manake miaka yako minne umeipoteza bure kabisa....... Heri ungeimba bongo fleva sahizi ungekuwa mbali sana kimaisha........ Shame on you
 
Naomba mtu anihabarishe...hivi kiujumla waandishi wa habari wanaopitia humu JF wana mawazo gani? Umoja wa waandishi wa habari upo kweli? Ndugu zangu mkiwaacha hawa manyang'au yatambe tu iko siku yatawapata na nyie. Kalamu mnazo na kalamu ndizo silaha zenu...kazi kwenu.

Waandishi wa tanzania wengi wanapenda bahasha kuliko kalamu
 
Gazeti
la Mwanahalisi lilikuwa linamilikiwa na Saed Kubenea lilifungiwa miezi
kadhaa iliyopita kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi iosipokuwa tu
“uchochezi” – kufuatana na barua aliyoandikiwa na idara ya Maelezo.

Barua haikueleza ni “uchochezi” upi isipokuwa tu
inaaminika kutokana na habari gazeti lilikuwa likiandika kuhusiana na
kutekwa na kuteswa Ulimboka.

Mwanahalisi lilianza kufanikiwa kupata undani wa wa
kutekwa na kuteswa kwa mwanaharakati huyo kwani kidole kilianza
kuonyesha Ikulu kwa maana afisa mmoja wa usalama (TISS) ndiye mhusika
mkuu.

Baada ya kufungiwa Jujwaa la Wahariri (TEF)
lilimuona Kubenea ni “mkosaji” kwa kuandika habari zile na lilimtaka
akubali kosa kwa kuandika habari ambazo wengi wa wajumbe wa TEF katika
kikao kimoja waliona ni za “majungu” na wengine hata kudiriki kusema
Kubenea alikuwa anakwenda kinyume cha maadili ya uandishi.

TEF ilimtaka Kubenea ashirikiane na Jukwaa hilo ili
kumuombea kwa serikali gazeti lifunguliwe mradi tu kwanza akubali hilo
“kosa” lake.

Kubenea aliipuuza TEF kutokana na msimamo wake huo
wa ajabu na alikuwa anasusia vikao vyake.

Sasa hili la Kibanda limetokea ni kama lile lile la
Dr Ulimboka ikizingatiwa ile “pattern” ya tukio. Sasa sijui TEF
watawapinga wote wale watakaokuwa wanaandika habari kwa undani za
kuteswa kwa Kibanda kama habari hizo zinaonyeshea kidole wahusika ambayo
inaaminika ni wale wale waliomfanyia unyama Ulimboka?

Kwa maneno mengine ni kwamba iwapo wahariri
watagundua “ukweli” kuhusu kuteswa kwa Kibanda watatakiwa kufunga midomo
yao?

Kwa mtazamo wangu naona Kubenea amewaumbua sana TEF.

Nawasilisha

weka wazi kama unafaham waliotenda kwa mwanahabari huyu, unaweza kusaidia upelelezi na kukamatwa kwa watu hao kuliko kuandika au kulopoka, tunaomba kama unaundani halisi wa tukio hili tujuze.
 
nahisi humjui kubenea,huyu mtu wasomaji wa magazeti hasa yanayoandika makala na habari za uchunguzi tunamfahamu vizuri na tunajua umuhimu wake,kufungiwa kwa mwanahalisi bila kushitakiwa yaonyesha wazi udhaifu wa Serikali yenu.
 
Naomba mtu anihabarishe...hivi kiujumla waandishi wa habari wanaopitia humu JF wana mawazo gani? Umoja wa waandishi wa habari upo kweli? Ndugu zangu mkiwaacha hawa manyang'au yatambe tu iko siku yatawapata na nyie. Kalamu mnazo na kalamu ndizo silaha zenu...kazi kwenu.

upo sawa mkuu hawa waandishi hawana umoja njaa tupu kila mmoja ni shabiki wa wanasiasa basi kila siku wanamtukuza anaewapa bahasha
 
Hata ninyi mnaowatetea hawa wauaji kwa kupotosha ukweli msidhani mtakuwa salama, hata Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri wakati gazeti la Mwanahalisi linafungiwa hakukumbuka kuwa mwenzako akinyolewa na wewe tia maji. Wewe unamkumbatia nyuki unategemea nini?
 
Bravoo Kubenea na ziii UWT wa magamba mnatumia kodi zetu kutuangamiza, siku zenu zinahesabika.
 
Kubenea ni mwandishi asiyeyumba, anaandika anachokiamini kwa sababu anafanya uchunguzi na kupata uhakika wa habari anyoiandika. Mwanahalisi ni gezeti pekee ambalo liliandika hahari kuhusu 11 shame names na kuwataja kwa majina baada ya mkutano ule wa mwembe yanga. kwakweli nalikosa sana Mwanahalisi. Ila DR. kikwete asidhani kuwa ccm itatawala milele na hivyo kitakuwa kichaka chake milele!!!!1

Kubenea ni muislamu japo anaishi maisha kama ya yesu kwani pamoja na kejeli na mateso hakuyumba hadi alipouokoa ulimwengu
 
Kubenea ni muislamu japo anaishi maisha kama ya yesu kwani pamoja na kejeli na mateso hakuyumba hadi alipouokoa ulimwengu

kinacho waumiza waandishi wa habari hawana umoja. tatizo la mmoja wao sio lao wote. walianza sanifu hakuna aliyesema, wakaja mwanahalisi wakachekelea sasa wanafungia mmoja baada ya mwingine. ukila nyama ya mtu huwezi kuacha. ccm kufungia magazeti ni sana na wamekula nyama ya mtu. mia
 
mnaishia kumfariji kubenea jukwaani, mpelekeeni hela ya kula. tef ndo walishamtema hivyoo!. Sa si bora hata awe anahudhuria vikao vya tef apate bahasha, anajifanya ana misimamo!

unadhani ana njaa kama wewe gamba unayeishi kwa buku 7? kuwa imara njaa itakufanya upelekwe m.o.m.b.a.s.a
 
Yaani wewe kwa uandishi huu lazima una zero...... Wewe ndie mzigo kwa taifa manake miaka yako minne umeipoteza bure kabisa....... Heri ungeimba bongo fleva sahizi ungekuwa mbali sana kimaisha........ Shame on you

ni kweli bro,angeimba bongo fleva leo hii asingekuwa anajidharilisha kwa mgao wa buk 7 hapo lumumba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom