Kutengeneza bisi (pocorn)kwa mashine

Kutengeneza bisi (pocorn)kwa mashine

😹😹😹 Marhaba
Mashine lote hilo ununue kwa kutengenezea bisi za kula, kibongo bongo hajatukamata 🤣
Ah lakini inawezekana tu mbona, mimi ninalo ndani lilibaki baada ya kuacha hiyo biashara, japo sina uzungu wa kununua mahindi ya bisi nikachoma.

Pia watu wanayo kibao tu hasa wale waliowahi kununua kwa kufata mkumbo, hivyo sio ajabu akalipata kutoka hata kwa ndugu.
 
kwanini uliacha biashara? ulikuwa unatumia machine ya umeme au ya gas?
 
Usichemshe kwanza mafuta kisha uweke mahindi ya bisi, weka vyote kwa pamoja (mahindi na mafuta).

Japo situmii machine, ukiweka mafuta yachemke kwanza halafu uweke mahindi, yanaungua, kwa uzoefu wangu mdogo
 
Najaribu kutengeneza bisi kwa popcorn mashine lakini sifanikiwi nyingi zinauungua tu,naweka mafuta kwenye kichombo,yakichemka naweka bisi,sasa shida ni kwamba chache zinapasuka vizuri ila. nyingi zinaungua.Naomba mwenye ufahamu juu ya hizi mashine zinavyofanya kazi anifundishe nifanyeje.Ni zile mashine kubwa ambazo hutumiwa na wafanyabiashara wa popcorn hii yangu ni mr uk
Ushahidi wa picha
 
Leo Shida ipo wapi mkuu?
Leo sijatengeneza,ila shida ipo kila nikichoma nusu zinaungua na nusu ndio zinapasuka,nimejaribu njia mbili:
1.nilitanguliza mafuta yakapata moto ndio nikaweka bisi
2.Niliweka bisi na mafuta kwa wakati mmoja lakini njia zote hizo matokeo ni yaleyale
 
Mkuu kama maelezo niliyokupa pale juu yamefeli, itabidi tuongee kwa kutumia simu, wiki hii niko bize siwezi kuandika maelezo marefu, kwa sababu kuna vitu naandika kwenye simu, humu jf huwa nakuja nachungulia na kujibu comment za wadau kisha nazama tena.

Ila unaweza kuchagua kimoja kati ya hivi.
👇
1. Nipe kama siku mbili hivi nisajili namba maalum kwa ajili ya kuongea na wewe.

2. Subiri kama wiki hivi nitafungua uzi kabisa nitaweka heading JIFUNZE KUCHOMA POPCORN KWA KUTUMIA MASHINE ili wadau wengine pia wajifunze.
 
Back
Top Bottom