Kutenguliwa Uafisa Habari ACT-Wazalendo

Kutenguliwa Uafisa Habari ACT-Wazalendo

Heb
Hebu tuonyeshe hapa bandiko lako ukilosifia ACT au chama tofauti na lumumba a.k.a utopolo fc!!!. Ukiwa kwenye mapambano huwezi kumsifia adui yako.
Sasa islamic brotherhood of Tanzania unaweza kuwasifia? Mtu unasifia chama kinachofanya mazuri kama kuhamasisha umoja na uzalendo. Kusimamia vizuri ilani yake n.k
 
Umewahi kuona Lumumba buku 7 (LB7) wakisifia ACT humu !!?

Hukuwa mtu sahihi kupata hicho cheo kwakweli tena umejidhalilisha mno na umemdhalilisha aliekuteuwa pia!

Njoo LB7 uunge juhudi.
 
Ulikwishaona Polepole akiisifia ACT? Chukuwa kadi ya CCM na endelea kusifia upuuzi wa kujipuliza mvuke, mapapai kuwa na corona, nk.

The guy is extremely dumb. Natarajia hata huko CCM kuna waajiri makini wanaojua “publicity official” aliyekosa common sense kabisa.

Ajiulize kwa nini Polepole hathubutu kutoa zile kauli zake mahsusi za kweli kuhusu CCM alizokuwa akitoa enzi akiwa “mwanaharakati huru”. Badala yake anaongea kinyume chake ilhali hajazikanusha rasmi.
 
KUHUSU KUTENGULIWA UAFISA HABARI ACT WAZALENDO.

Mimi Suphian Juma, ninashukuru kwa fursa niliyopewa ya kuwa Afisa Habari na nina uhakika nimejitahidi kufanya kazi kubwa ya kuiweka ACT Wazalendo mahala panapostahili kwenye Mitandao ya Kijamii na hata nje ya mitandao ya kijamii si tu tangu nilipoteuliwa nafasi hiyo bali pia mara tu nilipojiunga na Chama cha ACT Wazalendo Mwaka 2015.

Nimetambua kuwa ni kosa kuanzisha mijadala inayoendana na kile ambacho Serikali inasimamia au kufaulu, ni kosa kuanzisha mjadala kwa ku-post barakoa yenye Maandishi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ni kosa kumtakia kheri Waziri Mwigulu Nchemba baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli na vivo hivyo ni kosa kumpongeza Rais Magufuli kwa Hatua kadhaa alizochukua dhidi ya janga letu sote kama Taifa la Corona, maana vyote hivi ndivyo vilivyozua mijadala katika mitandao ya kijamii.

Kiufupi ni kosa kuanzisha mijadala yenye agenda zilizoanzishwa na vyama vingine nje ya ACT wazalendo ikiwemo CCM na CHADEMA kama nilivyofanya mara kadhaa kupitia kurasa zangu "binafsi" za mitandao ya kijamii hata kama mijadala hiyo ina manufaa kwa Taifa.

Hivyo, nimepokea kutenguliwa kwangu kama Afisa Habari wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa kwa moyo mkunjufu na hivyo nitandelea na uhuru wangu wa kujadili mambo yenye manufaa kwa Taifa langu kwenye kurasa zangu binafsi kama mwanachama wa kawaida wa ACT Wazalendo na kama Mtanzania mpenda Tanzania yake.

Aidha kipekee nawashukuru Waandishi wote wa Habari na Vyombo vyao, wanachama wenzangu, Viongozi wa Chama pamoja na Watanzania wote walionipa ushirikiano uliotukuka katika kipindi chote nilichohudumu kama Afisa Habari wa ACT Wazalendo. Nawaomba ushirikiano huo wampe pia atakayeshika kijiti hiki nilichokuwa nacho.

Aluta Continua, Daima Taifa Kwanza Leo na Kesho.

Suphian Juma,
Mei 03, 2020.
View attachment 1438783

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kwa husuda uliyofanyiwa na wanaojiita wazalendo, hongera kwa kusimamia maslahi ya Taifa na uzalendo kwa Nchi yetu. Demokrasia na uhuru wa kweli upo CCM, karibu tushirikiane kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom