Kutenguliwa Uafisa Habari ACT-Wazalendo

Kutenguliwa Uafisa Habari ACT-Wazalendo

Suphian Juma

Senior Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
140
Reaction score
579
KUHUSU KUTENGULIWA UAFISA HABARI ACT WAZALENDO.

Mimi Suphian Juma, ninashukuru kwa fursa niliyopewa ya kuwa Afisa Habari na nina uhakika nimejitahidi kufanya kazi kubwa ya kuiweka ACT Wazalendo mahala panapostahili kwenye Mitandao ya Kijamii na hata nje ya mitandao ya kijamii si tu tangu nilipoteuliwa nafasi hiyo bali pia mara tu nilipojiunga na Chama cha ACT Wazalendo Mwaka 2015.

Nimetambua kuwa ni kosa kuanzisha mijadala inayoendana na kile ambacho Serikali inasimamia au kufaulu, ni kosa kuanzisha mjadala kwa ku-post barakoa yenye Maandishi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ni kosa kumtakia kheri Waziri Mwigulu Nchemba baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli na vivo hivyo ni kosa kumpongeza Rais Magufuli kwa Hatua kadhaa alizochukua dhidi ya janga letu sote kama Taifa la Corona, maana vyote hivi ndivyo vilivyozua mijadala katika mitandao ya kijamii.

Kiufupi ni kosa kuanzisha mijadala yenye agenda zilizoanzishwa na vyama vingine nje ya ACT wazalendo ikiwemo CCM na CHADEMA kama nilivyofanya mara kadhaa kupitia kurasa zangu "binafsi" za mitandao ya kijamii hata kama mijadala hiyo ina manufaa kwa Taifa.

Hivyo, nimepokea kutenguliwa kwangu kama Afisa Habari wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa kwa moyo mkunjufu na hivyo nitandelea na uhuru wangu wa kujadili mambo yenye manufaa kwa Taifa langu kwenye kurasa zangu binafsi kama mwanachama wa kawaida wa ACT Wazalendo na kama Mtanzania mpenda Tanzania yake.

Aidha kipekee nawashukuru Waandishi wote wa Habari na Vyombo vyao, wanachama wenzangu, Viongozi wa Chama pamoja na Watanzania wote walionipa ushirikiano uliotukuka katika kipindi chote nilichohudumu kama Afisa Habari wa ACT Wazalendo. Nawaomba ushirikiano huo wampe pia atakayeshika kijiti hiki nilichokuwa nacho.

Aluta Continua, Daima Taifa Kwanza Leo na Kesho.

Suphian Juma,
Mei 03, 2020.
IMG-20200503-WA0050.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Tuone Na Wengine Nao Wafanye
Kazi Kubwa Sana Ipo Muhimu Endelea Kuunga Mkono Juhudi Za Chama Chako
 
Sawa Mkuu, nimefurahi kuona huna chuki wala kinyongo.

Kilicho sahihi na chenye manufaa kwa Watanzania wote, endelea kukisimamia hichohicho kwa uadilifu mkubwa.
 
Sawa Mkuu, nimefurahi kuona huna chuki wala kinyongo.

Kilicho sahihi na chenye manufaa kwa Watanzania wote, endelea kukisimamia hichohicho kwa uadilifu mkubwa.
Kwa hiyo barua nilivyoisoma tayari inaonyesha kinyongo, hakupaswa kusema katumbuliwa sababu ipi ila kaongelea kuonyesha km vile kaonewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulifanya kosa kusifia upuuzi wa chama kingine hata kama ulikuwa nje ya page za chama chako. Huwezi kuona manager wa kitengo chochote cha Samsung anaisifia au hata kuijadili Huawei mbele ya watu. Mijadala hiyo ni confidential na inatakiwa kufanyika nje ya macho ya watu. Lini uliona Polepole anajadili mafanikio ya CUF? Sijui walikuokota wapi, tena cheo cha Afisa Habari unatakiwa uepuke makosa kama haya.
 
Huo mfao ni mufu. Hata hoja ya msingi ni maslahi ya taifa. Kama mtu anasifia kitu kwa maslahi ya taifa hakuna tabu kabisa.
 
Back
Top Bottom