Kuteswa kwa Kibanda: Kubenea aliumbua Jukwaa la Wahariri (TEF) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuteswa kwa Kibanda: Kubenea aliumbua Jukwaa la Wahariri (TEF)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 8, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,408
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Gazeti la Mwanahalisi lilikuwa linamilikiwa na Saed Kubenea lilifungiwa miezi kadhaa iliyopita kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi iosipokuwa tu "uchochezi" – kufuatana na barua aliyoandikiwa na idara ya Maelezo.

  Barua haikueleza ni "uchochezi" upi isipokuwa tu inaaminika kutokana na habari gazeti lilikuwa likiandika kuhusiana na kutekwa na kuteswa Ulimboka.

  Mwanahalisi lilianza kufanikiwa kupata undani wa wa kutekwa na kuteswa kwa mwanaharakati huyo kwani kidole kilianza kuonyesha Ikulu kwa maana afisa mmoja wa usalama (TISS) ndiye mhusika mkuu.

  Baada ya kufungiwa Jujwaa la Wahariri (TEF) lilimuona Kubenea ni "mkosaji" kwa kuandika habari zile na lilimtaka akubali kosa kwa kuandika habari ambazo wengi wa wajumbe wa TEF katika kikao kimoja waliona ni za "majungu" na wengine hata kudiriki kusema Kubenea alikuwa anakwenda kinyume cha maadili ya uandishi.

  TEF ilimtaka Kubenea ashirikiane na Jukwaa hilo ili kumuombea kwa serikali gazeti lifunguliwe mradi tu kwanza akubali hilo "kosa" lake.

  Kubenea aliipuuza TEF kutokana na msimamo wake huo wa ajabu na alikuwa anasusia vikao vyake.

  Sasa hili la Kibanda limetokea ni kama lile lile la Dr Ulimboka ikizingatiwa ile "pattern" ya tukio. Sasa sijui TEF watawapinga wote wale watakaokuwa wanaandika habari kwa undani za kuteswa kwa Kibanda kama habari hizo zinaonyeshea kidole wahusika ambayo inaaminika ni wale wale waliomfanyia unyama Ulimboka?

  Kwa maneno mengine ni kwamba iwapo wahariri watagundua "ukweli" kuhusu kuteswa kwa Kibanda watatakiwa kufunga midomo yao?

  Kwa mtazamo wangu naona Kubenea amewaumbua sana TEF.

  Nawasilisha
   
 2. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2013
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  siku zote huwa namkubali kwa msimamo wake, hucmamia juu ya kile anachokiamini hata kama hakuna wa kumtetea, hatetereki hata kidogo
   
 3. Rockcity native

  Rockcity native JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 31, 2012
  Messages: 2,087
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kubenea ni jesh la m2 mmoja kama Anorld Schwatzneger
   
 4. T

  Taso JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,723
  Likes Received: 522
  Trophy Points: 280
  Hakupuuza, wala haukuwa "msimamo wa ajabu." Kuandika ushahidi wa maovu yanayodhaminiwa na Usalama wa Taifa na kukataa kuomba msamaha ni uzalendo, sio "msimamo wa ajabu!" Please!
   
 5. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  umewaza vyema.wengi wa hoa mabwana ni waoga na wanafiki wasio na msimamo.wnapaswa kujifunza ujasiri sasa kwani hata wasio andika za ulimboka wapo matatizoni sasa.wana adui mmoja ila kwa ujinga wanagawanyika
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,408
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Bushfire Umenena ukweli mtupu mkuu: TEF hamna kitu pale -- badala ya kuwa nyuma ya Kubenea kuibana serikali kuhusu kuteswa kwa Ulimboka, ilianza kumuandama Kubenea eti alikiuka maadili na hapo hapo 'watesaji" wakapata nguvu na hivyo kurudia vitendo vyao.

  TEF imebakia Jukwaa la kupokea bahasha za posho -- kutoka taasisi mbali mbali za serikali hususan NSSF. Ndiyo maana hatusomi habari negative za NSSF huku wakati kuna madudu mengi tu -- wanachama michango yao haipelekwi wakati NSSF inakaa kimya bila kuwachukulia hatua waajiri.

  Ufisadi wa mwisho kuusikia wa NSSF ni ule wa Magodown ya Ubungo na Manjni, tangu hapo hakuna kibaya kinachoandikwa dhidi ya taasisi hiyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani nani asiyejua ya kuwa jukwaa la wahariri nchini (TEF) linatumiwa na mafisadi. Acheni porojo Saed Kubenea ile ni number nyingine, ndo maana hata mafisadi pamoja na fedha zao za Uswis wameshindwa kumthibiti, na hivyo kubaki na option either ya kumuua au kulifungia gazeti lake kwa mda usio fahamika.
   
