Sufian Juma, pole kwa yaliyokukuta.
Sintaongea juu ya kutenguliwa wadhifa wako kwa kuwa siifahamu Katiba wala Kanuni za ACT.
Umesema hukujua kama ni kosa 'kumpongeza JPM kwa juhudi alizochukua kuikabili Corona'.
Naomba nikuulize swali.
Kwa nini JPM anasema tufuate maelekezo ya Wataalam wetu wa Afya wakati Wataalam wenyewe wamepigwa marufuku kuuelimisha umma?
Profesa Mohamed Janabi aliongea mambo yenye manufaa sana juu ya janga hili, kilichofuatia alinyamazishwa mpaka zikaenea tetesi za kufukuzwa kazi.
Uliyemtakia kheri, Mwigulu, amesikika akisema Corona iwe siri ya Taifa.
Je, ni kweli kheri hiyo uliitoa wewe mwenyewe, ukiwa na akili timamu, bila kushinikizwa na mtu yeyote, au kitu chochote?
Sufian, ninaomba majibu