Gazeti la Mwana Habari lamrarua Kubenea

Chevi_masta

Member
Sep 13, 2021
11
15
Katika hali isiyo ya kawaida kwenye Gazeti la Raia Mwema linalomilikia na Sead Kubenea limekuwa na mwendelezo wa kuchafua viongozi mbalimbali wa Kiserikali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa kwa mfululizo pasipokuwa na woga wowote,lakini haishiii hapo hapo awali alishawahi mchafua pia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Ackson Tulia.

Kwa muendelezo huo wa taarifa za maksudi kabisa zenye lengo ya kuwachafua viongozi wakuu wa Serikali zimekuwa zikileta taharuki na mshangao kwa baadhi ya wadau wa Habari nchini,wanabaki vinywa wazi na kujiuliza kwa haya anayoyafanya Kubenea nyuma pazia kuna Nani ? ambaye anampa nguvu ya kutokuwa na uwoga wowote wakuheshimu viongozi wa mamlaka za juu kama Waziri Mkuu wa nchi na Spika wa Bunge la nchini.

‘Tumekuwa tukishangaa kuona Gazeti la Raia Mwema kuwa na mwendelezo wa kuchafua na kuleta taharuki kwa habari zisizokuwa na Ukweli lakini hakuna mahala tumesikia pia mamlaka husika zikimuonya mtu huyu kwa kuwa anachokifanya sasa ni uhuru uliopitiliza kwenye tasnia ya Habari nchini,ameanza na hao kwa kujiamini kabisa bila uwoga wa sura ya haiba itapelekea siku kumzushia habari zisizokuwa za kweli mpaka Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tanashauri kwa ustawi mzuri wa nchi na kwa manufaa makubwa ya Taifa letu huyu mtu akomeshwe tabia hii ya kuwaandika viongozi waandamizi wa nchi ambao kwa kiasi kikubwa tunaona uzalendo wao na kujitoa kwako pasipokujali itikadi za Kisiasa,kabila na udini kwa wananchi ili kufikisha Taifa hili katika kujitegemea kiuchumi na kuhakikisha huduma zote za kijamii zinawafikia takribani Watanzania wote kwa wakati’ alisema mdau

Kupitia mwandishi wetu na maoni aliyopokea kwa wadau tofauti wa Habari nchini,kwakweli kuna haja ya kutafuta suluhu ya maksudi na ya haraka kukomesha tabia hiyo kuchafua viongozi wa Serikali kwa taarifa za uongo na uchochezi ambazo zinazoweza kusababisha matabaka kwa baadhi ya Wazalendo wa nchi kwa kushindwa kuelewa maana uhuru huo wa mtu kujitokeza na kuchafua viongozi kwa taarifa za uongo ndio uhuru wa Habari ama ni Michezo michafu ya kisiasa nchini.

Rai yetu ni kufika ukomo wa tabia za kuandika taarifa za uongo ambazo hazina afya kwa Taifa kwenye Media mbalimbali yakiwemo magazeti na vyanzo vingine vya habari kwani nchi inahitaji ukweli na uwazi ili viongozi waendelee kuchapa kazi katika kujenga uchumi imara chini ya watu imara.

Cc. Mwhabari

IMG_20221111_062656_544.jpg
 
Waziri mkuu achafuliwe kwani ni msafi? Kiongozi anayeingia madarakani kwa wizi wa kura usafi autoe wapi? Au mnadhani mtu akishapata madaraka maana yake ni mtu msafi?
 
Back
Top Bottom