 8. k

  kinauche JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 7,685
  Likes Received: 839
  Trophy Points: 280
  Ina maana TEF haipendi habari za kiutafiti au?

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 9. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenikumbuka kampuni ya ki-fisadi ya Erolink ambayo haipeleki michango ya wanachama NSSF na hakuna wa kuigusa.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,408
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani hujaielewa vizuri sehemu ya nukuu (in red). "Msimamo wa ajabu" ni msimamo wa TEF, siyo wa Kubenea.
   
 11. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,639
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Unategemea Juma Pinto na Gazeti lake akae upande upi?vipi ulitaka wapinge wakati SACCOS ya TEF mtaji wake wa kuanzia walipewa na Ikulu,siku chache baada ya Mwana Halisi kufungiwa?Devide et Empire......Wagawanye na Uwatawale!
   
 12. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani Kubenea ni mfano wa kuigwa katika tasnia hii ya uandishi wa habari; Siyo siri nimemisi sana makala zake za ki-uchambuzi kama ile iliyosababisha gazeti lake lifungiwe "Aliyemteka Dk. Ulimboka huyu hapa ni Ramadhan Ighondu"
   
 13. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2013
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Yaani title ya thread yako na ulichokiandika ni mbuzi na manyoa ya kondoo.Kawa hadithia watoto wa form waliomaliza
   
 14. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,808
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  what goes around, comes around
   
 15. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 2,163
  Likes Received: 2,665
  Trophy Points: 280
  Kubenea big up.
  Uko sahihi kabisa mheshimiwa.
  Tatizo la sehemu kubwa ya Media ya Habari Tanzania imejaa unafiki na nidhamu za woga.
  Kuna wahariri wanaojikomba kwa serikali ili siku moja wapewe Ubunge wa kuteuliwa,u-DC au u-RC.

  Kuna matukio mengi sana yanayotokea hapa nchini ambayo yanahitaji uandishi wa kichunguzi ili kuweka wazi udhaifu wa serikali ya CCM lakini utakuta yanaandikwa juujuu tu kama vile hakuna kinachotokea. Issue kama ya Mwandishi wa CH10 Daudi Mwangosi aliyeuawa huko Iringa mwaka jana coverage yake ilikuwa very poor! Kupigwa na kumwagiwa tindi kali kwa Saidi Kubenea na kutekwa kwa Dr. Ulimboka hali kadhalika. Mwanahalisi peke yake ndilo lilianzisha uandishi wa kina kujua kulikoni na likafungiwa!!!

  Natamani Mwanahalisi lirejee ulingoni ili litupashe habari ni NANI YUKO NYUMA YA KUPIGWA NA KUJERUHIWA KWA ABSOLOM KIBANDA. Tayari Kibanda ameelezea watekaji wake walikuwa wanaitana AFANDE!!!Sasa hii Afande ni ya Jeshi gani????Hapa ndipo pa kuanzia. Lakini hatuna waandishi ambao wako tayari ku-risk kazi zao na vyombo vyao kwa uchunguzi wa habari hii!!!!!!!

  Shame on you waandishi makanjanja,wanafiki na wenye kujikomba.
   
 16. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,918
  Likes Received: 44,768
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusikie leo watatoa tamko gani.
   
 17. W

  Waambi JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 736
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TEF imejaa wapuuzi watupu. Kazi kumlamba miguu Dr Dau na Eriyo ili wapewe bahasha. Si kundi la professionals bali wanafiki na wenye njaa. Ni aibu tupu!! Wahariri wenye heshima zao si wanachama.
   
 18. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2013
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,135
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Adui wa Watanzania ni unafki. Miezi michache iliyopita Absalom Kibanda aliitwa mnafki na Baadhi ya Memba JF humu JF kisa tu kaamua kujiunga kwa muajiri wakidai si mwenye msimamo leo wanajifanya eti kafanyiwa mbaya kwa sababu ya msimamo usioyumba Mjifunze kuacha kulaumu watu na kufanya Political analysis bila ya kuwa na utaalamu!
   
 19. Wiyelelee

  Wiyelelee JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2013
  Joined: Nov 9, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Kubenea walisema ameiumbua Swirikali. TEF walionekana malaika, na yakampata Kibanda. Sasa waandishi waandike nini?
   
 20. hugochavez

  hugochavez JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 1, 2013
  Messages: 1,724
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 180
  kibanda ameteswa na waajiri wake wa mwanzo ambao hakuagana nao vizuri baada ya kuacha kazi kwao
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...